Nadhulumiwa nyumba msaada wenu tafadhali

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
453
Reaction score
175
Habari wadau,

Kuna nyumba imeachwa na marehemu baba yetu, mimi na ndugu yangu tupo wawili tu. Yeye amenizidi umri kama miaka 20. Nyumba hiyo amedai ni ya kwake na wala si ya baba yetu kama ilivyokuwa ikifahamika na kutamkwa na marehemu mzee wetu.

Nimejaribu kumwambia ukweli wa kauli ya mzee wetu anadai si kweli nyumba ni ya kwake. Tumefanya vikao kadhaa ameonesha ushahidi wa yeye ndiye mmili halali wa nyumba hiyo.

Ushahidi alioutoa ni leseni ya makazi (sio hati) iliyotolewa mwaka 2012 yenye jina lake. Swali aliloulizwa baada ya kutoa leseni hiyo ya makazi, je ana ushahidi wa umiliki wa nyumba hiyo kabla ya kupata leseni ya makazi mwaka 2012. Alitoa karatasi ya mauziano ya nyumba hiyo ya mmiliki wa awali
kabla ya kuimiliki yeye.

Lakini ushahidi huo alioutoa umegundulika si wakweli. Imebainika mauziano hayo yanaonesha ni nyumba ya eneo lingine na sio hiyo inayokusudiwa. Kumbuka nyumba ni ya miaka tangu 1970s na ipo maeneo ambayo hayajapimwa.

Ukweli ni kuwa nyumba hiyo ilinunuliwa na Marehemu baba yetu na kwa kuwa huyo mwenzangu ni mkubwa aliwahi kuchukua documents zinazohusu nyumba wakati mzee anaumwa. Mzee wetu amefariki miaka sita iliyopita.

Kwa kweli nimekwama nahitaji msaada wenu nifanyeje ili niweze kupata haki ambayo nadhulumiwa.

Asanteni sana.
 
Mkuu achana nayo hiyo nyumba ya urithi tafuta yako,.... utaanza kuokota makopo bure shauri yako.

Mimi walinikosakosa.
 
Ila ndg yangu poposindege, Achana kabisa na mambo ya urithi kama vp pambana tu ujenge nyumba kwa jasho lako, watoto wengi wa Kitanzania wamelemaa na mali za urithi yaani kukicha wanaomba wazazi wao wafariki wagawane mali .
 
​ Ha ha ha balaa!!!!!

Mkuu wee aha tu,

Walianza kunitafuta kwenye elimu...... kipindi niko shuleni form six boarding ile nakaribia kufanya mthihani wa taifa wiki moja kabla niliugua maralia moja sijapata kuugua malaria kama ile....... nikaenda nikanywa mimetakelfini wapi, mipanadol wapi...., ikabidi niwapigie ndugu zangu mbalimbali wenye upendo na mimi waanze kuniombea huwezi kuamini ile malaria ilikuja kukata Jumapili wakati jumatatu ndo mthihani wa nakumbuka Mathematics na Gs ndo ilikuwa inaanza.... basi nikaifanya ivyoivyo kibishibishi,.... nilipomaliza Mithihani nikarudi nyumbani sasa kuna kipindi maadui zangu waligombana wao kwa wao hapo ndo nikapata siri kwmba walinirushia kitu nilipokuwa shule kwani walikua wanaumbuana wao kwa wao.....

Basi nikachukia nikaanza kudai Urithi wangu nakumbuka kabla sijaenda chuo ile naanza process tu za kudai mara nikaanza kujihisi kuchanganyikiwa,kichwa kinakuwa kama kimevurugwa vile akili zote ziliruka nilijiisi kama mnyama vile...... daah ilibidi nishit nikimbilie chuo.

Ivi nnavyokwambia tangu niingie chuo mpaka sasaivi na kumaliza nilishamaliza kule HOME sikukanyaga tena zaidi ya mara moja tu nilipokwenda kuchukua vitu vyangu vyote...!

Nyumba za urithi sio ndugu kama anauwezo Achagame ajenge yake.
:smow:

Wale malipo yao watayapata hapahapa duniani.Yaani ni Mateso mpaka kufa.
:hatari:
 
Kama kaka yako kaamua kukuzulumu, Mwachia Mungu and move forward .... Utaingia kwenye tabu! Ipo Siku Atajua amefanya dhuluma na kujirudi ila usipambane

Habari wadau,

Kuna nyumba imeachwa na marehemu baba yetu, mimi na ndugu yangu tupo wawili tu. Yeye amenizidi umri kama miaka 20. Nyumba hiyo amedai ni ya kwake na wala si ya baba yetu kama ilivyokuwa ikifahamika na kutamkwa na marehemu mzee wetu.

Nimejaribu kumwambia ukweli wa kauli ya mzee wetu anadai si kweli nyumba ni ya kwake. Tumefanya vikao kadhaa ameonesha ushahidi wa yeye ndiye mmili halali wa nyumba hiyo.

Ushahidi alioutoa ni leseni ya makazi (sio hati) iliyotolewa mwaka 2012 yenye jina lake. Swali aliloulizwa baada ya kutoa leseni hiyo ya makazi, je ana ushahidi wa umiliki wa nyumba hiyo kabla ya kupata leseni ya makazi mwaka 2012. Alitoa karatasi ya mauziano ya nyumba hiyo ya mmiliki wa awali
kabla ya kuimiliki yeye.

Lakini ushahidi huo alioutoa umegundulika si wakweli. Imebainika mauziano hayo yanaonesha ni nyumba ya eneo lingine na sio hiyo inayokusudiwa. Kumbuka nyumba ni ya miaka tangu 1970s na ipo maeneo ambayo hayajapimwa.

Ukweli ni kuwa nyumba hiyo ilinunuliwa na Marehemu baba yetu na kwa kuwa huyo mwenzangu ni mkubwa aliwahi kuchukua documents zinazohusu nyumba wakati mzee anaumwa. Mzee wetu amefariki miaka sita iliyopita.

Kwa kweli nimekwama nahitaji msaada wenu nifanyeje ili niweze kupata haki ambayo nadhulumiwa.

Asanteni sana.
 
Huwa sijisikii happy kwa vitu vya urithi napamba nipate changu and will be proud of having my own assets
 
Pole sana ndugu poposindege naona watu waliopona kufanyiwa juju wamekutisha sana hadi umetokomea..

Unaweza kupata haki yako. Baada y mazazi wenu kufariki mlikaa kikao cha familia na kufungua jalada mahakamani kuteua msimamizi wa mirathi? Kama sio huyo ndugu yako anapata wapi haki ya kujigawia nyumba!

Umesema baba yenu amefariki miaka sita iliyopita lakini residential licence aliyonayo ndugu yako imetolewa mwaka 2012, fuatilia huenda hiyo document ni batili

Fungua kesi baraza la ardhi na nyumba kwenye eneo lako. kuna gharama lakini haki yako itapatikana. Unaweza kuwaona NOLA kama huna uwezo wa kugharimia wakili.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana lakini Mkuu ningekua wewe wala nisinge taka ningezidi kumuomba mungu anipe changu,sisi tumezaliwa 13 matumbo mawili,upande wetu tuko 8 na mwengine 5 wao wenzetu ndio wakubwa mzee kufariki aliwacha nyumba 6
kwa upande wetu sie 8 watoto wa kiume ni 5 na kwa upande wa wale wakiume ni 1 basi kabla ya urithi tuliipata fresh,
Tuna lala usiku unashanga unakuta nyoka ndani ya shuka,ukienda jikoni unakuta nyoka kwenye sofa,na hapo wameshajua kama sie ndio tuna pata nyumba nyingi,tumesoma kisomo tuka muachia mungu,tatizo ya wale wenzetu shule zero walikata kusoma wakajua tutaadhirika,tulikuja kuzinunua nyumba zote kwao na sasa bila aibu watoto wao wanalelewa nakusomeshwa na sisi,chamsingi usigombanie mali usioichuma..
 
Mkuu achana nayo hiyo nyumba ya urithi tafuta yako,.... utaanza kuokota makopo bure shauri yako.
Ahsante kwa ushauri
Mimi walinikosakosa.
pole sana ndugu
Ila ndg yangu poposindege, Achana kabisa na mambo ya urithi kama vp pambana tu ujenge nyumba kwa jasho lako, watoto wengi wa Kitanzania wamelemaa na mali za urithi yaani kukicha wanaomba wazazi wao wafariki wagawane mali .
Ushauri mzuri ahsante ndugu
Kama kaka yako kaamua kukuzulumu, Mwachia Mungu and move forward .... Utaingia kwenye tabu! Ipo Siku Atajua amefanya dhuluma na kujirudi ila usipambane
Ni kweli anajua kama anadhulumu, ila hajali kitu
Huwa sijisikii happy kwa vitu vya urithi napamba nipate changu and will be proud of having my own assets
Ni kweli usemayo, lakini nina haki ya kurithi
Yaani brother ako wa damu anakudhulumu?
Ndio ni ndugu wa damu kabisa tena tumbo moja
Pole sana lakini Mkuu ningekua wewe wala nisinge taka ningezidi kumuomba mungu anipe changu,sisi tumezaliwa 13 matumbo mawili,upande wetu tuko 8 na mwengine 5 wao wenzetu ndio wakubwa mzee kufariki aliwacha nyumba 6
kwa upande wetu sie 8 watoto wa kiume ni 5 na kwa upande wa wale wakiume ni 1 basi kabla ya urithi tuliipata fresh,
Tuna lala usiku unashanga unakuta nyoka ndani ya shuka,ukienda jikoni unakuta nyoka kwenye sofa,na hapo wameshajua kama sie ndio tuna pata nyumba nyingi,tumesoma kisomo tuka muachia mungu,tatizo ya wale wenzetu shule zero walikata kusoma wakajua tutaadhirika,tulikuja kuzinunua nyumba zote kwao na sasa bila aibu watoto wao wanalelewa nakusomeshwa na sisi,chamsingi usigombanie mali usioichuma..
Naendelea kumuomba Mungu aniepushe kwa mabaya yote yanayoelekezwa kwangu
We lazima utakuwa ndiye kaka wa mtoa mada yule zulumati
Inawezekana ni yeye kaingia humu ha! ha! ha!
 
Ahsante Lusajo11 kwa ushauri mzuri
Maoni ya kwamba ntafanyiwa juju hayajanitisha ila yameniongoza ktkkufanya tahadhari zaidi.
Kuhusu residential licence iliyotolewa 2012 ni halali. Ni kwamba hizo leseni hutolewa bila ya masharti mengi na uthibitisho mwingi. Nilijaribu kupata maelezo kwa watu wa wizara ya ardhi walinambia kwamba hizo leseni zilitolewa kwa yule aliyejitambulisha kwamba yeye ndiye mmiliki wa nyumba bila ya kupata uthibitisho wa nyaraka zingine. Yaani walipopita ktk nyumba kwa zoezi la uandikishaji aliyejitambulisha kwamba ndiye mmiliki basi walimuandikisha yeye. Na hili ndio alilofanya ndugu yangu. Watu hao wa Ardhi walinambia zoezi hilo lilileta kesi nyingi kwa baadhi ya maeneo walipojitokeza watu zaidi ya mmoja kudai wamiliki wa nyumba moja. Kesi ya Mirathi ilishafunguliwa na mimi kuteuliwa kama msimamizi wa mirathi lakini kukawa na utata wa nani mmiliki halali wa nyumba kati ya baba yetu au kaka yangu. Utata huo tukaambiwa twende kwenye mahakama za juu ili kutatuliwa na kujulikana nani mmiliki halali kati ya marehemu baba yetu au kaka yangu. Tatizo lililopo documents za manunuzi ya nyumba alivyonunua baba yetu kaka yangu kazificha kama kupoteza ushahidi wa mmiliki halali wa mwanzo. Gharama za kufungua kesi baraza la ardhi na nyumba ni kiasi gani?
Pole sana ndugu poposindege naona watu waliopona kufanyiwa juju wamekutisha sana hadi umetokomea..

Unaweza kupata haki yako. Baada y mazazi wenu kufariki mlikaa kikao cha familia na kufungua jalada mahakamani kuteua msimamizi wa mirathi? Kama sio huyo ndugu yako anapata wapi haki ya kujigawia nyumba!

Umesema baba yenu amefariki miaka sita iliyopita lakini residential licence aliyonayo ndugu yako imetolewa mwaka 2012, fuatilia huenda hiyo document ni batili

Fungua kesi baraza la ardhi na nyumba kwenye eneo lako. kuna gharama lakini haki yako itapatikana. Unaweza kuwaona NOLA kama huna uwezo wa kugharimia wakili.
 
Ahsante Lusajo11 kwa ushauri mzuri
Maoni ya kwamba ntafanyiwa juju hayajanitisha ila yameniongoza ktkkufanya tahadhari zaidi.
Kuhusu residential licence iliyotolewa 2012 ni halali. Ni kwamba hizo leseni hutolewa bila ya masharti mengi na uthibitisho mwingi. Nilijaribu kupata maelezo kwa watu wa wizara ya ardhi walinambia kwamba hizo leseni zilitolewa kwa yule aliyejitambulisha kwamba yeye ndiye mmiliki wa nyumba bila ya kupata uthibitisho wa nyaraka zingine. Yaani walipopita ktk nyumba kwa zoezi la uandikishaji aliyejitambulisha kwamba ndiye mmiliki basi walimuandikisha yeye. Na hili ndio alilofanya ndugu yangu. Watu hao wa Ardhi walinambia zoezi hilo lilileta kesi nyingi kwa baadhi ya maeneo walipojitokeza watu zaidi ya mmoja kudai wamiliki wa nyumba moja. Kesi ya Mirathi ilishafunguliwa na mimi kuteuliwa kama msimamizi wa mirathi lakini kukawa na utata wa nani mmiliki halali wa nyumba kati ya baba yetu au kaka yangu. Utata huo tukaambiwa twende kwenye mahakama za juu ili kutatuliwa na kujulikana nani mmiliki halali kati ya marehemu baba yetu au kaka yangu. Tatizo lililopo documents za manunuzi ya nyumba alivyonunua baba yetu kaka yangu kazificha kama kupoteza ushahidi wa mmiliki halali wa mwanzo. Gharama za kufungua kesi baraza la ardhi na nyumba ni kiasi gani?

Kuhusu gharama, ingia kwenye website ya Wizara ya Ardhi zilibadilika mwaka 2012 nadhani. Ila ni affordable hata kwa mtu wa kawaida.

Kuhusu utata wa nani mmiliki kati ya mzee wenu na ndugu yako, ni suala la ushahidi tu. Kwa kuwa nyumba yenyewe ipo kwenye squater, andaa majirani waliokuwepo tangu zamani lakini muhimu zaidi yule aliyeuza nyumba kama utampata. Documents alizoficha zisikutishe ukikomaa utamkamata mahali tu. Kuna kesi za documents huwa zunakuwa complex zaidi ya hiyo ila haki inapatikana
 
Lusajo11 nashukuru sana kwa ushauri wako.
Ni kweli naweza kumbana sehemu. Kwa mfano ktk kesi
ya mirathi alileta documents za kuonesha umiliki wa awali
kabla ya kupata leseni ya makazi, ambazo tuligundua zina tatizo.
Ni kwamba zina risiti za kulipiwa ardhi kitu ambacho si sahihi kwani
kiwanja kinacholipiwa ardhi ni kile kilichopimwa wakati nyumba ipo Squater area.
Aidha pia tukagundua hizo risiti zinaonesha kiwanja kipo eneo tofauti na nyumba ilipo.
Nimeangalia website ya ARDHI kiasi cha kufungua kesi hakikuwekwa wazi.
Kuhusu gharama, ingia kwenye website ya Wizara ya Ardhi zilibadilika mwaka 2012 nadhani. Ila ni affordable hata kwa mtu wa kawaida.

Kuhusu utata wa nani mmiliki kati ya mzee wenu na ndugu yako, ni suala la ushahidi tu. Kwa kuwa nyumba yenyewe ipo kwenye squater, andaa majirani waliokuwepo tangu zamani lakini muhimu zaidi yule aliyeuza nyumba kama utampata. Documents alizoficha zisikutishe ukikomaa utamkamata mahali tu. Kuna kesi za documents huwa zunakuwa complex zaidi ya hiyo ila haki inapatikana
 
Last edited by a moderator:
Pigania haki yako brooo,usiogope vitisho vya kurogwa wala chochote. Muamini Mungu ingia kwenye mapambano. Utakuja dhulumiwa hata yako ya kujenga,je utaogopa kurogwa? Mimi sikubali kudhulumiwa niko tayari hata kutoa roho yako.
 
Nipo safarini poposindege, nikiridi nyumbani nafikiri next week ntakuchekia kwenye library yangu. However, gharama zenyewe ni ndogo ndogo sana haitazidi 200,000/-;

Pia naona uko smart, umeweza kuuona udhaifu kwenye utetezi wake, ni point muhimu. Muhimu zaidi ni kwamba madai yako kwa ujumla ni mazito kiasi kwamba ukienda kwenye baraza utasikilizwa hiyo sina shaka;

Kama kesi imeshaamuliwa usisahau kuomba nakala ya hukumu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom