Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kuna uwezekano mkubwa kwamba malalamiko kuhusu ubovu wa katiba ya Chadema, yalichochewa na chuki binafsi dhidi ya wagombea uongozi Fulani ndani ya chadema, na kwahivyo hakuna haja ya viongozi hao walalamishi wenye chuki binafsi dhidi ya watu binafsi, kuhamishia na chuki hizo binafsi kwa wengine kwa namna ingine.
Na kama ilikua ni utapeli na hadaa za kisiasa kwaajili ya kuwarubuni wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa ili wawachague ni vema wakajistukia kwamba sio wote wanaweza kutapeliwa fikra kirahisi hivyo.
Kulikoni agenda kuu ya chadema iwe kuchangisha pesa za matumizi na sio mabadiko ya katiba yao waliyoiita mbovu sana?
Kulikoni wasianze kwanza kufanya kwanza marekebisho ya katiba yao kabla ya kuanza kuhitaji marekebisho kwingineko?
Je, ni kweli tatizo ndani ya chadema ilikua katiba au chuki binafsi dhidi mtu binafsi ambayo sasa inataka kusambaswa kwa wengine hata wasiohusika na hiyo chadema yenyewe?
Je, muendelezo wa madai ya viongozi wa chadema kuhusu mabadiko ya sheria ambazo tayari yameshafanyika sio chuki binafsi za vibaka na matapeli hao wa kisiasa dhidi ya viongozi waaandamizi wachapakazi na waadilifu serikalini?
Kuna methali ya kiswahili inasema, Nyani haoni kundule, huliona la mweziwe. Je, chadema wana tabia za nyani, maana hawayaoni makosa yao, ila wanaona ya wengine pekee na kuanza kubwekabweka?.
Ni muhimu kama Taifa kujianda kwaajili ya uchaguzi mkuu utakao fanyika mwezi October mwaka huu 2025 bila kubabaishwa na kelele za vibaka na matapeli wa kisiasa waliopoteza uelekeo nchini.🐒
Mungu Ibariki Tanzania