butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Upo sahihi Hali ya maisha ya Watanzania ni nzuri sana kama raia wa nchi za Scandinavia kule Ulaya!si kweli kwamba hali ya maisha ya watanzani ni mbaya.
nachelea kudhani hali yako binafsi yaweza kua mbaya,
hiyo ni sawa, na naushauri ujipange na kurekebisha, inawezekana kabisa kutoka kweye hali hiyo.
unasema, umeme ni shiida, maji ni shida, dawa ni shida nakadhalika nakadhalika.
ukweli ni kwamba huduma zote hizo zipo katika ukamilifu wake,
ispokua wewe ndie huridhishwi na kiasi au kiwango cha upatikanaji wa huduma zenyewe.
ni vigumu kumridhisha kila mtu,
changamoto, uchache, kutojitosheleza kwa huduma hizo, kasoro, upungufu na udhaifu ni vitu ambavyo serikali kutwa kucha wanavifanyia kazi na kuendelea kuviimarisha ili hatimae viweze kukidhi mahitaji ya watanzania wote.
Ziara hizi za Rais,
Ni muhimu sana na kwakweli zitachochea ukuaji wa kisekta kwa namna mbalimbali.
Mawaziri wa kisekta wanakwenda kuchota uzoefu, technolojia, mipango na mbinu mablimbali wanazotumia wenzetu katika kuimarisha na kutooa huduma muhimu kwa watu wao.
kupanga ni kuchagua....
Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app