Nachukizwa sana na baadhi ya watu wanye tabia ya kukata tamaa

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Salaam kwa wote,

Ni kweli maisha yana changamoto nyingi hilo halina ubishi, Pia ni kweli tumeumbwa kila mmoja na uwezo wake wa kukabiliana na changamoto za maisha.

Point yangu ya msingi ni kuwasihi watu wenye tabia ya kukata tamaa haijalishi unapitia chagamoto gani, iwe ni magonjwa, changaoto za kiuchumi nk.

Kamwe usikate tamaa, pambana hadi kieleweke, jipe moyo wewe mwenyewe, unajikatisha tamaa unadhani nani anaeweza kukutia moyo kama siyo wewe mwenyewe?

Nawakubali sana watu wenye ujasiri wa maisha, mtu anaumwa lakini anasema Mungu atanisaidia nitapona, Mtu hana kazi lakini anasema ntaendelea kumuomba Mungu, sitakata tamaa najua iko siku ntapata, Mungu ni mwaminifu anaona juhudi zako, atakupa hitaji la moyo wako. mfano mzuri mimi mwenyewe nilipita changamoto ya kukosa kazi kwa muda mrefu, niliomba kwa bidii huku naendelea kutafuta kazi, japo nilikatishwa tamaa lakini sikukata tamaa, mwisho wa siku nilipata kazi ambayo nilitamani kuipata na ina maslahi mazuri.

Sikusaidiwa na ndugu wala rafiki, ni mimi na Mungu wangu. Jinenee maneno ya ujasiri kwa mfano, Kwa uweza wa Mungu nitapona, nitapata kazi, nitajenga, nitakuwa tajiri nk, kumbuka kinywa kinaumba.

Ndugu zangu hakuna kitu kinapatikana kirahisi hapa duniani, kila kitu kinapatikana kwa juhudi na kutokukata tamaa, Pambana, wahenga walisema mgaa gaa na upwa hali wali mkavu.

Ukikata tamaa utayachukia maisha na hutaona thamani yako katika hii dunia.

Nb. Mungu kwanza mengine yanafuatia.
 
Huenda ujumbe haunihusu ila muombe sana Mungu usipite katika bonde la maumivu hasa ya ugonjwa au umaskini yes hupaswi kukata tamaa ila huwa sio rahisi
Nakuelewa sana mkuu na nimepitia msoto sana lakini kutokukata tamaa kumefuta maumivu yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…