Nadhani mabeberu wa nchi za Magharibi wanaelekea kulielewa somo sasa: Chezea kingine ila siyo sharubu za Putin

Nadhani mabeberu wa nchi za Magharibi wanaelekea kulielewa somo sasa: Chezea kingine ila siyo sharubu za Putin

Mabeberu kwa lugha ya kiingereza ni imperialists! na sera yao inaitwa imperialism! Ni watu watu wenye hulka ya kutaka kutawala kila eneo! lengo lao kuu ni kujitanua kwa kutumia mabavu ya kiuchumi na kijeshi!! Mfano mzuri ni marekani!! a policy of extending a country's power and influence through colonization, use of military force, or other means. Kihistoria hii ndiyo dhana ya ukoloni. Kwa leo tunauita ukoloni mamboleo!! Mabeberu hawaamini kama tunaweza kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo yetu kwa kuongozwa na maslahi yetu!!
Kwenye huu uzi mabeberu wamegonga mwamba kwa PUTIN!! Walikuwa na ndoto za kujitanua hadi Ukraine kwa mgongo wa NATO!! Kwa mtazamo wa urusi, NATO ni nyoka, hapaswi kupewa nafasi ya kujinafasi hadi ukraine ambayo ni sehemu nyeti sana kijeshi!
Umemaliza baba maana alijitoa ufaham kuwa ndo mara ya pili kusikia hilo neno
 
Naona unashabikia kitendo cha nchi moja kutaka kuwa na umiliki wa maamuzi ya nchi nyingine. Yani Ukraine achaguliwe marafiki na namna ya kuishi.

Pia unashabikia nchi moja kujimegea maeneo ya nchi nyingine na kujimilikisha kwa kisingizio cha referendum uchwara ambayo anaepiga kura ni mateka huku akiwa amesimiwa na mtutu wa bunduki

Pia unashabikia nchi moja kufanya uvamizi usio halali na kuingia nchi nyingine kwa vifaru mabom kisha kuua Raia(mauaji ya halaiki??), kuharibu mifumo ya nishati, kulipua majengo na kila aina ya uharibifu.

Pia unashabikia wavamizi wanaoangamiza taifa jingine kwa sababu za kijinga kabisa.

Ukraine ana haki ya kujilinda na aina yoyote ya uvamizi, uporaji na kila aina ya tukio linalohatarisha uwepo wake katika ramani ya Dunia.

What goes around comes around. Fikiria sisi kama nchi tufanyiwe anachofanyiwa Ukrane na Nchi jirani kwa muktadha wa kulinda usalama wake kisa sisi kuwa na urafiki na nchi flan tunahatarisha usalama wake.

Naamini ungefurahia vilevile.
Watu ni wapumbavu mnoo mkuu, inashangaza mnoo kwa huu ushabiki wao.
 
Hiyo si ndio kazi ya hawala yenu Marekani?,au umesahau?
 
Usicheze na nchi yenye maliasili zinazohitajika kwa lazima kwa maisha ya kiila siku: mafuta na gesi!!! Usicheze na nchi inayojitegemea na kutegemewa kwa chakula!! Hapo ndipo urusi ilipozikamatia pabaya nchi za kibeberu!!
Isipokuwa Tanzania na jamaa zake
 
Nashukuru!! Ila ujue nchini kwetu kuna wanyarwanda wengi sana ambao wanadai kuwa ni watanzania! Mnyarwanda ni kama myahudi, hasahau kwao! Hata akipata uraia wa nchi nyingine, anajihesabu ni mnyarwanda kwanza kisha huo uraia mwingine ndo unafuata!! Tulipokea wakimbizi wengi sana wanyarwanda miaka ile ya sabini. Wengi wao wameshakuwa raia wa Tanzania na kizazi chao wote (wanazaana sana) ni raia wa Tanzania lakini mioyoni mwao wanajihesabu ni wanyarwanda!! Ukitokea mgogoro kati ya Tanzania na Rwanda lazima kwa siri au kwa wazi watakuwa upande wa Rwanda!! Watatuhujumu na hatutawaweza!

Hilo ndilo tatizo la Marekani kuhusu wayahudi!! Marekani kuna wayahudi wengi ambao wamekuwa raia wa Marekani lakini mioyoni mwao bado wanajihesabu kuwa ni wayahudi. Wako kwenye kila sekta muhimu huko marekani, kwa hiyo marekani inalazimika kuitetea Israel hata kama haipendi vinginevyo itakula kwake!! Asante kwa kunitukana lakini huo ndio ukweli!!!

Watusi waliposhika tena utawala nchini nRwanda chini ya Kagame, watanzania wengi wenye asili ya Rwanda huko Kagera walirudi Rwanda kwa maelfu!! Siidharau nchi yangu wala si kwamba hatuna nguvu, lakini kupigana na kilichoko nguoni mwako ni maafa!!
Kuwa mnyarwanda sio ishu. Ishu kusema kwamba wataweza mziki wa jwtz. Ivi wewe Rwanda Sawa na Kagera mkoa. Leo useme ipambane na Tanzania ni upuuuzi tuuu. Kwanza ujue Kagera mkoa kuna kizazi cha kinyarwanda, Kirundi na kiganda. Kwa iyo kusema watamsaidia kagame ni uwongo mwingi sana. Mimi Mama anagu ana asili ya kinyarwanda wa Kagera na miaka iyo alienda JKT ya kipindi icho miaka ya 1975. Na Mke wangu ana asili ya kinyarwanda na wamezaliwa apa apa Tanzania na hawana uo upuuuzi kama wako wa kusema sijui watamsaidia Rwanda.
 
Umemaliza baba maana alijitoa ufaham kuwa ndo mara ya pili kusikia hilo neno
Aliyejitoa ufahamu ni nani? Mimi?!

Mwenzako unayempongeza anadai kuwa ubeberu ni "extending a country's power and influence through colonization, use of military force" na kadhalika.

Mimi nimemuuliza swali dogo tu: aliyeivamia Ukraine kijeshi naye ni beberu ama si beberu? Ameishia kuikana definition yake mwenyewe.

Nani aliyejitoa ufahamu hapo?
 
Wamemwekea vikwazo lukuki wakiamini kuwa uchumi wa urusi utakufa ghafla, kinyume chake uchumi wa nchi zao ndio unaoanguka!! Usicheze na nchi yenye maliasili zinazohitajika kwa lazima kwa maisha ya kiila siku: mafuta na gesi!!! Usicheze na nchi inayojitegemea na kutegemewa kwa chakula!! Hapo ndipo urusi ilipozikamatia pabaya nchi za kibeberu!!

Ukigomea mafuta na gesi yake wengine wengi tu wanachukua na wewe bei inakuwa juu kwa kupungukiwa na bidhaa hiyo muhimu!! Wanaumiza kichwa: Tumfanyeje PUTIN? kumpindua hatuwezi! tukimtenga wengine wanamkimbilia!! Tumsapoti Ukraine kwa silaha ndo kwanza anahalalisha majimbo manne kuwa sehemu ya urusi!! Kuyakomboa ni kuingia vitani na urusi!!

Ni nani mwenye ubavu huo-hakuna!! Tuifundishe ukraine kufanya ugaidi ndani ya urusi kama kushambulia daraja la crimea kwa mbinu za kigaidi: hapo sasa ndo kwanza umechezea sharubu za Putin, ametembeza kichapo cha masaa kadhaa ambacho hajawahi kukitoa tangu vita vianze na kuna kilio kote kwenye ulimwengu wa magharibi!.

Sasa USA wamesema watapeleka mitambo ya ulinzi wa anga lakini urusi ana supersonic missiles zinazopenya kwenye ulinzi wowote wa anga!! Asikudanganye mtu, Katikati ya jiji la kiev kulikuwa kunalindwa na hiyo mitambo ya ulinzi wa anga lakini pamechakazwa usipime!! Tumfanyeje PUTIN? Mimi niwape jibu, ni rahisi sana!!

Acha kupeleka silaha ukraine na hapo Ukraine haitakuwa na ubavu wa kuendeleza kiburi na vita vitakomea hapo!! Ila kuhusu yale majimbo manne yaliyojiunga na Urusi, hiyo ni hasara ya ukraine ya milele!!

Kingine Ukraine itabaki ikiugulia na madeni hadi mwisho wa dunia!!
Unaota
 
Kaka mbona kla siku Israel anayachukua maeneo ya palestna???sijackia USA Wala EU kuiwekea vkwazo Israel
Kwani lazima wawekewe vikwazo na Us au EU. Na nyinyi mataifa ya hovyo ya Afrika wawekeeni vikwazo kama mnaweza maana hakuna aliyewazuia.
 
Juzi EU wamemwomba Putin aruhusu ngano itoke.
Yaani mnajifanya mnokmaa na vita alafu kumbe mna njaa
 
Back
Top Bottom