Slowly
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 10,589
- 35,268
View attachment 1125684
Salute..
kuna msemo sijui tulifundishwa au tulisoma wenyewe kwenye vitabu vyetu vya dini (Bibble & Qu'ran) msemo huo unasema kua Miaka elfu moja duniani ni sawa na siku moja mbingu, kiukweli kwa uelewa wangu mdogo wa maswala ya Theologia na Physics nasema huu msemo ni uongo ina wezekana waliotufundisha au tulipousoma kwenye vitabu tuliutafsiri tofauti.
Kwanza kama ulisoma uziwangu wa Time Travel kiasi wadau waliweza kuelezea kadri wajuavyo effect ya Time kwenye Maisha/Uhai wa mwanadamu, nilivutiwa zaidi na mchngowa mkuu BASANORARE kwenye comment hii https://www.jamiiforums.com/threads...-kuwa-suluhisho-la-kifo.1585916/post-31526494 sikutaka nimjibu pale nikaona nianzishie mada hii kitu labda kila mtu atoa mawazo yake juu huu msemo/Andiko.
.......
Ref kutoka Qu'ran: Surat Hajj 47, allah anasema kuwa siku moja ya Allah ni sawa na miaka elfu moja "1,000".
Ref from Bible: Zaburi 90:4 Kwako miaka elfu moja ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha kupita, kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku
2Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja
Haya ndio maandiko ambayo yamefanya kuenea kwa msemo ambao mimi kwa muono wangu naona si kweli kwa jinsi watu wanavyo
yatafsiri, mimii naelewa hivi kuhusu haya maandiko and I hope theseare aint Blasphemy kwani the Almighty hapendi wasiotaka kuhoji...Let's go!
Kwanza kabisa Kiasili Mungu ana sifa kuu ambazo ni Omniscience (Ajuaye yote), Omnipotence (Mwenye uweza na nguvu zote) na Omnipresence (aliyoko kila mahalii).
tunaposema kua kwa Mungu/Mbinguni siku moja sawa na miaka 1000 ya duniani msemo huu unauvunja vipande vipande ile sifa ya Mungu ya kua Ana uwezo wa kila kitu na Hana mwanzo wala mwisho.... Kivipi???????????
duniani sababu kuu ambayo inatufanya twafariki ni kwasababu i)Dhambi ya asili (ii)ili kuweza kubalnce nature na kuruhusu existence ya viumbe vingine duniani (iii)time. Yes tunakufa kwakua kuna muda duniani ambao unatuhesabia siku zetu tunazoishi hapa dunia ..Time is the biggest threat to mankind ndio maana nilisema kwenye mada yangu ya time Travelling kua tukiweza kudhibiti muda basi tunaweza kudhibiti KIFO. Kwa mantiki hiyo nachelea kusema kwamba kama kwa Mungu kuna Muda basi Mungu ana mwanzoo, Mbinguni kuna vifo there is no eternal life at all, Yawezekana basi hakuna Mungu mmoja maana watakua wanapita/wanafariki (God Forgive I feel like I'm going too far).
Kwa mujibu Fundamental physical quantity, the SI-Unit of Time is Second and other si-unit are year,day,month,decade,millisecond,century etc...Hivyo basi kama mbinguni Muda basi Mungu atakua ana muda maalumu aliotokea(ana mwanzo) maana ili muda uweze kuhesabiwa lazima kuwe na jua linalo zunguka, haingii akilini kwamba kila ikifika miaka elfu ya duniani basi Mungu hua analala kwakua jua limezama usiku umeingia haiwezekani.
Ninavyofahamu Mimi kwa Mungu hakuna muda (Timeless) hakuna future wala past kila muda kwake ni present, Mungu hawzi eti kesho nitafanya hivi na hivi big Nope ndio maana malaika hawazeeki wala hawafi maana hakuna Muda waliowekewa unaohesabu miaka yaoo labda technically aliyewaumba anajua umri wao. Sie wandamu tumewekewa muda ili tuweze kupanga malengo yetu, ili tuweze kuishi umri fulani tulipangiwa na Muunmba,,ili siku moja tufe that's all..
Kwa hiyo basi kwa kusema hivo yawezekana msemo huu inawezekana kutokna na ambiguity ya kiswahili chetu wakati unatafsriwa kutaka version ya lugha zingine sie tuliuelewa vibaya. au kwa vyovyote vile ulipokelewa kimakosa kama vitabu vinne vya wakorintho ilivyokua..
Mwisho kabisa niseme kua huu ni muono wangu na sio pie kwamba kila mtu alzima aelewe hivyo..Lakini naamini kwa Mungu ni Timeless
Anybody Concur with me......???????????
~Da'Vinci
Mkuu salute sana tuuu....
Biblia imeweka wazi kila kitu ambacho mwanadamu anakihtaj kwa ajli ya usalama wake...kama kuna maswali unajiuliza na umefanya kila jitihada lakn umekosa jibu..basi jua kabisa hilo jambo halina umuhimu wwte kwako na hata ukilijua halitakusaidia ndo mana Mwenyezi Mungu hajalitolea ufafanuzi...mbali na hayo kuna mambo mengi sana ambayo hayajulikani kwa wanadamu walio wengi...lakn sababu siyo kwamba Mungu ameyaficha ila tatizo ni uzembe wetu wa kutosoma Biblia....
Wakristo wengi wamekuwa wakihubir kuwa mwisho wa dunia umekarbia bila kujua dhana hyo inatumika katika mazingira gani..
Matokeo yake wengi wameishia kukata tamaa na kuamua kuishi maisha ya dhambi wakiamini kuwa Mungu ameiacha dunia ijiendeshe yenyewe....Ukweli ni kwamba bado takriban miaka 1000 dunia ifike mwisho wake...ufuatao ni ushahidi wa kibiblia fuatana nami....
Namba saba katika Biblia
Biblia hutumia namba saba kama namba kamilifu kwa jambo fulani...mfano Mungu aliumba dunia kwa siku sita siku ya saba akapumzika Mwanzo 2:2..
Mungu pia anasema tufanye kazi kwa siku sita na siku ya saba ni ya kupumzika..Kutoka 23:12
Mifano mingine ni kama ifuatayo
Kutoka 21:2 Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miakasita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.
Kutoka 23:10-11
Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; lakini mwaka wa saba utaiacha nchi itulie na kupumzika..
Joshua 2:2-5 ...fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbetasaba
za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba
mtauzunguka mji mara saba.
Hata ukisoma habari za naamani, safari ya saba kujichovya katika maji, ndipo akatakasika ukoma wake.
Eliya pia aliomba mara saba ili mvua inyeshe....1Wafalme 19
Kikawaida Mungu alimaanisha siku yenye mzunguko wa masaa 24 ambayo wanadamu huwa tunaitumia...Mwenyezi Mungu alidokeza pia kuwa kwake siku moja ni sawa na miaka elfu moja ya kibinadamu.. (hapa ndo kwenye kiini cha hoja hii) scenario ya namna hii huwez kuitumia popote ispokuwa kwenye unabii tena unabii mrefu sana...Kwa wataalamu wa Hesabu wanajua kuna wakati unapokokotoa swali la logarithms itakubidi kutumia concept ya exponent kupata jibu lililo sahihi..hvyo bas itatubid tutumie concept ya siku saba kama utimilifu wa jambo na badala ya kutumi siku kama siku tutumie siku=miaka 1000
ushahidi wa kibiblia unaonyesha kuwa tangu dunia kuumbwa ni takriban miaka elfu sita mpak sasa...kama mwaka mmoja ni sawa na miaka 1000 hii ina maana kuwa kwa mtazamo wa Mungu sasa ni siku ya sita na hii siku haijaisha ndo kwanza tumeianza (6017)...ili kufikia miaka 7000 bado miaka takriban 983 karbia 1000 ...so we have almost 1000 years to go and finish the game....
Yesu alibainisha kuwa kuelekea kufikia miaka elfu saba..watumishi wa kweli wa Mungu watapitia wakati mgumu sana ambao hakuna mtumishi yeyote aliyewahi kupitia tangu Dunia iumbwe na hvyo itamlazimu kufupisha siku hzo ili kuokoa wateule wachache watakaokuwa wapo hai (Mathayo 24:22..) hvyo miaka takriban elf iliyobaki inaweza ikapungua, hata hvyo bado ni miaka mamia kufikia huo mwisho....
Kuzaliwa kwa Yesu kulitokea lini
Adamu alipewa ahadi ya kuja kwa Yesu mara ya kwanza kama masihi..hata hvyo alikufa bila ahadi hyo kutimizwa...ahadi ilizidi kutolewa kwa watumishi wengine na waliitarajia kutokea kwa haraka hata hvyo Ibrahimu, Yakobo, Musa, Daudi na hata Danieli wote walikufa bila kuona Ahadi hiyo ikitimizwa...Yesu alitarajiwa kuokoa kizazi chote cha wanadamu tangu Adamu mpak pale mwisho wa dunia utakapofika..Yesu alizaliwa mwaka 4000 tangu dunia kuumbwa hii inaonesha kuwa alizaliwa katkat ya miaka 7000 japo ilizidi miaka 500 hii ilichangiwa na ugumu wa Wayahudi....Pia alizaliwa katikati ya dunia yote (Middle East is the center of the earth)...tokea Yesu azaliwe ni miaka 2017 sasa...ukijumlisha na ile miaka 4000 tangu dunia iumbwe tunapata miaka 6017...ili tufikie siku ya saba au miaka elfu saba tunahtaji miaka mingine karbia elf moja...hvyo bas bado miaka mamia kadhaa kuufikia ule mwisho....
Wanaosema Mwisho wa dunia umefika/umekarbia wapo sahihi?
Naweza nikakubali kuwa mwisho wa dunia umekarbia..hata hivyo jambo hili lipo kiroho zaidi...kwa Mungu ni bado masaa tu kufikia mwisho ila kwetu sisi hayo masaa kadhaa ni miaka mamia kadhaa ambayo kiuhalisia tuliopo hai sa hvi tutakutwa wote tumekufa...
Yesu aliwaambia wanafunzi naja upesi...hata walipokuw awanakufa waliamin kabisa kuwa atarud baada ya miaka michache tu lakn mpak sasa ni miaka 2000 imepita na bado dunia inasonga...
Swala la kifo ndo jambo la kuangalia zaidi kwa sasa kuliko mwisho wenyewe kwa sababu ukifa leo ni millsecond tu itakuchukua kuufikia ule mwisho wenyewe...haijalishi miaka mamia mangap itakuwa imepita tangu ufariki lakni kwako itakuwa ni sekunde tu au millsecond...Yesu aligusia hili akasema, Suala la kifo kwa wengi litafanya tukio la kuja kwa Yesu mara ya pili liwe la kushtukiza kama mwizi japo hata wale wataokutwa wapo hai wengi wao watastukizwa kam mwizi....(Hvyo usibweteke kuwa Yesu bado sana kurudi kwani kifo ambacho hakijulikan kitakuja lin ndo kizingiti kikubwa kwa sasa)
Baada ya siku sita au miaka 6999 or less than nin kitatokea ?
Baada ya siku sita siku ya saba watakatifu watapumzika na Mungu juu mbiguni kwa mda wa siku nzima ile siku ya saba ambayo ni sawa na miaka 1000. Biblia inaiita millenia mpya...
Je ni kweli hatujui siku wala saa ya kurudi mwana wa adamu au Yesu ?
Yesu alisema hakuna mtu ajuaye siku wala saa ya kuja mwana wa Adamu...hata hvyo dalili za kuja kwake ameziweka wazi..ni jambo la kuchunguza tu maana hata yeye mwenyewe alisema "Asomaye na Afahamu (Mathayo 24:15)"
Katika kumi bora ya watu maarufu wa mda wote waliowahi kuishi hapa duniani..wa nne kati yao wametoka ndani ya Biblia..huku Yesu akiwa ndo Mwanadamu maarufu zaidi kupita wote...