poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 453
- 175
Habari wadau,
Kuna nyumba imeachwa na marehemu baba yetu, mimi na ndugu yangu tupo wawili tu. Yeye amenizidi umri kama miaka 20. Nyumba hiyo amedai ni ya kwake na wala si ya baba yetu kama ilivyokuwa ikifahamika na kutamkwa na marehemu mzee wetu.
Nimejaribu kumwambia ukweli wa kauli ya mzee wetu anadai si kweli nyumba ni ya kwake. Tumefanya vikao kadhaa ameonesha ushahidi wa yeye ndiye mmili halali wa nyumba hiyo.
Ushahidi alioutoa ni leseni ya makazi (sio hati) iliyotolewa mwaka 2012 yenye jina lake. Swali aliloulizwa baada ya kutoa leseni hiyo ya makazi, je ana ushahidi wa umiliki wa nyumba hiyo kabla ya kupata leseni ya makazi mwaka 2012. Alitoa karatasi ya mauziano ya nyumba hiyo ya mmiliki wa awali
kabla ya kuimiliki yeye.
Lakini ushahidi huo alioutoa umegundulika si wakweli. Imebainika mauziano hayo yanaonesha ni nyumba ya eneo lingine na sio hiyo inayokusudiwa. Kumbuka nyumba ni ya miaka tangu 1970s na ipo maeneo ambayo hayajapimwa.
Ukweli ni kuwa nyumba hiyo ilinunuliwa na Marehemu baba yetu na kwa kuwa huyo mwenzangu ni mkubwa aliwahi kuchukua documents zinazohusu nyumba wakati mzee anaumwa. Mzee wetu amefariki miaka sita iliyopita.
Kwa kweli nimekwama nahitaji msaada wenu nifanyeje ili niweze kupata haki ambayo nadhulumiwa.
Asanteni sana.