Nachukia kupigiwa simu halafu mtu anadai eti amekosea namba

Nachukia kupigiwa simu halafu mtu anadai eti amekosea namba

Makinisanatu

Member
Joined
Mar 5, 2023
Posts
32
Reaction score
21
Kwa wale wenye familia na ambazo huwezi kuona namba mpya ukaipuuza kutokana na watoto na familia pale uwapo nje au safari. Eti unaona mtu ana beep🎼📞. Sometimes anakutext kabisa. Kuwa ...."Nipigie."

Nachukia sana tena anaandika nipigie...heck. Unapiga anadai eti nimekosea namba.

Mimi: Uwe makini.

Yeye: Si nimekwambia nimekosea namba mwehu nini!

Mimi: (Nashangaa)....wewe mdada unashida gani?

Yeye: Mshenzi wewe.

Wadau huyu anatakiwa afanywe nini?
 
Jana nimepigiwa na demu ana sauti nzuri sana anaulizia iphone 12. I am married ila nisingekuwa married ningeendeleza mawasiliano. Ila unaweza dhania anafanania na sauti yake kumbe ki kibonge flani hivi mwepesi 😃
Hebu kwanza ni wewe kumbe 😀😀😀😀
 
Juzi nilipewa namba na demu, kumbe nilikosea kuandika. Nikapiga hapokei, nikatuma sms akajibu "unasemaje" nikamnyookea kama Carlos The Jackal naomba nikupige mashine. Kumbe ni jamaa yuko Moshi. Jamaa akapiga simu anatetemeka na lafudhi ya kichaga. Tukayamaliza kiume.

Kinachomuuma mleta mada anaweza kuwa aligawa namba, sasa anasubiri simu kwa hamu. Halafu anapiga msukuma kakoses
 
Wasukuma sijui wanakuaga na shida gani jamani, wanaweza wakakosea watu watano kupiga wanne wote ukiuliza uko wapi? mwanza,geita
Na ukimwambia amekosea namba anaanza kukuuliza kwani uko wapi na unaitwa nani
 
Juzi napokea simu namba ngeni, ni masai nkimwambia umekosea namba ni mbishi haelewi, kang'ang'ana ni wewe , nlikasirika adi nkamblock
 
acha wakosee tu, bira makosa hamna usahihi. fanya ivi_ set simu yako kwenye condition kwamba namba ngeni inakua auto rejected that is [a_z]
 
acha wakosee tu, bira makosa hamna usahihi. fanya ivi_ set simu yako kwenye condition kwamba namba ngeni inakua auto rejected that is [a_z]
Kwa hiyo mtu ambaye hana namba yako hawezi kukupigia? Unaishi wapi ndugu yangu?
 
Back
Top Bottom