Nadhani tunahitaji vyuo vingi vya Ufundi stadi

aah! unamzungumzia yule jizi
 
Nimeongezea tu vijana wote wapewe skills wasiachwe njiapanda.
Vijana wote wakiwa na ujuzi huwezi kuta panyaroad mtaani.
 

Ameanza vizuri, Mdogo KILA mwaka akitenga bajeti ndani ya miaka KILA kata itakuwa na veta.
 
Serikali ingepunguza au iache mpango wa kutoa mikopo kwa elimu ya juu. Bora hizo pesa ijenge Veta KILA kata na iwakopeshe vijana ujuzi. Vijana wapate ujuzi kwa kujisajiri kwa kuwa na NIDA na TIN number hapa ni rahisi kufatilia pesa za mikopo ya elimu kwa maana tayari upo kwenye mfumo huwezi kimbia. Mkopo mnautoa kwa mhitimu mmoja wa chuo ambae akimaliza chuo ataishia kuwa machinga au bodaboda ungetosha kuwapa ujuzi vijana 30,mtu akiwa na ujuzi skills hawezi kuwa masikini atachochea uchumi kuliko hii ya kukopesha wanafunzi wa vyuo pesa wakimaliza vyuo uishia kuwa machinga.
How come unatumia miaka 20 darasani then unakuja kuwa machinga au bodaboda kwa sababu Hakuna mfumo wa kuwaajiri wahitimu nini hii si ni upumbavu huu, kwann usimalize tu la saba uwe bodaboda kuliko kupoteza mda mashuleni.
 

Nakubaliana na wewe Mkuu, watu wangepewa skills kila mtu akazalisha vizuri then uchumi ukiongezeka hapo baadae labda ndio tufikirie kuongeza ujuzi kwa watu wa juu (vyuo) kwa sasa we need to use the litlle of what we have efficiently kutuvusha kwenda next stage.
 
Kuondoa umasikini katika nchi ni kitu chepesi Sana, sema tu umasikini ni mkakati wa makusudi kabisa unaowanufaisha walamba asali na chama chao kwa msemo wa usiwaamshe waliolala mtalala nyie.
Ili wao wazidi kuishi ni lzm umasikini Uwepo.Thus utumia mifumo kama kodi,tozo,makatazo,nk kuwabana watu wasimudu kujikwamua.
 

Umenikumbusha miaka mingi iliyopita Mkuu
Ilikuwa miaka ya 70 nilipokutana na Mzungu mmoja naona yeye alikuwa carpenter by professional ila aliingia naona nchini kama Padre na alikuwa na kanisa na karakana yake

Akawa anasajili wanafunzi kuwafundisha kutengeneza milango, madawati, meza, viti you name it

Hapo vijana watalipa Ada ya kozi hiyo ila sasa Mzee akaniambia Yaani hii kazi nchi hii pekee nalipwa kuwafundisha hapo hapo nauza bidhaa hizi na kupata hela mara 2
Alikuwa ananunua mbao kwetu miaka hiyo

Kweli nimekumbuka old days
Kuna watu wanawaza hela haswa
 
Muwe hata mnafuatikia mambo ya serikali,nyie huwa mko busy na nini hasa kiasi kwamba unakuja kukosoa wakati hata hujajipa mda wa kutafuta habari sahihi kabla ya kuja hadharani?👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220613-184312.png
    129.1 KB · Views: 8
Ni upuuzi kuwa na mawazo kama haya.
 
Huu ni utoto unaongea..

Haiwezekani kwa nini? Hujasikia Serikali itaondoa matumizi ya magari na pesa zitakazookolewa huko zaidi ya bil.500 kutumika kwenye mikopo ya Wanafunzi wa ufundi na kuviendesha.
 
Muwe hata mnafuatikia mambo ya serikali,nyie huwa mko busy na nini hasa kiasi kwamba unakuja kukosoa wakati hata hujajipa mda wa kutafuta habari sahihi kabla ya kuja hadharani?👇
Sitakagi kukujibu, naomba usiwe unajibu mada zangu please, nahisi unalipwa kuandika upuuzi kwenye forum ya bwana Melo!
 
Sitakagi kukujibu, naomba usiwe unajibu mada zangu please, nahisi unalipwa kuandika upuuzi kwenye forum ya bwana Melo!
Utapata pressure na ulcers kwa upumbavu wako..

Yaani upotoshe afu usijibiwe? Tena una bahati sikuangalia kwamba ni wewe ulianzisha thread ningeanza kwa kukuponda maana una bichwa kubwa harafu umejaza mausaha kichwani.
 
Program hii ipo tangia enzi za NVTC kabla hata hilo jina halijabadilishwa kuwa VETA sema wewe ndio ulikuwa haujui.

Lakini kwa miaka ya sasa pamoja na watu kurasimisha ufundi wao au ujuzi bado hawana nafasi ya kuajiriwa iwe serikalini au mashirika binafsi kwa kigezo cha form four, sasa bado tatizo lipo pale pale la kiajira zaidi ni mtu kuwa na karatasi(cheti) ambacho bado hakikusaidii ndani ya nchi yako tofauti na miaka ya NVTC.

Najua utasema teknolojia imebadilika lakini je hionteknolojia sisi kwa mahitaji yetu inazuia watu wenye ujuzi wa kati kutokufanya kazi hizo??

Mfano, udereva,ufundi umeme wa majumbani, mechanics,ufundi bomba, ufundi bodi, useremala je ni kweli sifa hizi zinahitaji sana elimu ya zaidi ya darasa la saba?
Suala la lugha ni muhimu sana kuijua na hili ni la watu wote iwe la saba au chuo kikuu.

Matatizo ya kiajira na kujiajiri nchi hii hayawezi kutatuliwa na hawa wanasiasa ambao ni selfish.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…