NACTE imevishusha hadhi Vyuo 16 nchini na Vitatu vimefutiwa usajili

NACTE imevishusha hadhi Vyuo 16 nchini na Vitatu vimefutiwa usajili

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Vyuo 16 vimeshushwa hadhi na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kutokana na sababu mbalimbali na pia Vyuo vitatu vimefutiwa usajili.

Taarifa kamili itawajia muda mfupi ujao.

=======================

Vyuo vilivyofutiwa usajili ambavyo pia vilikuwa vimepatiwa usajili wa awali Institute for Information Technology chenye namba za usajili REG/EOS/014, Dar es Salaam College of Clinical Medicine na Ndatele School of Medical Laboratory Science.

Vyuo hivyo vimefungiwa kwa kutumia sheria ya Bunge sura Na. 129 na kanuni za Usajili (2001) na zile za Ithibati na utambuzi (2001), ambapo Februari 20, mwaka huu, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga, amesema Vyuo ambavyo vimefungiwa havitaruhusiwa kuendelea na udahili wa wanafunzi na wanafunzi ambao waliokuwa wameshaanza masomo watahamishiwa katika vyuo vingine kwa ada zao zile zile ambapo itabidi mmiliki azilipe.
 
Vilivyovutwa

dar es salaam college of clinical medicine
ndatele school of medical laboratory
institue of information technology
.
 
Wametoa taarifa kuwa vyuo vitatu vimefutwa na vingine 16 vimeshushwa daraja.Cha ajabu hawavitaji vyuo vyenyewe.kama habari hawakuipata yote si afadhali waiche hiyo habari kuliko kusema tu vya jijini Dar.mwenye habari atujuze jamani!
 
Habari wana bodi. Naangalia taarifa ya habari chanel ten kuna habari hapa kuwa kuna Vyuo vitatu vimefutiwa usahili na nacte na vyuo 16 vimeshushwa hadhi.Kwa bahati mbaya taarifa hii ya habari haijataja vyuo hivyo. Mwenye kujua majina ya vyuo hivyo atusaidie kuvitambua. Ukizingatia huu ndio muda wa maombi ya vyuo hivyo vijana wasije wakatapeliwa.


Nawasilisha.
 
Yeah.. Hii taarifa nimeiskia clouds na vyuo vingi ni vya udaktari na science ya computer
Vilivyofungiwa
 
Channel 10...not very professional aisee hawajavitaja...wanawaza tu jinsi ya kuyoa habari za watia nia..itabidi tusubiri tu ITV...
 
Vipi hiki cha gongo la mboto (KIU) hakipo kwenye list?? maana waziri mkuu leo alikuwa anakilalamikia mara baada ya kukutana na wawakilishi wa wazazi dodoma leo.
 
Katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt. Adolf B. Rutayuga alisema kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya vyuo husika kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na NACTE. "Kwa kutumia Sheria ya Bunge Sura Na. 129 na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujitetea na kufanya marekebisho yaliyobainishwa," alieleza. Kaimu Katibu Mtendaji huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya Taasisi na Vyuo vya Ufundi NACTE aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi vilivyopewa maelekezo ya kufanya marekebisho vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yabainishwa.

Hata hivyo alisema hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake. "Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa kwa makosa yafuatayo, moja kumalizika kwa muda wa Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); pili kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; tatu kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukuliwa hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na nne taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbali mbali," alifafanua

Vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na Dar es Salaam College of Clinical Medicine cha jijini Dar es Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali na Institute for Information Technology cha jijini Dar es Salaam pia chenye namba za usajili REG/EOS/014.

Taassi/vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kushindwa kutiza mashart ni pamoja na Sura Technologies – Dar es Salaam, Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam, Techno Brain – Dar es Salaam, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya, Mbozi School of Nursing – Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi. Vingine ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC – Songea, CATC – Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga, COTC – Musoma, Dental Therapists Training Centre – Tanga, Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.
 
Wametoa taarifa kuwa vyuo vitatu vimefutwa na vingine 16 vimeshushwa daraja.Cha ajabu hawavitaji vyuo vyenyewe.kama habari hawakuipata yote si afadhali waiche hiyo habari kuliko kusema tu vya jijini Dar.mwenye habari atujuze jamani!

mi hiki kituo hata huwa sikielewi, ni cha muda mrefu lakini huwa ubunifu ni zero!! wakati mwingine unakuwa unaangalia hizo picha utandhani unaangalia kupitia YouTube!! low quality, kwa majanga wanaanza tbc, kisha wao taarifa za habari zenyewe mmmm!!! hata clouds tv, nao wajipange sana kwenye upande wa tv ni kama nao walikurupuka tu,.
 
mi hiki kituo hata huwa sikielewi, ni cha muda mrefu lakini huwa ubunifu ni zero!! wakati mwingine unakuwa unaangalia hizo picha utandhani unaangalia kupitia YouTube!! low quality, kwa majanga wanaanza tbc, kisha wao taarifa za habari zenyewe mmmm!!! hata clouds tv, nao wajipange sana kwenye upande wa tv ni kama nao walikurupuka tu,.
Hataki kuajili qualified akikwepa kulipa mshahara mkubwa.kinawasinda kituo
 
Back
Top Bottom