Nadhani tuna haja ya kujadili mambo ambayo wasanii wetu wanayafanya ambayo kwa kiasi kikubwa yanaharibu utamaduni wetu

Nadhani tuna haja ya kujadili mambo ambayo wasanii wetu wanayafanya ambayo kwa kiasi kikubwa yanaharibu utamaduni wetu

Author

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
1,715
Reaction score
8,058
Habari wana JF

Nadhani tuna haja ya kujadili mambo ambayo wasanii wetu wanayafanya ambayo kwa kiasi kikubwa yanaharibu utamaduni wetu na yatapelekea vizazi vijavyo viyaone ni ya kawaida.

Nyakati wa uvaaji wa mlegezo (kata K) watu walipinga sana na kusema ni uharibifu wa tamaduni zetu
Baadae ukaja mtindo wa kusuka kwa wanaume, kukawa na lawamaa za kupinga na sasa limekuwa jambo la kawaida.

Ukaja mtindo wa kuvaa hereni kwa wanaume na nguo fupi kwa wadada na sasa limeonekana la kawaida, ukaja mtindo wa kuvaa nguo za kubana na kuonyesha mauongo kwa vijana wakiume na wakike nalo limeonekana la kawaida...na sasa uvaaji wa vikuku kwa wanaume nalo litaonekana la kawaida baadae.

Tutakuwa na jamii ya aina gani?.

Haya yote yanapitia kwa wasanii na wengine wanaiga....
Tunadhani tunawezaje kupambana na upotofu huu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora ya maboya yataelea kwenye maji ila kwa wao wache wapige deki kwa watangaazaaji,mademu wanawapitia makwao hawawangojei CD za show wanaenda kuwauliza ma DJ.
 
achana nao, we fanya yako wala hutoumiza kichwa.
 
Hakuna namna.... Ndio asili ya usanii maana usanii nao unatamaduni ,ikifika mahali hadi maofisini wanafanya hivyo ndio itakua tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wasanii wanachangia kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili haswa uvaaji kwa vijana
 
Katika vyote hapo mie wameninasa kwenye mlege tu. Hayo mengine nawaachia wenyewe
 
kusuka rasta za prima
unakuta janume limevaa kikuku halioni aibu

hayo mambo mikoa ya kaskazini mpaka kaskazini mashariki hayapo kabisa
ila Dar
 
Ndo maana wanaitwa wasanii, huwa unajisikiaje mtu akikuambia "Acha usanii bwana" haahaa Hapo ushaelewa msanii ni mtu wa aina gani
 
TENA SASA KUNA MTINDO WA KUPAKA KUCHA RANGI NIMEANZA KUONA KWA WASANlI WA MAREKANI KM TYDOLLAR SIGN WIZKHALIFA NA BAD BUNNY SOON UTAKUJA BONGO HUO MTINDO
 
TENA SASA KUNA MTINDO WA KUPAKA KUCHA RANGI NIMEANZA KUONA KWA WASANlI WA MAREKANI KM TYDOLLAR SIGN WIZKHALIFA NA BAD BUNNY SOON UTAKUJA BONGO HUO MTINDO
hao wapo, ktk Kufinikish agenda.

69, check swag zao, mara matattoo ya Maua uson, sijui nn,
 
Back
Top Bottom