Nachukua mkopo CRDB nianze biashara ya nafaka(mpunga na mahindi)

Tumia kwanza ulichonacho anzia level ya chini ujue changamoto.. ukishaizoea biashara ndipo utaamua ukope au uache.

Mimi ni Nafaka dealler.. Kuna ugumu sana katika kukusanya Mahindi na Ngano.. Taratibu za vijiji Sehemu nyingine hutoki na Mazao mkuu.
 
Fanya upendavyo...watu wanachukua Mkopo wanajenga Nyumba kumbe kiwanja kina mgogoro inabomolewa na marejesho unalipa kama kawaida
 
Mkuu kama anajua kuifanya hii biashara kwa usahihi.. Hiyo pesa atailipa na atapiga pesa nyingi sana zaidi ya hapo.

Ila asikope kabla hajaanza kuifanya.. Akubali kwanza kujifunza. Kupoeza miezi2,3-4 kujifunza; sio Ishu kwa Mjasiriamali.
 
Jipange kurejesha milioni 31 Hizo Bank sina hamu nazo ni wanyonyaji hasa.
 
Hii biashara ni kama kamari flani yenye low risk, ukiwa mvumilivu unaweza kupata faida ila mambo sio rahisi kama unavyodhani, wakati gunia la mahindi sasa hivi likiuzwa 40k Kuna ambao wanayo ya mwaka jana walionunua 70k wakisubiri Bei ipande
Sasa hivi hakuna mpungu gunia 40k, ni 60 na kwendelea, tena huo ni wakawaida tu, katani inaenda 70k hadi 90k.
 
Haitakuja itokee mimi nikope pesa bank, tena mamikopo ya riba mmhhh!!! Hapana
 
Njoo tuwekeze kwenye mbao utanishukuru.
 
Haitoshi hiyo pesa ni ndogo sana kama umeamua kufanya hii biashara. Itakatika na hauna utakachokuwa umefanya. Hii biashara ukitaka kuifanya serious miaka hii andaa around 35 million.

Kama hautaki haya nenda kajionee.
 
1.Kama unaweza anza na mill 10 kwanza.
Pia,uwe mzoefu,au tafuta mzoefu na mwaminifu akuongoze,hasa mwenyeji wa eneo husika.
(Usisahau kufanya utafiti)
2.Nenda site,kununua nafaka,ukiwa na mwenyeji,tafuta uwezekano wa kupunguza gharama kadili iwezekanavyo.
3.Ujue muda sahihi wa kuuza nafaka,hii itakusaidia kukwepa hasara,au faida kiduchu.
4.Usiwe na tamaa sana ya kupata super profit.Uza kwa wakati sahihi.
Mf;
Umenunua mpunga gunia@60,000/=
(+other costs)June
Mwezi November,bei ya gunia imefika 90,000/=
Hapo uza usisubiri bei ipande zaidi.
Ukisubiri,umechagua kubet kupata faida sana au faida kiduchu.
 
Uzi ufungwe hapa.
Wewe mwanamke inaonekana una akili sana.
I wish kama ungekuwa Mchumba wangu ili nikutolee posa kisha nikuoe.

I am ready to be corrected; ni wanawake wachache sana ambao naamini wapo vizuri sana upstairs like you.

Abarikiwe sana mwanaume uliyemkabidhi moyo wako maana hiyo ni bahati Katika maisha.
 

👆👆 Hayo ni maumivu mkuu,japo utaona makato madogo lakini hapo utakuwa umewanufaisha bank kwa kiwango kikubwa sana
Achana na hiyo kitu.

Kama unaweza kopa kwa muda mchache let say ni kama miezi 18 hivi hapo ndio wewe unakuwa na faida na sio kufaidisha Bank
 
Labda udanganye kwamba unaenda kujengea vinginevyo hakuna mtu atakupa Mkopo kuanzisha biashara Mpya unless unaendeleza
 
SIyo lazima uwe unaijua! Kama ashapata elimu kuhusu hiyo biashara? Watu wanaofanya hizi kazi wamejaa mtaani na huenda watu wameshampa mbinu zote.
 
Sikiliza moyo wako, mawazo ya watu yatakuyumbisha.
 
Kabla ya kuchukua huo mkopo hakikisha biashara unaijua nje ndani, jifunze kwa kupitia sehemu Kama hizi kabla na sehemu zinginezo pia ulijue soko lako, jifunze na ujue hasara huwa Inapatikana vipi na faida inaapatikana vipi....kabla ya kumiliki biashara Anza kwanza kuiishi hio biashara kichwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…