Naelekea Wizarani kumkabidhi Waziri bodaboda na vyeti ili asote navyo mwezi mzima

Naelekea Wizarani kumkabidhi Waziri bodaboda na vyeti ili asote navyo mwezi mzima

Walivyo wapigaji hao viongozi wenyewe, bodaboda yako watauza, vyeti wataghushi na kutumia majina yako na kesi watakubambikia ya kuwa muahini.

Roma katuliza akili hasa kwenye huu wimbo.
 
Nimekuelewa mkuu, hawajamaa wakisha pata vyeo huwa wanasahau kilicho waweka ofisini, huropoka ropoka tu vitu ili wazidi kujinufaisha wao wakati upande wa pili tukiumia, kama yule mzembe wa kufikiri aliyependekeza mafuta yaongezwe bei.

Tozo na makato yaliyowekwa kwenye mafuta,umeme na miamala haoni vinatosha pamoja na tozo zote hizo bado kukopa mikopo mikubwa kupo,zaidi ya yote michango kibao mashule ya serikali,kuhamasishwa kujenga shule, maospitali bila kujali tozo walizo tutwisha na Kodi nyingiii zisizo onyesha tija yoyote zaidi ya kuongezwa ongezwa kila kukicha.

Tuliona vitu vikiwezekana bila kuumizwa awamu ya tano, japo yapo yaliyo tukera pia ikiwa udikteta ila mambo yalienda Kwa kasi sana ndani ya miaka mitano tu. Sibirini Watanzania waamke katika usingizi wa kuonewa.
Suluhisho la yote haya ni uchaguzi ujao kama tu wananchi wataacha kisikiliza maneno ya uraghai na vijizawadi vya vitenge na vijisenti vya mkopo kwa akina mama

Inahitaji akili kubwa kufungua akili za watanzania. Viongozi wanayachukulia maisha simple tu ilihali wanawaumiza wananchi wa kipato cha chini

Subiri ifike 2024, utaona vijimaendeleo watakavyovifanya ili kuteka akili za wananchi. Hapo ndipo utawaona wabunge majimboni wakishika chepe ili kutindua mifereji, wengine watapanda vibajaji wakidai wanazungukia kero za wananchi wao

Hii nchi ni ngumu sana. Wakihashiba makande, hurejea bungeni kuishawishi serikali ipandishe kodi huku wakibeua na kujamba ovyo
 
Back
Top Bottom