Nachumbiwa na mtu wa Musoma

Huyo ni mtani na jirani yako, haina shida ila mama mkwe wako anaweza kukwambia ukeketwe sasa wakati we umezoea kurusha maji.
Hahaha! Hiyo inipite mbali aisee
 
Karibu mama karibu sirari border ya wajanja, mji umechangamka huu, kila biashara inaenda, huku kwetu hamna njaa njaa tunalima mahindi, muhogo, viazi, maharage utakula utashiba.
Sirari inapakana na Kenya shopping zetu tunaenda kufanya huko vitu bei chee, lakini pia kuna amani ya kutosha.
 
Mikate laini toka Kenya, aisee umenikumbusha mbali.
 
SIRARI wako wakrya wengi sana wale wa kenya...tarime mjini wako tofauti wengi wajanja wanjaa, rorya ndo wako og sasa...musoma ukivuka ngambo kule kinesi utawakuta wakrya wavuvi[hawa wanangoma sana] then watata ni wale wa nyamongoo
 
Hapa ndio ile methali ya "Ukitaka kuruka agana na nyonga" ina apply
 
Wanawake wengi sana Tanzania wanaogopa na hawapendi kuolewa na Wakurya.
 
Wanajua kupenda, wana wivu hasira za kufikia ila kikubwa kuliko vyotee sahau mambo ya kubebishana sijui honey, darling nk sahau zaidi umeitwa mamy basi hahah mie wang nmemzoea mnooo pamoja na ubabe wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…