Wadau Mimi ni mtumishi wa afya, mshahara wangu unaniruhusu kukopa mil 15.
Nataka nikope mil 15 niwe nakatwa kwenye mshahara Kwa miaka sita, Nichukie mil 10 niingie kwenye mpunga na mahindi. Silimi nafuata Kwa wakulima naweka store.
Nasubiri yapande niuze wakati mkopo unakatwa kwenye mshahara.
NAJIONA NIKO SAH

NAJIONA NIKO SAHIHI,PLEASE KAMA KUNA MKOSOAJ
Hongera kwa maamuzi hayo ndugu. Naomba kwa uelewa wangu wa kawaida nishauri yafuatayo:
1. Fanya utafiti wa kina juu ya hiyo biashara kuhusu;
• Wapi mzigo unapatikana.
• Miezi gani mzigo unapatikana kwa wingi?
• Bei zake zikoje
• Gharama halisi za kuendeshea biashara zikoje mf. (Usafiri, wapakiaji, washushaji, ununuzi wa magunia ambayo hayaruhusu wadudu)
• Utahifadhi wapi na kwa gharama kiasi gani kwa kila gunia?
• Usalama wa mzigo ukoje?(dhidi ya wizi, majanga kama mafuriko, moto, wadudu nk) • Soko lako litakuwa ni lipi?
• Sera za nchi kwasasa zikoje uhusu biashara hiyo, je, zinatabirika?
• Ushuru na tozo mbalimbali za serikali zikoje?
• Profit Margin yake ikoje(Faida kutoa(minus) Gharama zote za kuendeshea biashara)
• Fuatilia sana taarifa za bei za soko la hiyo bidhaa kila siku kila mahali-Wilaya na Mikoa yote(Bei hupanda na kushuka kulingana na Demand vs Supply) ili zikusaidie kufanya maamuzi sahihi ni lini uuze au usiuze.
Pia, tembelea site ambako utatarajia kununua mzigo, fanya mahusiano na watu ambao wameshafanya hiyo biashara wakupe uzoefu(Hapa kuwa makini, wengi hupenda kusifia mafanikio, wewe jitahidi utafute taarifa kuhusu changamoto za biashara hiyo.
Kwa ufupi, tafuta upate knowledge yote kuanzia unaanzia unaponunua mzigo hadi utakapouuza.
2. Kama utachukua M.15, usiwekeze yote kwenye hiyo biashara, kama huna uzoefu nayo. Biashara huwa inakuwa na intervening factors nyingi ambazo kama huna uzoefu zinaweza kukutoa mchezoni ndani ya siku moja. Kwaajili hiyo, chukua angalau 35% tu ya mkopo wako ndio uiingize kwenye biashara, nyingine 65% uitunze mahali ambapo patakufanya usiifikie na kuitumia(Usiwe na haraka)
Baada ya kuusoma mchezo wa kwanza, na kama faida imepatikana, chukua kiasi kingine angalau 10% ya mkopo uongezee ili uongeze mzigo, fanya hivyo taratibu mpaka utakapokuwa umeridhika kwamba umeshapata uzoefu wa kutosha kwenye biashara hiyo. NOTE: Msimu wa kwanza utumie kama msimu wa kujifunzia(Hata hivyo, jitahidi kucontrol factors zote zinazoweza kuhatarisha biashara). Upo uwezekano wa kuingia msimu mmoja na ukapata faida msimu huo huo.
3. Baada ya hapo fanya diversification ya mtaji wako kwa kuwekeza maeneo mengine, epuka kuweka mayai yote kwenye chungu kimoja. Sera za nchi hasa kwenye upande wa mazao ya nafaka bado haziko stable, hivyo usiingize miguu yote, Kenya au Zambia wakifunga tu mipaka, bei ya nafaka huporomoka sana!
NB: Kama kuhifadhi fedha itakuwa changamoto, chukua mkopo mdogo ambao unaweza kuulipa ndani ya mwaka au miezi 6. Ukishapata uzoefu nenda tena kachukue yena( Benki hazizuii kukopa kidogo kidogo)
Asante!
Wadau Mimi ni mtumishi wa afya, mshahara wangu unaniruhusu kukopa mil 15.
Nataka nikope mil 15 niwe nakatwa kwenye mshahara Kwa miaka sita, Nichukie mil 10 niingie kwenye mpunga na mahindi. Silimi nafuata Kwa wakulima naweka store.
Nasubiri yapande niuze wakati mkopo unakatwa kwenye mshahara.
NAJIONA NIKO SAHIHI,PLEASE KAMA KUNA MKOSOAJI ANISAIDIE