Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
- Thread starter
- #41
Nd. Mchambuzi,
Unasema, " Mwaka huu ni muhimu sana kwangu kuhusu maamuzi magumu." Kwanza sisi vijana wa nchi hii ili tuendelee inabidi tuachane na "siasa za maji taka" kama utumiaji wa maneno vague na meaningless kama mfano "maamuzi magumu" , "Kujivua gamba" etc. Hii misemo inatugharimu sana kama Taifa. Tujiulize ni nguvu kazi kiasi gani imepotea kwa wananchi kudiscuss maana ya hii misemo?
Wewe kama young professional tunayekutegemea kwanza inabidi utuambie unategemea mabadiliko gani pindi ikifikia Dec2012? Kama mategemeo yako yasipotimizwa (yote au baadhi), utaamua kuachana/kujiondoa kwenye CCM? Maana sijaona mahali ulipoweka wazi kuwa a,b,c ... zisipotimia basi ni time ya kuondoka CCM. Otherwise kama unaendelea kuongea kwa kutumia lugha za viongozi wako nawe utakuwa huna tofauti nao. Yaani unakuwa unaitumia JF kama platform ya kujijenga ndani ya CCM as "a Young turk" wakukumbuke kwani unajua bigwigs wa CCM wanategemea JF for reliable political news. Mwanakijiji amekusaidia kuweka wazi kabisa jinsi gani hizo changes zilivyo shallow na sijaona CCM diehards hata mmoja aliyejitokeza kuja kumpinga kuwa hajui political reality ya TZ kwa kuwa yupo Nje. Naona tunajadili jinsi gani ya kuzuia inevitable yaani pending kifo cha CCM similar to KANU. Unasubiria kuachana nacho pale tu daktari atakapo declare kuwa kimekufa, huoni kuwa CCM imeshapoteza dira, moral authority? Binafsi thinking hiyo ya kusubiria naifananisha na watu wanaoitwa "Political Opportunists" ambao daima ni hatari sana kwani leadership skills zao kikomo chao huwa kipo chini, mfano hai ni Dr, Baba Mwanaasha, Vasco D-G, Msanii na mengineyo....hayo majina yote yametokana na mapungufu makubwa aliyonayo kiongozi wenu.
Ni hayo tu ndugu yangu, siasa njema.
Angalizo: Sijakushauri ujiunge na chama chochote kwani natambua unaouwezo wa kupima vilivyopo kama vinafaa au la, na pia unaweza kuanzisha cha kwako.
Gogomoka,
Asante sana kwa mchango wako mzuri. Naelewa msingi wa hoja yako. Lakini naomba nitoe ufafanuzi kidogo. Uamuzi mgumu mimi nadhani ni neno zuri tu, ili mradi unalitumia inavyotakiwa. Kwangu mimi, uamuzi mgumu ni 'opportunity cost', kwamba ukichagua kitu kimoja, basi uwe tayari kuachana na kingine by 100%. Katika mazingira ya hoja yako, huo mchakato sio mrahisi kwangu kwa maelezo yafuatayo:
Kama umekuwa unanifuatilia huko nyuma, mimi tatizo langu na vyama vilivyopo ni itikadi. Najaribu sana kuepuka kujiunga na chama fulani kwa sababu ya umaarufu wa muda mfupi kama vile ilivyotokea kwa NCCR miaka ya tisini, ambapo umaarufu wake ulitokana na personalities/majina makubwa - lamwai, kaborour, mrema, bagenda, marando... pamoja na kelele za ufisadi ambao ulikithiri chini ya serikali ya mwinyi. Haikuchukua muda umaarufu kwa NCCR ukafa kwa sababu kilijipanga zaidi kuingia ikulu, lakini mbaya zaidi kwa kutegemea vitu ambavyo vinakipa uhai chama kwa mufa mfupi tu, badala ya itikadi iliyo sheheni Alternative to IMF Development Agenda. Hakuna chama chenye maelezo yake kwenye katiba kuhusu foreign policy in the context of development zaidi ya kusema kitashirikiana na vyama vingine afrika, duniani....
Mambo yale yale ya NCCR 1990s yameanza kujitokeza tena katika siasa za sasa - umaarufu wa personalities na kelele dhidi ya ufisadi, huku wakiwekeza almost nothing kwenye itikadi ya maana. Itikadi zinazofuatwa na CCM, Chadema, CUF hivi sasa ni ya uliberali i.e. 'IMF development alternative' ambayo haitamwokoa mtanzania wa kijijini. Uliberali ndio sababu ya watanzania kuwa maskini, ndio uliozaa azimio la ovyo la zanzibar, ndio unaolea ufisadi, ambapo ubepari umepotezewa meaning na ufisadi. CCM na serikali yake wapo busy kusafisha mafisadi badala ya kusafisha ubepari uliochafuliwa na mafisadi.
Ni muhimu kwa vyama vya upinzani kupingana na ufisadi ulipo lakini ni muhimu wakatambua kwamba 'power corrupts', hivyo chama chochote kitachoingia madarakani baada ya CCM, lazima kiwe na mkakati wa muda mrefu juu ya hilo, vinginevyo hakitachukua miaka zaidi ya mitano kwenye madaraka. Na sioni chama chochote chenye mkakati wa muda mrefu juu ya hilo kwani IMF alternative to development imeachwa intact.
Navutiwa sana na CCK.