Nadhani Boniface Mwabukusi amekosea fani ya sheria . Nadhani alitakiwa kugombea udiwani au ubunge

Bado upo nyuma sana ya wakati. Chadema mlipinga ujenzi wa bwawa la mwalimu Nyerere kwa sababu ya kampeni zenu eti tunaharibu mazingira. Ajabu treni imeanza kufanya kazi nyie ndio wakwanza mnapiga selfie kwenye treni. Shenzi sana.
Haujajibu swali, jamaa kakuuliza vizuri ingawa kwa sarcasm. Wamasai wameondolewa ili kuhifadhi mazingira na bioanuwai, sasa vipi mpango wa kutaka kuchimba madini kwenye hifadhi ambao mkuu alisema wanyama hawali madini?
 
Mmezaliwa jana nyote nyinyi , nyerere aliwaondowa wananchi sehemu walipozaliwa na walikuwa na mashamba yao waliondolewa kwa nguvu na kupelekwa kwenye vijiji vya ujamaa wakaanzishe maisha ya vijiji vya ujamaa waliondolewa kwa nguvu wengine walipoteza maisha kwa mawazo na wengine waliumia lakini kwa hilo mpo kimya bado mnamuita mtakatifu
 
Nje ya mada..,

Iyo TLS ina faida/mchango gani kwa Taifa hadi kupelekea watu kufikishana mahakamani na kumake headline ukitoa maslahi ya Posho wanazolipana kwenye iko kikundi?
Can someone please respond
TLS ni nzuri kwa ustawi wa mawakili na sheria nchini lakini imevamiwa na wanasiasa wakina Mwabukusi unategemea Nini?
 
Mmezaliwa jana nyote nyinyi , nyerere aliwaondowa wananchi sehemu walipozaliwa na walikuwa na mashamba yao waliondolewa kwa nguvu na kupelekwa kwenye vijiji vya ujamaa wakaanzishe maisha ya vijiji vya ujamaa waliondolewa kwa nguvu wengine walipoteza maisha kwa mawazo na wengine waliumia lakini kwa hilo mpo kimya bado mnamuita mtakatifu
Huwezi kuona faida ya matunda ya uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa .
 
..Na Mama Abduli kasema atachimba madini Serengeti hata kama Tanapa wanapinga.

..anatetea maamuzi yake kwa madai kwamba tambo na Simba hawali madini.

..Mama Abduli hajali mazingira, wala thamani ya Serengeti, kubakia ktk uasilia wake.

..Sasa nani mwenye akili kati ya Mama Abduli na Adv Mwabukusi?
Bwawa la mwalimu Nyerere mlikua mnapinga hivi hivi kwa sababu za kimazingira lakini Leo mnapiga selfie kwenye treni za umeme.
 
Nadhani Boniface Mwabukusi amekosea fani ya sheria . Nadhani alitakiwa kugombea udiwani au ubunge.

Tukubaliane kimsingi uendeshaji wa nchi mbali na kufuata sheria na katiba lakini maslahi ya nchi yapo mbele zaidi ya sheria hii ni common sense tu unaweza usiikute kwenye sheria au katiba.

Mwabukusi anasema ni kosa kuwaondoa wamasai ngorongoro. Kisheria anaweza kuwa sawa lakini je amepima athari za kimazingira katika maeneo ya hifadhi ambapo nchi hii tunapata zaidi ya 20% ya mapato ya serikali kuu?

Wafugaji wanaondolewa ngorongoro lakini wanapelekwa katika maeneo mengine yenye ardhi na makazi ya kisasa tofauti na ngorongoro walikua wanalala kwenye nyumba za manyata. Hivi katika Hali ya kawaida hii ni improvement au backwards?

Huyu Mwabukusi kwa hoja hizi chache tu nimemuonq ni mwepesi sana.nyie mawakili mtakaosoma hapa nawashauri Mwabukusi hafai kama anapenda kuwa kiongozi sana mwambieni mwakani agombee ubunge.

PIA SOMA
- LIVE - Mdahalo wa Wagombea Uraisi TLS na Chief Odemba
Na vipi ile kauli ya samia kuwa madini yachimbwe hata kwenye hifadhi kwasababu kinachotakiwa ni fedha tu nayo unaipimaje?
 
Nadhani Boniface Mwabukusi amekosea fani ya sheria . Nadhani alitakiwa kugombea udiwani au ubunge.

Tukubaliane kimsingi uendeshaji wa nchi mbali na kufuata sheria na katiba lakini maslahi ya nchi yapo mbele zaidi ya sheria hii ni common sense tu unaweza usiikute kwenye sheria au katiba.

Mwabukusi anasema ni kosa kuwaondoa wamasai ngorongoro. Kisheria anaweza kuwa sawa lakini je amepima athari za kimazingira katika maeneo ya hifadhi ambapo nchi hii tunapata zaidi ya 20% ya mapato ya serikali kuu?

Wafugaji wanaondolewa ngorongoro lakini wanapelekwa katika maeneo mengine yenye ardhi na makazi ya kisasa tofauti na ngorongoro walikua wanalala kwenye nyumba za manyata. Hivi katika Hali ya kawaida hii ni improvement au backwards?

Huyu Mwabukusi kwa hoja hizi chache tu nimemuonq ni mwepesi sana.nyie mawakili mtakaosoma hapa nawashauri Mwabukusi hafai kama anapenda kuwa kiongozi sana mwambieni mwakani agombee ubunge.

PIA SOMA
- LIVE - Mdahalo wa Wagombea Uraisi TLS na Chief Odemba
Haya mambo hayana tija Tundu Antipas Lisu alikuwa Rais wa TLS sikumbuki alifanya nini,sasa huyu Mwabukusi apewe tu maana hakuna atakachofanya zaidi ya kutafuna subscriptions .
 
Kwa mujibu wa Tafiti zilizofanyika sehemu mbalimbali Duniani, inaonesha kuwa ' indigenous people' yaani Wakazi wazawa au watu wa asili wa eneo husika(sijui kama nimetafsiri sahihi) wamekuwa wakionewa sana na mamlaka mbalimbali za Kiserikali Duniani kote. Na hii ni kutokana na wao kuwa katika category ya 'underrepresented group'. Hii imepelekea kuwepo na maazimio mbalimbali na sheria mbalimbali za kimataifa za kulinda haki zao.

Katika nchi zilizoendelea, masuala haya yanachukuliwa kwa uzito wa juu. Unfortunately, hawa watu wanapatikana zaidi katika nchi ambazo hazijaendelea (developing world) ambako misingi ya demokrasia bado si imara. Hii haimanishi hawapo katika nchi zilizoendelea. Hata huko wapo pia. Mfano Sami people in Scandnavian countries.

Hivyo basi, mtu yeyote ambaye ni mwanademokrasia wa kweli, mwenye kujali haki za binadamu kwa ukweli wake, lazima awe very conscious when it comes to this group of Indigenous and underrepresented people. Ndio maana hawa watu wanapoguswa kidogo tu hutafsiriwa kuwa wanaonewa hata kama kukiwa na mpango mzuri wenye maslahi makubwa zaidi kwa Taifa.

Changamoto ninayoona ni kuwa, kuna dalili kuwa huenda Serikali haikufuata baadhi ya misingi ya uwazi na ushirikishwaji wa kina juu ya lengo la kuwahamisha watu hao huko Ngorongoro. Na hii ni kawaida kwa nchi za dunia ya tatu. Sasa hapo ndo kelele zinapokuja. Kama Serikali ingeweka mambo haya wazi kabisa, namna gani wanakuwa compensanted, namna gani wanakuwa involved kwenye maamuzi na ushirikishwaji wa kina wa wadau wengine kama Non-governmental organisations, hakika makelele yangepungua.

Kwahiyo Mwambukusi anaweza kuwa sahihi katika context niliyoelezea hapo juu.
 
Haya mambo hayana tija Tundu Antipas Lisu alikuwa Rais wa TLS sikumbuki alifanya nini,sasa huyu Mwabukusi apewe tu maana hakuna atakachofanya zaidi ya kutafuna subscriptions .
Umesema kweli
 
Bwawa la mwalimu Nyerere mlikua mnapinga hivi hivi kwa sababu za kimazingira lakini Leo mnapiga selfie kwenye treni za umeme.

..kwani umeme wa maji hauwezi kuzalishwa eneo lingine lolote hapa Tanzania isipokuwa Stieglers gorge?
 
Nadhani Boniface Mwabukusi amekosea fani ya sheria . Nadhani alitakiwa kugombea udiwani au ubunge.

Tukubaliane kimsingi uendeshaji wa nchi mbali na kufuata sheria na katiba lakini maslahi ya nchi yapo mbele zaidi ya sheria hii ni common sense tu unaweza usiikute kwenye sheria au katiba.

Mwabukusi anasema ni kosa kuwaondoa wamasai ngorongoro. Kisheria anaweza kuwa sawa lakini je amepima athari za kimazingira katika maeneo ya hifadhi ambapo nchi hii tunapata zaidi ya 20% ya mapato ya serikali kuu?

Wafugaji wanaondolewa ngorongoro lakini wanapelekwa katika maeneo mengine yenye ardhi na makazi ya kisasa tofauti na ngorongoro walikua wanalala kwenye nyumba za manyata. Hivi katika Hali ya kawaida hii ni improvement au backwards?

Huyu Mwabukusi kwa hoja hizi chache tu nimemuonq ni mwepesi sana.nyie mawakili mtakaosoma hapa nawashauri Mwabukusi hafai kama anapenda kuwa kiongozi sana mwambieni mwakani agombee ubunge.

PIA SOMA
- LIVE - Mdahalo wa Wagombea Uraisi TLS na Chief Odemba
Hoja zako zipo chini. Wamasai ni sehemu ya ecologia. Na wamekaa kwa muda mrefu sana pembezoni mwa wanyama. Sio jambo geni.

Jambo la pili usiwapangie watu kitu cha kufanya.

Kila mtu Mungu amemuuba kwa sababu zake.

Next time try to sharpen your mind and improve your argument before writing
 
..kwani umeme wa maji hauwezi kuzalishwa eneo lingine lolote hapa Tanzania isipokuwa Stieglers gorge?
Umeme chanzo chake siyo lazima kiwe maji tu peke yake, hata jua pia ni chanzo Cha uhakika kabisa Cha uzalishaji wa umeme.
Tatizo ni kwamba kwenye hizi nchi zetu za Afrika watu wenye maono huwa wanakuwa hawana mamlaka/madaraka, na Watu wenye madaraka huwa wanakuwa hawana maono yoyote yale akilini mwao.
 
Nadhani Boniface Mwabukusi amekosea fani ya sheria . Nadhani alitakiwa kugombea udiwani au ubunge.

Tukubaliane kimsingi uendeshaji wa nchi mbali na kufuata sheria na katiba lakini maslahi ya nchi yapo mbele zaidi ya sheria hii ni common sense tu unaweza usiikute kwenye sheria au katiba.

Mwabukusi anasema ni kosa kuwaondoa wamasai ngorongoro. Kisheria anaweza kuwa sawa lakini je amepima athari za kimazingira katika maeneo ya hifadhi ambapo nchi hii tunapata zaidi ya 20% ya mapato ya serikali kuu?

Wafugaji wanaondolewa ngorongoro lakini wanapelekwa katika maeneo mengine yenye ardhi na makazi ya kisasa tofauti na ngorongoro walikua wanalala kwenye nyumba za manyata. Hivi katika Hali ya kawaida hii ni improvement au backwards?

Huyu Mwabukusi kwa hoja hizi chache tu nimemuonq ni mwepesi sana.nyie mawakili mtakaosoma hapa nawashauri Mwabukusi hafai kama anapenda kuwa kiongozi sana mwambieni mwakani agombee ubunge.

PIA SOMA
- LIVE - Mdahalo wa Wagombea Uraisi TLS na Chief Odemba
Mwabukusi ni mtu mwenye jazba na mihemko na ulimi usiokuwa na haya na aliyekosa subra.Hafai hata kuwa Mjumbe wa nyumba kumi zaidi ya kuwa kiongozi wa familia yake ambayo nadhani hata yenyewe itakuwa inaathirika vibaya na tabia zake.
 
Back
Top Bottom