Nadharia ya miaka 1,000 duniani ni sawa na siku moja mbinguni si sahihi kabisa

Nadharia ya miaka 1,000 duniani ni sawa na siku moja mbinguni si sahihi kabisa

View attachment 1125684
Salute..
kuna msemo sijui tulifundishwa au tulisoma wenyewe kwenye vitabu vyetu vya dini (Bibble & Qu'ran) msemo huo unasema kua Miaka elfu moja duniani ni sawa na siku moja mbingu, kiukweli kwa uelewa wangu mdogo wa maswala ya Theologia na Physics nasema huu msemo ni uongo ina wezekana waliotufundisha au tulipousoma kwenye vitabu tuliutafsiri tofauti.
Kwanza kama ulisoma uziwangu wa Time Travel kiasi wadau waliweza kuelezea kadri wajuavyo effect ya Time kwenye Maisha/Uhai wa mwanadamu, nilivutiwa zaidi na mchngowa mkuu BASANORARE kwenye comment hii https://www.jamiiforums.com/threads...-kuwa-suluhisho-la-kifo.1585916/post-31526494 sikutaka nimjibu pale nikaona nianzishie mada hii kitu labda kila mtu atoa mawazo yake juu huu msemo/Andiko.
.......
Ref kutoka Qu'ran: Surat Hajj 47, allah anasema kuwa siku moja ya Allah ni sawa na miaka elfu moja "1,000".
Ref from Bible: Zaburi 90:4 Kwako miaka elfu moja ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha kupita, kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku
2Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja
Haya ndio maandiko ambayo yamefanya kuenea kwa msemo ambao mimi kwa muono wangu naona si kweli kwa jinsi watu wanavyo
yatafsiri, mimii naelewa hivi kuhusu haya maandiko and I hope theseare aint Blasphemy kwani the Almighty hapendi wasiotaka kuhoji...Let's go!

Kwanza kabisa Kiasili Mungu ana sifa kuu ambazo ni Omniscience (Ajuaye yote), Omnipotence (Mwenye uweza na nguvu zote) na Omnipresence (aliyoko kila mahalii).
tunaposema kua kwa Mungu/Mbinguni siku moja sawa na miaka 1000 ya duniani msemo huu unauvunja vipande vipande ile sifa ya Mungu ya kua Ana uwezo wa kila kitu na Hana mwanzo wala mwisho.... Kivipi???????????
duniani sababu kuu ambayo inatufanya twafariki ni kwasababu i)Dhambi ya asili (ii)ili kuweza kubalnce nature na kuruhusu existence ya viumbe vingine duniani (iii)time. Yes tunakufa kwakua kuna muda duniani ambao unatuhesabia siku zetu tunazoishi hapa dunia ..Time is the biggest threat to mankind ndio maana nilisema kwenye mada yangu ya time Travelling kua tukiweza kudhibiti muda basi tunaweza kudhibiti KIFO. Kwa mantiki hiyo nachelea kusema kwamba kama kwa Mungu kuna Muda basi Mungu ana mwanzoo, Mbinguni kuna vifo there is no eternal life at all, Yawezekana basi hakuna Mungu mmoja maana watakua wanapita/wanafariki (God Forgive I feel like I'm going too far).
Kwa mujibu Fundamental physical quantity, the SI-Unit of Time is Second and other si-unit are year,day,month,decade,millisecond,century etc...Hivyo basi kama mbinguni Muda basi Mungu atakua ana muda maalumu aliotokea(ana mwanzo) maana ili muda uweze kuhesabiwa lazima kuwe na jua linalo zunguka, haingii akilini kwamba kila ikifika miaka elfu ya duniani basi Mungu hua analala kwakua jua limezama usiku umeingia haiwezekani.

Ninavyofahamu Mimi kwa Mungu hakuna muda (Timeless) hakuna future wala past kila muda kwake ni present, Mungu hawzi eti kesho nitafanya hivi na hivi big Nope ndio maana malaika hawazeeki wala hawafi maana hakuna Muda waliowekewa unaohesabu miaka yaoo labda technically aliyewaumba anajua umri wao. Sie wandamu tumewekewa muda ili tuweze kupanga malengo yetu, ili tuweze kuishi umri fulani tulipangiwa na Muunmba,,ili siku moja tufe that's all..
Kwa hiyo basi kwa kusema hivo yawezekana msemo huu inawezekana kutokna na ambiguity ya kiswahili chetu wakati unatafsriwa kutaka version ya lugha zingine sie tuliuelewa vibaya. au kwa vyovyote vile ulipokelewa kimakosa kama vitabu vinne vya wakorintho ilivyokua..

Mwisho kabisa niseme kua huu ni muono wangu na sio pie kwamba kila mtu alzima aelewe hivyo..Lakini naamini kwa Mungu ni Timeless
Anybody Concur with me......???????????
~Da'Vinci

Nafikiri umerukia mbali sana ungetuliza akili yako ukaanzia ktk maneno ya Mungu yaliomo ktk vitabu vya dini anaposema ameumba Dunia na vyote vilivyomo kwa muda wa siku sita, ukituliza akili hapo utapata jibu la siku moja kwa Mungu ni miaka 1000 ya duniani
 
So aliumba dunia kwa siku sita za duniani au siku sita za mbinguni ambapo ni sawa na miaka 6000 ?
 
ASANTE KWA HOJA YAKO NA MAONI YAKO MAZURI..

NAOMBA NIKCRASH POINT YAKO KWenye VIPANDE ELFU..
1.hata neno moja halitatanguka kwenye biblia ..dunia itapita lakin kwenye bible hata nukta haita pita...

2. ww umechanganya kipo cha muda na wakati...kwa maana ukisema kesho wewe unaelewa kwamba masaa 24 yajayo... lakin kiuhalisia icho ni kipimo cha muda ..hukuna kesho..kesho ni imagination yako... PIA KUMBUKA VIPIMO VYA MUDA NI VYA MWANADAMU KWA MUNGU KUNA UWEPO MWINGINE KABISAA NJE YA LOGIC YA BINADAMU YEYOTE .....

3. mfano mzur kuna mduduanaitwa tsetsefly kama sijakosea yeye anaishi maisha yake yote ndani ya maa 14 yaan anazaliwa anakua anazaa ndani ya huo mda ambao wewe unasema ni siku moja... kwaiyo siku moja kwao ni sawa na siku 24 kwake...
4. MUNGU SIFA YAKE NI KUWA YEYE NDIO MWANZO PIA YEYE NDIO MWSIHO... KILA KITOKEACHO KINATOKEA IN BETWEEN..

..KWAIYO SWALA LA SIKU MOJA MBAYO WEWE SISI TUNASEMA KUZAMA KWA JUA NA KUCHOMAZA ..NA SIO SAA ILIYOKIGANYANI MWAKO WALA ILIYO YA ATOMIC NI KWELI KABISA KWA MAAANA UFAHAMU A MWANADAMU HAUWEZ KUCHAMBUA YALIYO KATIKA HEAVEN KINGDOM...

AMEN
Bado sijakupata wamaanisha nini hasa
 
Bado sijakupata wamaanisha nini hasa
KWAIYO SWALA LA SIKU MOJA NI SAWA NA MIAKA ELFU NI SAWA.....SIKU MOJA MBAYO WEWE SISI TUNASEMA KUZAMA KWA JUA NA KUCHOMAZA ..NA SIO MAJIRA YA SAA ILIYOKIGANYANI MWAKO WALA ILIYO YA ATOMIC NI KWELI KABISA KWA MAAANA UFAHAMU A MWANADAMU HAUWEZ KUCHAMBUA YALIYO KATIKA HEAVEN KINGDOM..

.....

NIKURAHISISHIE UKIWA DUNIAN ..SIKU MOJA NDIO MAANA YAKE NINI????
 
Anaposema Mungu amefanya jambo fulani kwa muda fulani, hiyo ni kwa hesabu zake yeye za Mbunguni sio za duniani
Anaposema hivo basi ni kwa hesabu za duniani ili msichangnyikiwe, kwake hakuna muda
 
Anaposema hivo basi ni kwa hesabu za duniani ili msichangnyikiwe, kwake hakuna muda

Tumia akili kidogo unaposema kwa Mungu hakuna Muda unamaanisha nini, kama ingekuwa hakuna muda ameuazishaje muda ? wewe umefahamu kitu muda kutoka wapi? (I mean initially)
 
Tumia akili kidogo unaposema kwa Mungu hakuna Muda unamaanisha nini, kama ingekuwa hakuna muda ameuazishaje muda ? wewe umefahamu kitu muda kutoka wapi? (I mean initially)
heheee fact yako nyepesi mno.. kwahiyo unataka kusema Mungu hawezi anzisha kitu ambacho mbinguni hakipo, so tunakufa kwakua mbinguni kuna vifo, mbinguni kuna jua na mwezi right?
 
heheee fact yako nyepesi mno.. kwahiyo unataka kusema Mungu hawezi anzisha kitu ambacho mbinguni hakipo, so tunakufa kwakua mbinguni kuna vifo, mbinguni kuna jua na mwezi right?

Nafikir unapata tabu hujuwi maana ya muda na akili yako imeganda ktk usiku na mchana ndio muda, na huelewi hata hapa duniani kunasehemu kama za north pole wapo watu hawajui usiku nini, sasa utsema aje hawana muda,?

Halafu neno kufa pia hujui maana yake, hata viumbe wa mbuguni siku yao ikifika watakufa, kila nafsi itaonja umauti, nafsi zilizopo mbinguni na aridhini, sijui kama ulikuwa unalielewa hilo.
 
Mmmmh.
Hapa umenivuruga completely mkuu.
Kwa kusema hata vya mbinguni vitakufa.
 
Papaayenga haya nafikiri unamwandikia mkuu Da vinc. Mimi siye mwenye mada bali ni mchangiaji tu.

Kilichonichanganye kwenye post tangu ni mchangiaji mmoja tena mtu anaeonekana wa ufahamu wa juu sana katika masuala ya kiroho kudai kuwa kwa andiko la kila nafsi itaonja mauti linajumuisha na hata nafsi za walioko mbinguni kwamba nao watakufa.

Hapa ndipo nilipochanganyikiwa maana kwa uelewa wangu nilidhani kwamba kuna viumbe wa kimbingu ambao they are not subjected to death. Mfano malaika wateule, wenye uhai wanne nk.

Nafahamu kuwa hawa hawajawahi kuanguka wala kuwa na miili ya kifo (flesh)'
Kama vipi mkuu hebu toa uelewa wako katika hili.
 
Papaayenga haya nafikiri unamwandikia mkuu Da vinc.
Mimi siye mwenye mada bali ni mchangiaji tu.
Kilichonichanganye kwenye post tangu ni mchangiaji mmoja tena mtu anaeonekana wa ufahamu wa juu sana katika masuala ya kiroho kudai kuwa kwa andiko la kila nafsi itaonja mauti linajumuisha na hata nafsi za walioko mbinguni kwamba nao watakufa.
Hapa ndipo nilipochanganyikiwa maana kwa uelewa wangu nilidhani kwamba kuna viumbe wa kimbingu ambao they are not subjected to death. Mfano malaika wateule, wenye uhai wanne nk.
Nafahamu kuwa hawa hawajawahi kuanguka wala kuwa na miili ya kifo (flesh)'
Kama vipi mkuu hebu toa uelewa wako katika hili.
Oooh kumbe ni wewe papaayenga ulietoa hili wazo. Sasa sijajua ni kwa mujibu wa Quran au bible.
 
Hiyo ndio kanuni kila kilocho hai lazime kife, we hukusoma shule kanuni hii
Ninachofahamu ni kwamba kuna viumbe vilivyo chini ya sheria(kanuni) hasa vya kimwili ndio hufa lakini kuna vingine viko juu ya kanuni za maumbile hasa vya kiroho hivi havifi.
Biblia haijasema kuwa kila nafsi itakufa bali kwamba nafsi itendayo dhambi ndio itakayokufa.
 
Humo hamna kanuni ya maumbile, utapata tabu sana kuelewa unaposema Roho unaelewa maana yake? Roho nini ? Na nini kinachokufa kati ya roho na mwili, neno Roho limetokana na lugha ipi? Je roho inaweza ku exist bila mwili?
Nipe tofauti kati ya Nafsi na Roho
 
Roho ni nguvu ya uhai ya kila kiumbe hai kwa maana kwamba kila kiumbe hai kina roho ya uhai ila sii viumbe wote hai wenye nafsi. Nafsi ni utu.

Kuhusu miili ni kwamba kila kiumbe kina mwili iwe ni cha kimwili ama ni cha kiroho na miili hii inatofautiana kifahari kulingana na status yake
 
Post ya 100 hii katika uzi huu.

Bado nakubaliana na dhana ya Biblia na Qur'an.

Nikipata muda nitaelezea kwa nini huku nikijikita kwenye hoja hizo.
 
Back
Top Bottom