Nadharia mpya kuhusiana na matatizo fulani ya mfumo wa neva na kupelekea kupooza kwa viungo

Aisee we jamaa ni muongo sana. Dah [emoji58]Yaani imani ya mtu inahusiana hadi na seli. Si useme tu unaeneza neno!

Ubongo una maeneo yasiyowasiliana karibu muda wote ili yasiingiliane kazi. Kazi mwilini ziko nyingi, hakuna anayezaliwa akijua mwili unafanyaje kazi. Kinachojua kazi hizo ni seli zenye kazi husika. Imani na uongo mwingine zinafundishwa kama nadharia zingine. Hata Kuja kuelewa function za organ ni baadae. Ndio tuelewe maisha sio imani. Kimoja ni uhalisia kingine porojo.

Unaweka mkao kama unatoa elimu kumbe unasambaza hadithi za uzushi.

Subconscious functions na conscious actions haziko na ukaribu unaojaribu kudanganya. Ni uongo kuleta dhana kwamba bila imani inapelekea cell misbehavior. Unafikaje kwenye hizi hitimisho zako? Ni bora uwe unaweka vyanzo vya hizi taarifa zilizojaa utata.

Nilidhani uliteleza uzi mmoja, kumbe zote ni vielelezo vya mungu tu bila taaluma yoyote!
 
Masdinero masdinero tafadhali unataka kufanya kosa ambalo skeptic hatakiwi kuenenda hivyo. Hapa hoja sio kwamba jambo hili lipo au halipo.

Hoja ya huku ni athari za imani binafsi ya mtu na muenendo wa seli zake jaribu kuichunguza hiyo. Hata mimi hapa nimeileta kama mada ya utafiti mezani.

Imani yangu isikubabaishe, imani yako isikusimamishe ichunguze hiyo hoja kama hoja
 
Ngoja nitatafuta mda nimsome ili nijue, labda nifunguke maana mi tafiti yangu bado inaendelea. Ukipata mfano mwingine niambie ili tuachane na hiki mnachokiita 'uzushi'
 
Ngoja nitatafuta mda nimsome ili nijue, labda nifunguke maana mi tafiti yangu bado inaendelea. Ukipata mfano mwingine niambie ili tuachane na hiki mnachokiita 'uzushi'
Huko itaenda kusoma hata baadaye lakini niache kwanza na uthibitisho hapa wa kuonesha Mungu yupo niendelee kuusoma
 
Hapana, kwa huku hili sio lengo la mada. Uthibitisho wa wazo la Mungu tunaendelea kuufanyia kazi kule kwenye mada ya Mwanabaiolojia, uhalali Mungu
Basi wacha mi nikomee hapa kama hakuna uthibitisho, hakuna ukweli.

Sioni sababu ya kustick kwenye mada yenye mlengo wa kupotosha watu ikitaka waamini claims zake bila uthibitisho

Hii mada inawahitaji sana faithfoolers kuliko freethinkers
 
Haya tunayaweka wazi ili tupate watu wengi zaidi wa kuyachunguza.

Mfano ukiachana na hilo la kupooza yapo na mengine Mengi tu, mfano kisukari:

Nikileta nadharia ya kwamba imani kwamba; "pesa ndo kila kitu, na kuwa nazo nyingi ni jambo zuri. Jitahidi ujikusanyie na kutunza pesa za kutosha. Usizitumie kuwa bahili" inapelekea seli ndani ya mwili kuamini kwamba "Sukari ndio kila kitu, kuwa nayo nyingi ni jambo zuri. Jitahidi ujikusanyie na kutunza sukari ya kutosha. Usitumie sukari kuwa mchumi. Nikasema kuwa zote hizi ni imani mbaya na matokeomyake sio ya afya

Bali imani nzuri ni [nadharia inaendelea] "Pesa ni muhimu kuendesha maisha yetu kijamii. Jitahidi utafute pesa kulingana na matumizi yako. Tunza kiasi tu lakini nyingi ziwekeze kwenye shughuli za kuzalisha mali ma kusaidia wewe familia na jamii kwa ujumla. Pesa itumike kwa mambo ya maana." kwamba itapelekea seli za mwilini nazo kutumia sukari kwa mtindo mzuri. Kuipata sukari kuitumia kujilisha na kusaidia shughuli za mwilini?. Nasisitiza hizi ni nadharia tu. Sina mamlaka bado ya kitafiti. Tusaidiane kutafiti wote
 
Basi wacha mi nikomee hapa kama hakuna uthibitisho, hakuna ukweli.

Sioni sababu ya kustick kwenye mada yenye mlengo wa kupotosha watu ikitaka waamini claims zake bila uthibitisho

Hii mada inawahitaji sana faithfoolers kuliko freethinkers
Bado tafiti zinaendelea, na maanisha uchunguzi unaendelea. Na freethinkers ndo mnakaribishwa. Nimetoa mfano wa imani usiomuhusisha mungu hapo juu #47. Ili tuijadili tu imani kama imani.

Imekaa hivyo jamani nasisitiza kuwa lengo la hii mada lili kuwa ni kujadili imani na sio imani ya kidini. No. Hizihizi tu imani zetu mbalimbali je tunahisi zinaishia hewani tu au zina madhara yanayopimika kabisa?
 
Inamaana unataka kusema S. Hawking afya yake ilichagizwa na imani yake ya kutoamini mungu?
Kitu kama: nadharia hii imejikita zaidi kwenye imani, yaani jinsi alivyoamini katika ulimwengu ulivyo na uongozi wake ndio ilichagiza mwili wake kuitikia vile. Ni nadharia bado tunakusanya data mfano below👇
 
Nipo kufuatilia hapa, kujua imani yake lakini inaniwia vigumu kwa sababu vyanzo vyangu vya taarifa ni kiduchu. Siwezi kuvinunua vitabu vyake ila nategemea reviews ambazo ni mawazo ya watu yanaweza yasiwe yanamuwakilisha vizuri yeye! Kama ningesoma vitabu vyake kiukamilifu ningekuwa na ushahidi zaidi kwa imani yake kuhusu mungu na ulimwengu mzima unavyoendeshwa ilivyokuwa.

Uchunguzi unaendelea lakini mfano nikasema: 1.Alimuamini Mungu ndio lakini pia imani yake ilijengwa na fujofujo za duniani hadi akaelekea kuamini tupo katika mwisho wa dunia ifikapo 2000[the end]. 2. Alionekana kutoamini kama mamlaka zinaweza kuongoza vizuri bali labda watu wajiongoze wenyewe [blinded by might].

Labda alifika mahala akaishi akiamini kuwa'sasa hakuna sheria wala mamlaka ya maana tupo tu tunasubiri Yesu ashuke hivi karibuni'. Watu wanaoamini mwisho wa dunia umefika samtaimu wanaachaga kufanya kazi. Ndo mambo yakaanza mwilini kuunga mkono hoja!! Sasa sijui kama hizi dots nnazoungaunga zina ukweli au ni bias zangu zinaendelea?

Kumbuka hoja hapa sio kuamini au kutoamini mungu hoja ni kwamba hiyo imani yako ipojepoje, je unaamini ulimwengu/dunia ipojepoje je ina kiongozi au haina na uongozi wake upojepoje? Kama ni kani mbalimbali zipoje, je ni order au ni chaos? Ile imani kwa ujumla je inaathiri miili yetu? Hicho tu.

Nazitegemea kwelikweli critisisms zenu wana ili tuondokane [au tuendelee] na hii nadharia;
 
Sababu za uwepo wa maajabu fulani ambayo kwa ufaham wa mwanadamu kashindwa kuujua kiundani haimaanishi kuwa point ya kuprove uwepo wa Mungu.

Kuna hawa wanaochukua vifungu vya vitabu vya dini zao as reference ya kuprove uwepo wa Mungu, hawa nao ni wajinga maana wanakuwa hawana imani pasipo kutegemea hayo mavitabu yao, na pia inaonesha kabla ya ujio wa dini mababu hawakuwa na imani ya Umungu nje ya izo dini? Na je dini zisingekuja vipi mnge quote wapi vifungu ili tumjue huyo Mungu?

Elimu hii ni ngumu na wala haihiatji ujuaji na kuwahukumu wanaopinga uwepo wa huyo Mungu, maana kuna mengi yameshaharibiwa kuhusina na imani ya kweli, so kila mtu abaki akiamni ajuacho kulko kuwaforce wengine waamini uwepo wa Kitu ambacho binafsi kimeshindwa kujitetea kuwa kipo bila ya kuwatumia wanadamu dhaifu.
 
Kitu kama: nadharia hii imejikita zaidi kwenye imani, yaani jinsi alivyoamini katika ulimwengu ulivyo na uongozi wake ndio ilichagiza mwili wake kuitikia vile. Ni nadharia bado tunakusanya data mfano below👇
Unazungumzia vipi wale watoto ambao siku yao ya kwanza kuzaliwa wanakuwa wamezaliwa na matatizo mbalimbali mfano mzuri ni watoto kuzaliwa katika hali ya mdogo sungura au sehemu ya miili yao ikiwa imeungana. Je hawa watoto huwa wanaanini nini?
 
Unazungumzia vipi wale watoto ambao siku yao ya kwanza kuzaliwa wanakuwa wamezaliwa na matatizo mbalimbali mfano mzuri ni watoto kuzaliwa katika hali ya mdogo sungura au sehemu ya miili yao ikiwa imeungana. Je hawa watoto huwa wanaanini nini?
Ndugu yangu sijakataa wala sijasema kuwa maambukizi ya bakteria si kitu.
Wala sijakataa kama ajali zinatokea na kuharibu afya
Kwamba kuna miale inaweza kusababisha uharibifu wa afya [harmful radiation]
Mambo yote, kemikali ngeni na upungufu wa vitamini ni baadhi ya visababishi

Nnachojaribu kuuliza hapa ni 'Je tunaweza kuiweka na imani nayo kama chanzo mojawapo cha kuhifadhi/kuharibu afya kwa mwanadamu?'

Maana ukiangalia hizo sifa hapo juu zinamuweka mtu kama muhanga, hapa tunataka kuipeleka mbele kidogo elimu na kumpa mamlaka mtu awe ndio mtendaji:
 
Nisamehe sana kama umeona ninahukumu? I am a mere mortal here mimi kama nani? Sema hii mada inapendekeza kwamba isije kuwa tupo tunajihukumu wenyewe kwa namna tunayochagua kuamini!?

Kakaa, una uhuru wa kuamini chochote na vyovyote unavyotaka. Ninachojaribu kugusia hapa ni kwamba je tunao ushahidi kwamba imani yako inaweza kukuponya/kukuangamiza?

I mean kama tupo na tunaishi duniani penye aina nyingi tu za ukweli na uongo unaoweza kuufuata[free will]. Kwa nini tusichague at least zile kweli ambazo zitatusaidia kufurahia maisha yetu hapa duniani. Na kama yapo mengine zaidi ya hapa nayo tutajitahidi kufanya chaguzi za kuyafaidi pia.

Jiambie tu mwenyewe kwamba kama nitayaishi haya maisha, basi nitajitahidi kuyaishi vizuri.
 
Afu kinginee Kwa Ushindi victory na Scars na wengine mnaokomalia kutaka uthibitisho wa Mungu, tena muda mwingine mnaenda mbali kutaka ajitokeze mbele yako physically laivu ajithibitishe hamjajua tu kile mnachokiomba. Poleni sana.

Kutokana na utukufu alionao ikitokea akaamua kujitokeza kwako nikwambie ndugu hautabaki majivu, bali hata hayo majivu yatavukishwa na huo mvuke utatawanyika uwe atomu nazo zivunjikevunjike yaani hautaona hata kavumbi ka matirio ya mwili wako. Hiyo ni kutokana na ule tunaita utukufu, utukufu ni zaidi ya nguvu maana wenyewe ndio msingi hata wa hizo nguvu zenyewe. Hayupo mtu anayeweza kumutazama Mungu na akaishi. Utawaona malaika wake, utaziona nguvu zake kama moto etc lakini Yeye ukimuona utabaki mvuk... no.. hapana... hata mvuke wako hautaonekana.

Lakini njia ambayo inatumika ni ile ya kuwasiliana ki-roho na watu waliokuza vyeo vyao kiroho. Nayo sio directly ni kama resonation, resonance bila kugusana. So mitume na manabii wanapo-resonate na ujumbe wa Mungu basi wanatuambia na sisi hayo ndiyo mafunuo na unabii.

Lakini usijione mdogo, kila mmoja anayo nafasi ya kuresonate/kuitikia na mambo ya kiroho inaanza tu na yeye kukubali kuwa wake Mwenyezi. After all imani ni mahusiano binafsi kati ya kiumbe na Mola wake. Haya makundi ya umoja yanatusaidia maana tunajumuisha elimu ya kila mmoja wetu. Mtu anaweza kuwa mkristo au muislamu lakini kwa imani yake binafsi. Sasa mimi natafuta athari za imani binafsi sio ya jumuiya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…