.umenikumbusha kijijini
ilikuwa tunasubiri hadi walale
kule wanamme wanakaa usiku wamekoka moto wanaota.
Basi nilikaa nimesubiri wazee wakalale nimgongee binti.
Nikawa nimejilaza kwenye jiwe kubwa
hadi nikapitiwa usingizi
nikaja kuamshwa na maji kama umande unanidondokea
ahamadi, nilipoamka kumbe ni fisi alikuwa ananichunguza kama nimekufa ale mzoga
nilikimbia nikawavamia walokuwa wanaota moto
baskeli yangu ilibidi ilale kichakani nilipokuwa nimepaki.
Dah, ujana maji ya moto.
Dah! Huu uzi ungeanzishwa kivyake