Program hii ipo tangia enzi za NVTC kabla hata hilo jina halijabadilishwa kuwa VETA sema wewe ndio ulikuwa haujui.
Lakini kwa miaka ya sasa pamoja na watu kurasimisha ufundi wao au ujuzi bado hawana nafasi ya kuajiriwa iwe serikalini au mashirika binafsi kwa kigezo cha form four, sasa bado tatizo lipo pale pale la kiajira zaidi ni mtu kuwa na karatasi(cheti) ambacho bado hakikusaidii ndani ya nchi yako tofauti na miaka ya NVTC.
Najua utasema teknolojia imebadilika lakini je hionteknolojia sisi kwa mahitaji yetu inazuia watu wenye ujuzi wa kati kutokufanya kazi hizo??
Mfano, udereva,ufundi umeme wa majumbani, mechanics,ufundi bomba, ufundi bodi, useremala je ni kweli sifa hizi zinahitaji sana elimu ya zaidi ya darasa la saba?
Suala la lugha ni muhimu sana kuijua na hili ni la watu wote iwe la saba au chuo kikuu.
Matatizo ya kiajira na kujiajiri nchi hii hayawezi kutatuliwa na hawa wanasiasa ambao ni selfish.