Nachingwea, Lindi: Mwanamke wa miaka 28 ajiua baada kuchepuka

Nachingwea, Lindi: Mwanamke wa miaka 28 ajiua baada kuchepuka

Watanzania wengi ni watoto wa nje ya ndoa ndo maana kuchepuka wanaona sio kosa
 
Mwanamke anayeitwa Salma Shaibu(28) amefariki dunia Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi baada ya kujiua kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu chanzo kikidaiwa ni kujihisi mwenye hatia baada ya kukiri mwenyewe kabla ya kujiua ya kuwa alichepuka na Mwanaume mwingine.

Salma ambaye ameacha Watoto wawili akiwemo mkubwa ambaye anasoma elimu ya awali, enzi za uhai wake alikuwa akiishi na Mumewe Ramadhan Hamisi Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na akasafiri kwenda Wilayani Newala, Mtwara ambako alishawishika na kuingia kwenye mahusiano na Mwanaume mwingine, na baada ya kurudi nyumbani kwa Mumewe Masasi, Salma hakuwa mwenye furaha kwakuwa nafsi ilikuwa inamsuta.

Salma aliamua kumsimulia Rafiki yake wa kike na Mdogo wake na wote walimpa moyo na kumwambia akae kimya kwani jambo hilo akilisikia Mumewe linaweza kuzua balaa lakini aliendelea kuonekana mwenye simanzi mpaka Mumewe akahisi tofauti na kuumuliza Rafiki wa Mkewe ambapo alimsimulia kila kitu lakini Mume huyo hakukasirika na alisema ni jambo la kawaida na akamwambia Mkewe asiwe na wasiwasi.

Licha ya kusamehewa na Mumewe Salma hakuwa na amani na akaaga kwenda Wilayani Nachingwea kumsalimia Baba yake aliyekuwa mgonjwa ambako alikaa siku mbili na kuamua kunywa sumu kali ya kuulia wadudu kwenye mikorosho na kuacha na karatasi yenye ujumbe unaosema “NIMESHINDWA KUISHI KWA MAKOSA YANGU MWENYEWE” huku mkononi mwake akiwa ameandika ujumbe ambao unaendana sawa na maneno aliyoyaandika kwenye karatasi na kusisitiza sio tatizo la yeyote bali ni ujinga wake na kujihisi ameikosea Familia na Mungu wake.

Baada ya Mwili wa Marehemu kufikishwa kwenye Hospitali ya Mnero, imebainika ya kuwa alifariki baada ya sumu aliyokunywa kuathiri zaidi viungo vya ndani ya mwili na mfumo wa upumuaji, RPC wa Lindi Pili Mande, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa vijana kushirikisha Watu mbalimbali masuala yanayowasibu na kupata ushauri namna ya kutatua huku akiwaelekeza kutumia dawati la jinsia la Jeshi hilo kuelezea changamoto mbalimbali za kisaikolojia na mahusiano ili kupata msaada na kuepusha maamuzi magumu ya kujiua.
Kamba
 
Mume alijibu kirahisi mno kitu ambacho sio kawaida kwa mwanaume,inawezekana alijua kuna siku isiyo na jina mumewe angemgeuza asusa,akajiwahi.

Mtu anayejibu kirahisi hivyo ni wa kuogopwa
na huu ndio ukweli!

Unajisikiaje pale unapotukana mtu, alafu akakujibu kwa upole?? Utahisi hatia hatia!

Mwanamke akifanya kosa kama hilo, anatarajia kuadhibiwa,kuonywa au kuachwa!

Kama utaujua ukweli, na usipofanya hata mojawapo kati ya hayo, umemwacha ajihukumu mwenyewe!
 
na huu ndio ukweli!

Unajisikiaje pale unapotukana mtu, alafu akakujibu kwa upole?? Utahisi hatia hatia!

Mwanamke akifanya kosa kama hilo, anatarajia kuadhibiwa,kuonywa au kuachwa!

Kama utaujua ukweli, na usipofanya hata mojawapo kati ya hayo, umemwacha ajihukumu mwenyewe!
Ni kweli kabisa,angepewa adhabu angeridhika ila kitendo cha kuachwa kilimletea hatia moyoni akaamua kujitafutia adhabu
 
In reality haileti sense sana, waangalie asije kua alipewa sumu watu wanatafuta pa kutokea
Wamakonde wachawi sana

usije ukakuta Jamaa alinyunyuzia akamla Marehemu bila ya kujitambua …akili ziliporudi nafsi ikamsuta sana


kuna DHRA mmoja namfahamu analiwa ma Dalali wa Magari wa katikati ya Jiji ambae ni Mmakonde

Kamtengeneza yule Mkurugenzi wa rasilimali watu hadi wakati mwingine anapigiwa Simu na Mke wa dalali akiwa na shida anamsaidia hata kumpa fedha na hivi sasa Dalali anajengewa nyumba na yule Mama Mkurugenzi kwny kiwanja cha Mkewe wa ndoa



Ukiona Binti yako ana chenji halafu anazengewe na marioo wa Kimakonde andika DP world imeingia kwny ukoo wako
 
Back
Top Bottom