Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limetoa taarifa kuwa limefanya maboresho ya mawasiliano yake kwa njia ya simu ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wadau wake.
NACTVET imeeleza kuwa mbali na namba za simu za Makao Makuu, maboresho hayo yamejumuisha upatikanaji wa namba za simu za Ofisi za Kanda za NACTVET zilizopo nchini kote.