Nimekuelewa mkuu, hawajamaa wakisha pata vyeo huwa wanasahau kilicho waweka ofisini, huropoka ropoka tu vitu ili wazidi kujinufaisha wao wakati upande wa pili tukiumia, kama yule mzembe wa kufikiri aliyependekeza mafuta yaongezwe bei.
Tozo na makato yaliyowekwa kwenye mafuta,umeme na miamala haoni vinatosha pamoja na tozo zote hizo bado kukopa mikopo mikubwa kupo,zaidi ya yote michango kibao mashule ya serikali,kuhamasishwa kujenga shule, maospitali bila kujali tozo walizo tutwisha na Kodi nyingiii zisizo onyesha tija yoyote zaidi ya kuongezwa ongezwa kila kukicha.
Tuliona vitu vikiwezekana bila kuumizwa awamu ya tano, japo yapo yaliyo tukera pia ikiwa udikteta ila mambo yalienda Kwa kasi sana ndani ya miaka mitano tu. Sibirini Watanzania waamke katika usingizi wa kuonewa.