NACTVET: Baraza limeongeza kasi ya kushughulikia maombi yote ya AVN Number kwa dharura

NACTVET: Baraza limeongeza kasi ya kushughulikia maombi yote ya AVN Number kwa dharura

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mara baada ya Mwananchi kuwasilisha malalamiko kwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kuhusu changamoto ya kukosekana kwa Namba ya Utambuzi wa Tuzo (AVN) kwa Watu waliohitimu ngazi ya Diploma na hivyo kukwama kufanya maombi ya kujiunga na vyuo mbalimbali, ufafanuzi umetolewa.

Kusoma alichoandika Mdau bofya hapa ~ NACTVET watusaidie tupate AVN number kwa uharaka tunashindwa kuomba Chuo

UFAFANUZI KUHUSU CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA NAMBA YA UTAMBUZI WA TUZO (AVN)
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kijamii ‘JamiiForums.com” kuhusu waombaji wa Namba ya Utambuzi wa Tuzo (AVN) kushindwa kupata namba ya malipo (control number) na kukosa msaada juu ya suala hilo.

Mfumo wa utoaji wa AVN unafanya kazi kikamilifu na hakuna changamoto ya ucheleweshaji wa namba ya malipo (control number). Hata hivyo, baadhi ya waombaji hushindwa kupata AVN kwa wakati kutokana na kutokamilisha taarifa zao katika mfumo, ikiwemo kutojaza taarifa kwa usahihi na kukosekana kwa matokeo ya mitihani.

Ili mwombaji aweze kupata AVN, anatakiwa kuhakikisha anakamilisha mambo yafuatayo:

I. Kujaza taarifa kwa usahihi katika mfumo wa AVN, ikiwemo namba ya simu, barua pepe na namba ya usajili iliyotumika kuwasilisha matokeo yake NACTVET.

II.
Kwa waombaji waliohitimu Diploma kuanzia Mwaka 2015, matokeo yao yawe yamewasilishwa na vyuo husika kwenye Mfumo wa NACTVET.

III. Kwa waombaji waliohitimu Diploma kabla ya Mwaka 2015, waambatishe vyeti vya kitaaluma na hati za matokeo kwenye mfumo wa AVN kwa usahihi.

Baraza linawakumbusha waombaji wote wa AVN kuhakikisha wanahakiki matokeo yao kupitia mfumo wa "Student`s Information Verification" unaopatikana kwenye tovuti ya NACTVET www.nactvet.go.tz kabla ya kuwasilisha maombi ya AVN.

Aidha, kutokana na wingi wa maombi ya AVN katika kipindi hiki cha udahili, Baraza limeongeza kasi ya kushughulikia maombi yote kwa dharura. Baraza pia linawahimiza wanafunzi wote kuhakiki taarifa zao ili kuepuka changamoto za baadaye.

Mnamo tarehe 6 Mei, 2025, NACTVET ilizindua kampeni ya Mwanachuo Smart kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi wa Astashahada na Stashahada kuhakiki taarifa zao mara kwa mara kwenye mifumo ya NACTVET ili kujihakikishia kuwa taarifa zao zipo kwenye mifumo ya NACTVET. Hatua hii ni muhimu ili kuepuka changamoto wakati wa kuomba AVN na hati za matokeo(transcript).

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko – NACTVET
31 Julai, 2025
UFAFANUZI AVN_page-0001.jpg
​
 
AVN namba Inapatikana kwa urahisi kabisa na kwa haraka , sema tatizo ni ugumu wa vichwa vyao..
 
Back
Top Bottom