Naendelea kuomba, CCM itatoka uchaguzi mkuu wowote ujao 2025

Naendelea kuomba, CCM itatoka uchaguzi mkuu wowote ujao 2025

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Najua watu wenye Nia njema wamekua wakiomba kwa uwazi ama kwa kificho kuhusu haki mbalimbali za kisiasa hapa Tanzania.Mimi Ni mmojawapo niliyeomba kivyangu ili Mungu afanye mabadiliko bila vurugu Wala madhara.

Mambo Ni hatua kwa hatua.
Katika uchambuzi wangu pamoja na maombi naona yafuatayo 2025 au kabla ya hapo.

Mgombea wa chama au vyama vya upinzani atashinda Kama kawaida na safari hii atatangazwa kuwa mshindi na Tume ya Taifa ya uchaguzi.

CCM na Tume watajaribu kufanya figisu kutaka kupoka ushindi Kama walivyozoea lakini watazidiwa nguvu na jumuiya za kimataifa,taasisi za kimataifa,nchi jirani na nchi marafiki,watu wenye ushawishi duniani na ndani ya nchi.

Unajua kwa Nini ,Ni kwa sababu figisu za CCM dhidi ya upinzani zimeshawachosha.

Nguvu Za CCM zinaendelea kufungua,kwa sababu vijana wenye umri wa kupiga kura wataongezeka Sana,na wazee wanaoipenda CCM watakua wamekwisha kabisa.

Watu waelewa na wenye elimu ya uraia watakua wameongezeka Sana.

Vyama vya upinzani vitapata misaada ya HAKI ya uwazi na ukweli kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi kwa vyama rafiki na taasisi rafiki Kama ipatavyo CCM,lakini wapinzani watapata zaidi hata kutoka kwa vyama rafiki wa CCM.

Vyombo vya dola vitajiweka mbali na CCM kwa kuepusha lawama zinazoelekezwa kwao Kila Mara.

Viongozi wa Sasa wa CCM wenye Chuki Kali na Upinzani wataendelea Kula ngumi ya Mungu,Kama sio kuondoka kabisa basi ni kupoteza uwezo wa kufanya lolote kiafya.

Hali hii ya kuondoka Ni kutokana na ghadhabu ya Mungu kwa dhuluma wanazowafanyia wananchi juu ya kuchagua mtu wampendae,Mungu hapendi kabisa kuwanyang'anya watu haki yao ya kutawaliwa na mtu wamtakae.

Hii Ni chukizo kubwa mno kwa Mungu.Nadhani wote hamkutarajia.Sasa watakao shupaza shingo watafuata.wapo watakaoshituka na kujiweka mbali na dhuluma za uchaguzi.

Hadi kufika 2025 wapo wengi watapukutika kwa sababu watu waliomba na wanaendelea kuomba,nikiwa mmoja wao.

Wakubwa wa Dunia wameivumilia Sana CCM ,uvumilivu una mwisho.
Hii ni kwa hata marafiki wa jadi wa CCM wataitenga ikiwa tu itataka kufanya figisu.

Hatimae kwa Taabu sana CCM itafanya Kila hila ili iwemo kwenye serikali ya Upinzani na kulazimisha serikali ya Mseto.
Lakini baada ya miaka michache Sana itatoweka kabisa na kuwa chama dhaifu Cha Upinzani.

Jamani huu sio utabiri,haya Ni maono kutokana na maombi.

Mimi ni mwombaji,hata wewe unawezabkuomba kivyako kwani Mungu ni wa wote.
Mungu Hana dini.

Nitaitoa CCM peke yangu tu, kwa njia mbadala​

1 of 4Next Last
 
Amen..

Marekebisho kidogo. Siyo "uchaguzi mkuu wowote mwaka 2025" bali wakati wowote kuanzia sasa. Si lazima watolewe kwa uchaguzi hawa...

Njia yoyote inaweza kuwafuta kabisa. Hata ikibidi kwa COVID 19 mmoja baada ya mwingine until the whole evil circle is wiped out...

Nami naomba iwe hivyo hata kesho...

Obviously, tunasubiri nyakati na majira haya mapya kwa shauku kubwa..

Dalili ziko wazi sana. Kifo cha JIWE akiwa madarakani is one of the vital signs za haya mambo..

Wasipotubu sasa mwisho wao uko karibu sana...
 
Najaribu kuwaza huyo wa kuitoa ccm ni nani?

Chadema na yule belgiji?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Acheni kuchekesha jamani
 
Mimi Ni mmojawapo niliyeomba kivyangu ili Mungu afanye mabadiliko bila vurugu Wala madhara.
Kamanda naona unamtafuta Mungu lawama bure tu. Mungu atuondoe kwenye stability tulinayo, hata kama ina mapungufu, atupeleke kwenye chaos za vyama visivyo na kichwa wala miguu? Mungu ni wa utaratibu, hawezi kututoa kwenye stability na kutupeleka kwenye sintofahamu. Labda awe na makusudi maalumu, ambayo akitaka kuyatimiza atawafunulia manabii (watumishi wake). Lakini kwa sasa, Mungu anatuinua na kutupandisha juu.
 
Najaribu kuwaza huyo wa kuitoa ccm ni nani?

Chadema na yule belgiji?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Acheni kuchekesha jamani
Lisilowezekana kwa mwanadamu linawezekana kwa Mungu.
Mungu anajibu maombi ya watu waaminifu ndugu hata Kama muombaji Ni mdogo kama sisimizi akiomba kwa kumaanisha Mungu anasikia na anajibu.
Niliomba Mungu amejibu,ingawa najua na wengine waliomba kivyao.
Nina ushahidi humu.
 
Mungu hadhihakiwi ndugu.
Daudi alionekana dhaifu,so lolote so chochote mbele ya nduguze akichunga kondoo lakini Mungu akasema huyohuyo ndie atakua Mfalme.
Tatizo unaangalia mambo haya kwa macho ya kibinadamu na kisisasa.
Wewe unadhani Samia amekaa hapo kwa kwa bahati mbaya? yeye mwenyewe hakujua,wewe hukujua Jiwe hakujua ila Mimi nilijua kwa sababu niliomba nilimpa Mungu sababu zangu za kuomba mabadiliko hayo. Na amejibu.na bado nilisema mmoja baada ya mwingine.
Kamanda naona unamtafuta Mungu lawama bure tu. Mungu atuondoe kwenye stability tulinayo, hata kama ina mapungufu, atupeleke kwenye chaos za vyama visivyo na kichwa wala miguu? Mungu ni wa utaratibu, hawezi kututoa kwenye stability na kutupeleka kwenye sintofahamu. Labda awe na makusudi maalumu, ambayo akitaka kuyatimiza atawafunulia manabii (watumishi wake). Lakini kwa sasa, Mungu anatuinua na kutupandisha juu.
 
Amen..

Marekebisho kidogo. Siyo "uchaguzi mkuu wowote mwaka 2025" bali wakati wowote kuanzia sasa. Si lazima watolewe kwa uchaguzi hawa...

Njia yoyote inaweza kuwafuta kabisa. Hata ikibidi kwa COVID 19 mmoja baada ya mwingine until the whole evil circle is wiped out...

Nami naomba iwe hivyo hata kesho...

Obviously, tunasubiri nyakati na majira haya mapya kwa shauku kubwa..

Dalili ziko wazi sana. Kifo cha JIWE akiwa madarakani is one of the vital signs za haya semamambo..

Wasipotubu sasa mwisho wao uko karibu sana...
Ndio hivyohivyo unavyosema ndivyo nilivyomaanisha,Ni uandishi tu tofauti.
Mwenyezi Mungu Muumba mbingu na dunia kaamua.
 
Kwa mfano maombi yako yanakubaliwa,ni mpinzani gani ukimuangalia ana.akili ya kuongoza hili taifa?yaani ambaye sio mwizi,hana chuki/roho mbaya,ambaye hajipendekezi kwa watu weupe,ambaye si mropokaji,ambaye anaipenda kweli nchi yetu,ni nan?
 
Macho yako sio sawa na macho ya Mungu.

1. Msiba
2. Polepole
3. Makonda
4. Muro
5. Ole sabaya
 
Mungu hadhihakiwi ndugu.
Daudi alionekana dhaifu,so lolote so chochote mbele ya nduguze akichunga kondoo lakini Mungu akasema huyohuyo ndie atakua Mfalme.
Tatizo unaangalia mambo haya kwa macho ya kibinadamu na kisisasa.
Wewe unadhani Samia amekaa hapo kwa kwa bahati mbaya? yeye mwenyewe hakujua,wewe hukujua Jiwe hakujua ila Mimi nilijua kwa sababu niliomba nilimpa Mungu sababu zangu za kuomba mabadiliko hayo. Na amejibu.na bado nilisema mmoja baada ya mwingine.
Acha kumburuta Mungu kwenye porojo zako na tashwishi za kikamanda.
 
Back
Top Bottom