A
Anonymous
Guest
Mimi ni mdau wa elimu kutoka Jiji la Arusha.
Kwa sasa dirisha la maombi ya kujiunga na vyuo vya kati kwa kozi za afya lipo wazi. Hata hivyo, jambo linalozua maswali mengi ni hatua ya NACTVET kuongeza vigezo vya udahili kwa baadhi ya kozi muhimu za afya, hususan Pharmacy na Nursing.
Kwa mfano, hapo awali mwanafunzi aliyekuwa na ufaulu wa angalau D katika Biology na Chemistry, pamoja na kuwa na sifa ya ziada katika Basic Mathematics, aliweza kuomba kozi ya Pharmacy. Vivyo hivyo, kwa kozi ya Nursing, mwanafunzi alihitaji kuwa na angalau D tatu katika masomo ya Physics, Chemistry na Biology (PCB).
Kwa sasa, vigezo hivyo vimepandishwa kwa kiwango kikubwa zaidi. Baadhi ya taarifa zinaonesha kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na angalau C katika Biology na Chemistry pamoja na D katika Physics. Kwa mtazamo wa wengi, vigezo hivi vinafanana zaidi na mahitaji ya kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita kuliko vyuo vya kati vinavyolenga kutoa fursa kwa wahitimu wa kidato cha nne.
Kutokana na mabadiliko haya, maswali kadhaa yanaibuka:
Tunaomba NACTVET itoe maelezo rasmi kuhusu suala hili ili kuondoa maswali na wasiwasi uliopo miongoni mwa wadau wa elimu.

- Je, NACTVET imelenga kupunguza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na taaluma za Pharmacy na Nursing nchini?
- Je, kuna utafiti au tathmini maalumu iliyobaini umuhimu wa kuongeza vigezo hivi vya udahili?
- Kwa nini wadau wa elimu, wanafunzi na wazazi hawakupewa taarifa na maelezo ya kutosha mapema kabla ya mabadiliko haya kuanza kutumika?
- Je, NACTVET ilifanya mashauriano na wadau wa sekta ya afya, vyuo vya mafunzo ya afya na taasisi nyingine husika kabla ya kuidhinisha miongozo hii mipya?
- Dhumuni kuu la kuongeza vigezo hivi ni nini, na je, limeelezwa wazi kwa umma ili kuondoa sintofahamu iliyopo sasa?