NACTE imevishusha hadhi Vyuo 16 nchini na Vitatu vimefutiwa usajili

NACTE imevishusha hadhi Vyuo 16 nchini na Vitatu vimefutiwa usajili

mi hiki kituo hata huwa sikielewi, ni cha muda mrefu lakini huwa ubunifu ni zero!! wakati mwingine unakuwa unaangalia hizo picha utandhani unaangalia kupitia YouTube!! low quality, kwa majanga wanaanza tbc, kisha wao taarifa za habari zenyewe mmmm!!! hata clouds tv, nao wajipange sana kwenye upande wa tv ni kama nao walikurupuka tu,.

Clouds tv ndio bogus kabisa kipindi kinachoeleweka pale ni mahusiano basii...vingine vyote quality hovyooo...
 
Wametoa taarifa kuwa vyuo vitatu vimefutwa na vingine 16 vimeshushwa daraja.Cha ajabu hawavitaji vyuo vyenyewe.kama habari hawakuipata yote si afadhali waiche hiyo habari kuliko kusema tu vya jijini Dar.mwenye habari atujuze jamani!

Ingia kwenye tovuti ya NACTE utaona vyuo ambavyo vipo Accredited and Not Accredited.
 
Ni kweli kuna vyuo vyenye usajili wa NACTE vimefutwa nimemuona msemaji toka NACTE kwenye kipindi cha Hot Mix cha EATV akiongea kuhusu swala hilo, bahati mbaya nimekuta ndio mahojiano yanamalizika ila kwa alietazama mahojiano yote atujuze.
 
Nitafurahi nikikiona chuo cha wahindi St.joseph,wle jamaa hawana uoga kwenye nchi za watu.wanajisikia huru utadhani wapo kwao.
 
Kichwa cha habari na contents ni vitu viwili tofauti.
 
Nitafurahi nikikiona chuo cha wahindi St.joseph,wle jamaa hawana uoga kwenye nchi za watu.wanajisikia huru utadhani wapo kwao.


Taarifa ya kuhuzunisha kwako nimeona St. Joseph Arusha-Campus iko Accredited japo haijaonesha kwa muda gani,, Na St. Joseph Morogoro ni Full registered mkuu
 
Mimi nataka kujuwa hivi vilivyoshushwa hadhi ni vipi? lakini pia nataka kujuwa vimeshushwa hadhi kivipi kwamba tusiende kusoma?, walimu itakuwa hamna?, wanafunzi wasiombe? ama vipi?
 
Chuo changu nachosoma nacho ni kimoja wapo kimeshushwa hadhi sasa weny uelewa wa haya mambo ebu watujuze
 
Safi NACTE kuna vyuo vingi tu vinavyokula pesa za wananchi huku taaluma wanayoitoa ni hafifu, navyo vifutiwe usajiri ili kuinua taaluma Tanzania.
 
Wapendwa chuo changu nilichosoma kimefutiwa usajili, mimi nimehitimu mwaka jana naweza kuendelea na maombi ya Elimu ya juu au kwa waliomaliza haiwahusu?
 
KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi
KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi
KCMC AMO General School – Moshi
Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi
kwa taarifa hii inabidi KCMC ichunguzwe kwa kina. Haiwezekani taasisi zake tatu ziwe katika orodha hii. Je, tutaaminije wanafunzi wanaozalishwa hapo?
 
Habari wana bodi. Naangalia taarifa ya habari chanel ten kuna habari hapa kuwa kuna Vyuo vitatu vimefutiwa usahili na nacte na vyuo 16 vimeshushwa hadhi.Kwa bahati mbaya taarifa hii ya habari haijataja vyuo hivyo. Mwenye kujua majina ya vyuo hivyo atusaidie kuvitambua. Ukizingatia huu ndio muda wa maombi ya vyuo hivyo vijana wasije wakatapeliwa.


Nawasilisha.

Soma gazeti la HABARILEO toleo la tarehe 25/06/2015 Alhamisi utapata habari kamili.
 
Back
Top Bottom