Nabii kiboko ya wachawi, naona anafanya maigizo

Only in Christian
 
Mlishaonywa jihadharinina mbwa mwitu wenye kuvaa ngozi ya kondoo...

Mungu yupi na ufalme wake hutekwa na wenye nguvu (sio mabaunsa), bali wale waliopigana vita na muovu na kumshinda...

Mtu mpumbavu ataiambia nafsi yake ya kwamba hakuna Mungu wala Kristo, itoshe kusema wote waliompokea aliwapa uwezo kuwa wana wa Mungu, wale tu waliaminilo jina lake...
 
Haya maigizo alijaribu kunichezea nabii flora wakati naingia Dar akachemka
Nilipelekwa bwana na rafiki yangu mmoja nikiwa Binti nasoma chuo,kipindi hicho alikuwa njia ya kuelekea Salasala,nilimshangaa sana mavazi yake,nywele zake,alivyojichubua sasa,aliponiacha hoi ni Ile lipstick nyekunduuu kama damu halafu akatoa lipstick pale mbele akakolezea,,,Huwezi Amini sikuendelea na ibada nikitoka zangu nje nikamsubiri mwenzagu alivyotoka nikamsema sana,,,nilikuwa namsema mpaka akaacha kwenda....nashangaa watu wanamshagaa Zumaridi wangemuona flora ndio wangeshangaa vizuri
 
Wakristo tunahitaji macho ya rohoni,na kusoma neno na kulitafakari
 
Yaani watu tumekuwa wakupenda muujiza,Hadi imefika mahali hii muujiza unaona kabisa ni scene zinetengenezwa,,,kama hii nilivyoisikiliza Jana ni full maigizo yenye comedy ndani yake....maana huyo mchawi kabana sauti aonekane ni Mzee yaani ni huzuni....Yesu asaidie kanisa
 
Mfano mdogo, hii mada yako hapa kwa kiasi fulani imeleta mashaka kwenye maswala ya wokovu, wale waliokua wanapingana na wakovu wanazidi kupata paku simamia
Ni Kweli inaleta ukakasi,lazima wajue kuchagua mbivu na mbichi ndio maana ukiangalia mwisho wa mada nimeweka mstari wa neno la Mungu kama muongozo
 
Ni Kweli inaleta ukakasi,lazima wajue kuchagua mbivu na mbichi ndio maana ukiangalia mwisho wa mada nimeweka mstari wa neno la Mungu kama muongozo
Naomba kuuliza joannah kama hutajali, mimi ni mkristo naamini katika Kristo.
Hayo yote yanafanyika kama ulivyoelezwa kwenye mada hii.
Udanganyifu upo mwingi, miujiza feki, matukio ya kupangwa au kuigiza huko makanisani na matukio yote mabaya ambayo kwa ujumla Mungu hapendi.
Sasa ni kwanini Mungu anaruhusu hayo, ipi faida ya uwepo ya hayo, hamna namna inaweza kupunguza mambo kama hayo?
Najifunza lakini .
 
Wagalatia mazuzu acha watapeliwe,ukiwasanua watakuambia ww kobazi
 
Kwa upeo wangu,Mungu amempa kila mmoja wetu akili na utashi, uwezo wa kuchagua mambo mema na mabaya,amekupa ruhusa ya kuchagua upande unaoutaka....ndio maana anaruhusu Haya Ili wewe Binafsi uchague lililo Jema .....kama wakristo tuna kila sababu ya kujifunza kumjua sana Mungu na kuyatenda Mapenzi yake,na kuzishika amri zake bila kuyumbishwa na manabii fake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…