Nachukua mkopo CRDB nianze biashara ya nafaka(mpunga na mahindi)

Ibra ruge chabenzi

New Member
Joined
Aug 26, 2018
Posts
4
Reaction score
17
Wadau Mimi ni mtumishi wa afya, mshahara wangu unaniruhusu kukopa mil 15.

Nataka nikope mil 15 niwe nakatwa kwenye mshahara Kwa miaka sita, Nichukie mil 10 niingie kwenye mpunga na mahindi. Silimi nafuata Kwa wakulima naweka store.

Nasubiri yapande niuze wakati mkopo unakatwa kwenye mshahara.

NAJIONA NIKO SAHIHI,PLEASE KAMA KUNA MKOSOAJI ANISAIDIE
 
Kama hujawahi fanya biashara hiyo na kujua changamoto zake, sikushauri kuchukua mkopo na kuanza hiyo biashara.

Mkopo huwa ni kwa ajiri ya kuimarisha/kukuza/ kuendeleza biashara ambayo tayari ipo.
 
Mimi naona uko sahihi.Inabidi ununue kwa wakulima siyo kwa wachuuzi.Wachuuzi watakuchanganyia mambo meusi
 
Hii biashara ni kama kamari flani yenye low risk, ukiwa mvumilivu unaweza kupata faida ila mambo sio rahisi kama unavyodhani, wakati gunia la mahindi sasa hivi likiuzwa 40k Kuna ambao wanayo ya mwaka jana walionunua 70k wakisubiri Bei ipande
 
Hiyo biashara unayotaka ina turnover ndogo (mzunguko) wakati makato yake ni kila mwezi. Yaani kuna miezi mingi itakuwa inapita ukiwa umezika hela.

Pia biashara yako inategemea kama kubeti, kwamba kuna nafaka zitapanda bei na hujui ni bei kiasi gani wala huwezi kadiria sababu siasa zinaweza fanya price fluctuation.

Kama unataka hio biashara fanya savings uianze kwa hela yako na sio ya mkopo. Badala ya kukopa 10M basi kopa hata 2M ongezea na hela yako mwenyewe kiasi chochote ulichonacho uone kwa vitendo. Sio unajilipua mkopo wa muda mrefu kwenye biashara hujawahi fanya.
 
Ataanza vipi sasa na atajifunza lini? Mi naamini kwenye falsafa ya kufeli ni Bora kuliko kutojaribu
Falsafa ya kiwendawazimu. Mfano mtu auze nyumba akafanyie biashara hela yote ili akifaulu awe tajiri na akifeli awe mlalahoi. Endapo amekuwa mlalahoi umwambie ni bora kuliko alivyokuwa na nyumba.

We unaona kuna matumizi ya akili hapo?
 
Kama hujawahi fanya biashara hiyo na kujua changamoto zake, sikushauri kuchukua mkopo na kuanza hiyo biashara.

Mkopo huwa ni kwa ajiri ya kuimarisha/kukuza/ kuendeleza biashara ambayo tayari ipo.
Umemaliza , ZINGATIA HAYA MAELEZO
 
Hiyo biashara inahitaji uzoefu wa mazingira na hali ya hewa, niliwah kununua mahind kg 1 Tsh 700 nikaweka kwenye kinga njaa nikaweka store ilikuwa mwezi wa 5 imefika mwezi wa 9 nikaotea tu kuwa nikisubir mwez wa 10 had 12 yataletwa yale mahind ya msaada ya serikal yanauzwa 900 kwa kg 1 basi nikauza yangamu mwezi wa 9 kwa 1200 kwa kg 1 na yameisha tu ya 900 yakaingia mpak wengne wakajilaum kwanin walinunua kwangu sasa uxipokuwa mzoef unaweza nunua gunia 70 elf ukauza 40 elf
 
Falsafa ya kiwendawazimu. Mfano mtu auze nyumba akafanyie biashara hela yote ili akifaulu awe tajiri na akifeli awe mlalahoi. Endapo amekuwa mlalahoi umwambie ni bora kuliko alivyokuwa na nyumba.

We unaona kuna matumizi ya akili hapo?
Basi aendelee kutegemea mshahara maisha yake yote alafu akija kustaafu aje kulilia kikotoo Cha serikali

Chukua mkopo calculate risk ya biashara yako, wekeza 40% kwanza huku ukisoma mchezo, Hio 60% una integrate taratibu kutokana na mwendo wa biashara, maisha haya bila uthubutu utasindikiza watu maisha yako yote
 
Uzi ufungwe hapa.
Kama mtu Hana mtaji wa kufanya biashara, let's say na mshahara unakuta umebana kwenye matumizi yake na familia, mnamshauri Nini akitaka kujikwamua, wabongo bana, ukichukua mkopo kununua gari ya kutembelea(liability) watu Wanaona poa tu ila huyu anayetaka kuanza biashara mnamkatisha tamaa, mleta mada usiogope, hata mo juzi kasema anadaiwa zaidi ya bilioni 500 licha ya kua ndo tajiri namba 1 nchini
 
Umeongea ukiwa hali ya kawaida au jazba? Hebu relaaaax
Afu tafakari upyaa.
 
Kama mtu Hana mtaji wa kufanya biashara, let's say na mshahara unakuta umebana kwenye matumizi yake na familia, mnamshauri Nini akitaka kujikwamua, wabongo bana, ukichukua mkopo kununua gari ya kutembelea(liability) watu Wanaona poa tu ila huyu anayetaka kuanza biashara mnamkatisha tamaa, mleta mada usiogope, hata mo juzi kasema anadaiwa zaidi ya bilioni 500 licha ya kua ndo tajiri namba 1 nchini
Ukiwa na wazo au jambo lako lenye manufaa usiwashirikishe wabongo......jambo la kwanza kwa mbongo ni kukukatisha tamaa......atakupa kila ugumu WA jambo mpaka ughairi..........

Wabongo watu wa ajabu sana......

Hapo angesema anakopa aoe watu wangemuunga mkono........
 
Wadau Mimi ni mtumishi wa afya, mshahara wangu unaniruhusu kukopa mil 15.

Nataka nikope mil 15 niwe nakatwa kwenye mshahara Kwa miaka sita, Nichukie mil 10 niingie kwenye mpunga na mahindi. Silimi nafuata Kwa wakulima naweka store.

Nasubiri yapande niuze wakati mkopo unakatwa kwenye mshahara.

NAJIONA NIKO SAHIHI,PLEASE KAMA KUNA MKOSOAJI ANISAIDIE
Ungeanza walau na 2M ili utafute njia na changamoto zake ili hata ukipata hassara isikuumize sana na ukipata faida ni vizuri zaidi kwa ajili ya kipindi kijacho ila kama uliwahi kupitapita huko na changamoto zake unazifahamu unaweza kuendelea
 
Ndugu mtoa mada.....

Wazo lako ni zuri na Mungu akufanyie wepesi kwenye jambo lako la kheri.......

Ushauri ni kuwa kabla ya kuchukua hatua tafuta mtu anayefanya biashara hii mwenye uzoefu.....akupe mwangaza..........

Maisha ni kujaribu, kupata na kupatia, kusimama au kuanguka......kuteleza au kuporomoka........

Kama una wasaa wa kukopa ili kufanya jambo lako fanya hivyo...... inawezekana miaka kadhaa ukaijutia kupoteza nafasi hii au wanao au familia yako wakakuona shujaa kwa maamuzi haya........

Nakutakia kila la kheri......na Mungu akutangulie kwenye kheri....
 
Unakopaje milioni 15 kwa miaka 6? hizi ni akili au matope?
Hapo unarudisha sio chini ya milioni 28 sasa hiyo biashara itakuingizia zaidi ya milioni 28 na faida juu ndani ya hiyo miaka?
Hata hivyo kama huna mtaji sio lazima ufanye biashara.

Jikusanye mwenyewe upate hela uanze biashara utakayoimudu kwa hela uliyonayo ukishaifahamu na kuweza kuona mwelekeo ndo ukakope uongeze mtaji.
 
Back
Top Bottom