Nadharia ya Makadirio ya ukubwa wa changamoto ya upumuaji ukiiweka kitakwimu ili uone ukubwa wa tatizo uchukue hatua

Nadharia ya Makadirio ya ukubwa wa changamoto ya upumuaji ukiiweka kitakwimu ili uone ukubwa wa tatizo uchukue hatua

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Wakati mwingine Saikolojia inashauri kwamba!

Ili ufanikiwe kujikinga na jambo lazima ulikadirie ukubwa wake! (Assuming and assumption theory)

Mtu anaekata mti ili abaki salama ni lazima awe anafahamu vyema kukadiria madhara ya mti au tawi analokata litakavyoanguka!

Kumekuwepo na ongezeko kubwa la taarifa za misiba siku hizo!

Lakini hii haina maana hapo kabla watu walikuwa hawafi la hasha!

Ukweli ni kwamba pamoja na kwamba misiba ilikuwapo tangu zamani lakini awamu hii kelele za misiba zimeongezeka sana lakini watu hawashituki na kuchukua hatua!

Yamkini hapo zamani watu wengi waliokufa hawakutajwa kwenye media kutokana na nafasi zao za umaarufu kuwa ndogo (low profile)

Yamkini hapo mwanzo vyanzo vya vifo vilitofautiana na havikuwa na mfanano kama yanayotukia sasa!

Ni vigumu sana kupata taarifa za vifo vya changamoto ya kupumua kitakwimu za kimamlaka!

Lakini siyo kila jambo linahitaji upewe takwimu ndipo uchukue tahadhari.

Mazingira ya kupata takwimu au vipimo sahihi yanapokuwa magumu unakumbushwa usiache kutumia ASSUMPTION THEORY YA MKATA MTI

Mkata mti anapoangalia madhara yatokanayo anguko la mti huwa hahitaji kuupima urefu mti mzima kabla ya kuukata, hufanya assumption na kukata vizuri kabisa!

Hivyo kama vifo vya watu high profile vinatokea kila siku kwa changamoto ya kupumua!

Mahesabu tuyaweke hivi! (Assumption)

MTU mmoja maarufu katika kila hospital ya mkoa kwa Siku anapotajwa kufariki kwa changamoto ya kupumua basi kuna watu wengine wa kawaida+ ( 5 to 9 of low profile)

Mfano Tu assume hospital ni moja tu kila mkoa, na jumla ya mikoa iwe 31 nchi nzima. Hivyo hesabu itakuwa ifuatavyo kwa mfano!
6 × 31 = 186 death in minimum au 10×31=310 death in maximum

Hii inamaanisha kama maiti hizo zote zitakuwa na vimelea vya ugonjwa wa kuambukiza maanayake uwezekano wa kila jokofu walimohifadhiwa maiti hao linaweza kuhifadhi miili mingine hivyo kuongeza madhara kwa ndugu wengine watakaozikaa miili hata ile ya magonjwa ya kawaida.

Kwa mfano huu, unaweza ukahisi ukubwa wa tatizo lilivyokuwa kubwa na kuchukua tahadhari!

Chukulia mfano ingekuwa ni chombo cha usafili kinauwa watu 186 hadi 310 kwa siku kila siku au hata kila wiki!
Ungechukua tahadhari gani!

Tusisubiri kupewa takwimu tujipime wenyewe na kuchukua tahadhari!

Msiwasikilize wachungaji wanafiki wanaoipuuza sayansi!

Hata maandiko matakatifu yanasema wazi kwamba, Ijapokuwa Mkiomba na kufunga lakini msiache kutumia siraha na njia zote za kumwangamiza yule muovu!

Kama siraha ni sanitaiza tumia, kama ni kunawa mikono nawa, kama ni barakoa vaa, tumia kila aina ya siraha ukikumbuka assumption theory ya watu 186 hadi 310 wanaokata moto kwa changamoto ya upumuaji kila siku!
 
Sasa hivi hata wanaomeza ARV wakikata moto utasikia wamekufa kutokana na nimonia.

Watu wanapindisha ukweli kwa manufaa yao.

So far, kwa nchi yenye watu milioni 60, hata ukiwa na death rate ya 2%, ina maana kwa mwaka 'wanatakiwa' wafe watu 1,200,000 kwa sababu mbali mbali. Hii ina maana kwa mwezi 'wanatakiwa' wafe watu 100,000.

Sasa wewe umeona tangazo wamekufa watu ishirini unaanza kupaniki na wakati kabla hata ya huu ugonjwa watu waliokuwa wanakufa ni wengi tu.. Hizi media zisikupanikishe. Pia kuwa maarufu sio kinga ya kuepuka kufa.. Watu lazima wafe ili wengine wazaliwe.

Cha muhimu jikinge ili uwe na siku nyingi katika nchi upewayo na Bwana Mungu wako, ila kaa ukijua, hakuna mwenye mbio kukishinda kifo.. Siku ikifika, hakuna anayeweza kukikwepa!
 
Yule atakayeshindwa kufanya chochote ili kujikinga mwenyewe inabidi awe anatizama tu au abaki kushangaa tu kama mimi.
 
Back
Top Bottom