Nadharia ya miaka 1,000 duniani ni sawa na siku moja mbinguni si sahihi kabisa

Ngoja na mimi nijaribu kuwaza kwa sauti na kuchangia;

Nadhani hiyo phrase na context zilipotumika zinazidi kuelezea na kuthibitisha "umilele" wa Mungu
Kwanza kwenye zaburi, mtunga zaburi anaomba na ku-acknowledge that things we see taking a long time to us as humans can be done in a very short time by God. Angalia anazungumzia perishing in the para. Hii ya kusema miaka elfu ni sawa na siku moja mimi nadhani mwandishi amewaza 1000 years (millenium) kuwa kipindi kikubwa cha kulinganisha na siku moja. So unaweza kujua kwa mfano kwenye zaburi hiyo hiyo anapoendelea kuzungumzia 70 to 80 years ya uhai wa binadamu ingekuwa ni miaka mingapi. Meaning to God what we think as long time is a very short moment and what we think can be done in long term (1000 years in this case) can be done in almost instant moment by God

Kwenye kitabu cha Peter, mwandishi anajaribu kuwakumbusha na kutukumbusha sisi sote kutoishi kwenye dhambi kwa vile eti Bwana aliahidi angerudi then watu wanaona amekawia so waka-assume hatarudi.
He is bringing in this concept of time to remimd them kwamba wasiweke ukomo kwa lini Bwana atarudi au wasiache kuenenda kwenye njia sahihi just because time has passed and the Lord has not come back.

Hizi phrase actually zinatuambia tusiweke ukomo kwenye existence na acting ya Mungu kwa sababu God is eternal and we should not think kwamba the action is time barred. To us ni miaka 1000 lakini kwa Mungu ni kama one day (kwamba we think wa have waited for so long, but hii inatuambia tuwe wavumilivu kwani what we think as 1000 years (too long), Mungu anaitazama kama siku moja ( very short period)
 
Siri za uumbaji wa hii dunia hakuna mwanadamu anazijua, manabii walitoa chache na nyingi ni ngumu kuzielewa.

Kwa mfano hakuna mwanadamu ajuaye dunia hii imekuwepo kwa miaka mingapi tangu uumbaji...

Shetani alipotupwa duniani alitoa baadbi ya siri Hasa wanazotumia watu kwenda kuzimu; namna ya kutenganisha mwili na nafsi nk

Yesu kristo alitoa mafundisho tu lakini hakusema kule mbinguni nini kilifanyika kabla ya uumbaji na baada ya uumbaji, mamlaka yaliyokuwepo nk.. Kulikuwa na limitation kwake kwa sababu naye alizaliwa kama binadamu wa kawaida ili kupitia kwake tuamini.
 
Kwa uelewa wangu"Miaka 1000 = 1day" ni lugha ya picha ambayo ina tafsiri yake so hutakiwi kuichukulia kama ilivo. Vitabu vyetu vya Imani vimetumia lugha ya moja kwa moja(direct) na ya picha/ mafumbo (indirect).

UELEWA WANGU KATIKA HILI.
Ni kwamba vitu ambavyo vinaweza kufanyika kwa miaka 1000 hapa duniani kwa Mungu huweza kufanyika siku moja tu/. Mambo ambayo binadamu tunayaona ni magumu kwa Mungu ni rahisi sana.
 
Basi na iwe tu hiyo hiyo miaka 1,000. Maana tumejikuta tupo tu na hatuna uwezo wa kuipunguza. Vyovyote tutapokea.
 
Ili tuhesabu siku ni lazima vitu viwili vitokee
1.Mchana kuuvua usiku
2. Usiku kuuvua mchana
Kama vitu hivi kwa Mungu huko alipo hakuna basi , utakuwa umesema kweli
 
Kwa uelewa mdogo tu, siku huhesabiwa kwa kuzama kwa jua na kutokeza, this results due to earth rotation. Sasa je, huko kwa Mungu kuna dunia inazunguka jua?

Hii nadharia ya Mungu inachanganya sana!
Kwani wakati wa uumbaji si Mungu alikuwa akiumba huku akiwa huko huko mbinguni na biblia ikihesabu siku kwa kusema "ikawa jioni, ikawa asubuhi", siku ya pili, ya tatu hadi ya saba? Sasa kudai kwamba miaka elfu moja ya duniani ni sawa na siku moja ya mbinguni si itapelekea madai mengine kwamba uumbaji uliofanyika kwa siku saba za mbinguni zinamaanisha ilitumika miaka 7,000 ya duniani kukamilisha uumbaji?

Na hivyo siku ya kupumzika (sabato ya bwana?) inatakiwa iwe kila inapotimia miaka 7,000?
 
hujaelewa hapo

Iko hv..hebu fikiri
1:mfano mzuri ujenzi wa nyumba hata uwe na matirio yote kwa binadamu huwezi kujenga kwa siku moja nakuhamia siku hiyo hiyo..utatumia muda hata wiki mwezi kama sio miezi.je utatumia miaka mingapi kujenga nyumba za mfano mtaa mmoja tu,àu bara moja tu,au sayari moja tu?

Kisima cha maji pamoja na mitambo yote utachimba wiki au siku kadhaa je.je utatumia muda gani kuchimba,au kutengeneza au kuyafanya maziwa,bahari au mabwawa yaliyopo duniani leo hii.??

Lazima tutatumia miaka na miaka
Lakini kwake hiyo kazi ikikuwa ni simpo tu aliyoifanya kwa kwa siku saba tu. Kama vile wewe unavyoweza kuchakachua kura za jimbo lenu lote na kumtangaza mbunge uliyempanga kuwa ni mshindi ndani ya siku 7 tu.

"Muhudumu naomba Kvant nyingine"
 
 
Nikubaliane na mleta post kwa hoja yake ya Mungu kutokuwa na kipindi cha wakati yaani yeye ni wa eternally hana mwanzo wala mwisho. Nino hili la kiswahilili "milele" linapotumika ndani ya maandiko matakatifu limeonyesha kuwa ni kupindi cha wakati maalumu. Kama utaielewa lugha ya biblia mwanzo ambao ni ilipoanzia nyakati ni baada ya anguko la Adamu. Kabla ya hapo kulikua na umilele. Sasa baada ya anguko kukawa na kupungukiwa na utukufu wa Mungu kwa mamkind. Huu upungufu umetuwekea veil . Kiasi kwamba mapana ya ulimwengu wa roho ulio mbali sana na huu wa mwili umepotea kwa mamkind unless otherwise.

Kwa watu waliojaliwa mfano wa manabii wamepewa uwezo wa kuona ambayo watu wengi wa kawaida hawaoni wala kufahamu kwayo.

Ili Mungu kuchukuana na watu wa stara(pazia) imebidi itumike lugha ya mfano. Na hasa akitolea mifano vitu vinavyofahamika katika mazingira yetu wanadamu. Kwa suala la hii miaka imetumiwa lugha ya 'kama' sii halisi. "Mwaka mmoja ni kama miaka elfu".

No wonder Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake hasa wale tenashara "Kama ikiwa naongea na ninyi yaliyo ya kidunia hamuelewi itakuwa vipi nikiwazungumzia ya mbinguni?"
Hata hivyo sii kwamba mtabaki vipofu kwa ya uhaibuni bali "Yafaa mimi niondoke ili yule msaidizi niliyewaambia habari yake kutoka kwa Baba aje naye ni Roho mtakatifu"
Ndio kusema kuna kuachana mbali kati ya hekima ya kibinadamu na hekima ya Mungu.
 
Ngoja kwanza

Kwa nini sasa sir God anataka tufe

Hafu pia kwani kati yetu sisi na malaika nani ni bora kwake ?

Kwa nn na sisi asingetufanya kama malaika ?!
 
Mambo Ya Rohoni Kuyafasiri Kwa Jinsi Ya Mwilini Ni Ukengeufu Na Uposhaji Wa Maandiko. Mambo Ya Rohoni Yanajulikana Kwa Jinsi Ya Rohoni Tu. Biblia Haisomwi Kama Gazeti Au Kitabu Cha Historia.
 
Ngoja kwanza

Kwa nini sasa sir God anataka tufe

Hafu pia kwani kati yetu sisi na malaika nani ni bora kwake ?

Kwa nn na sisi asingetufanya kama malaika ?!
Mkuu umeuliza kwa nini sir god anataka tufe...

Sijajua umeuliza kwa mujibu wa kitabu gani mkuu bibilia ama Qurani..mana naweza kukujibu kwa mujibu wa Quran hilo swali kumbe wewe umeuliza kwa mujibu wa bibilia..



Mimi naomba nikujibu kwa mujibu wa Qurani vipi mkuu uko tayari ?
 
Dah hii KVANT yako ya Leo Si mchezo, Post moja inarudiwa mara 4, Hongera kwa kupata KVant
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…