Nafanya biashara ya Miamala. Naombeni ushauri wenu

Nafanya biashara ya Miamala. Naombeni ushauri wenu

Nimeanza biashara ya miamala mwezi wa 9 na commission ya kwanza kwa mitandao yote mi4 (Tigo, Voda, halotel, na Airtel) ilikua 21 ila mwezi wa 12 nimeingiza commission ya 310,000 kwa mitandao yote mi4.

Usimvunje moyo, MWANZO MGUMU.

#YNWA
kwa mtaji wa sh ngapi? huyu tatizo lake usimamizi ni mdogo pia inawezekana hiyo biashara gaiko senta nzuli
 
Inategemea na sehemu alipo, mimi December nimepiga 400, 000 kwa tigopesa pekeake. Hapo bado voda, Artel na Halotel. Ubaya wa hizi biashara miezi haifanani
biashara yote ina msimu wake
 
Hao vijana ulio waajiri ndiyo wanakupiga. Na ukiweka mtaji mkubwa, wazee wa kazi nao watakutembelea (matapeli, vibaka, wezi, na majambazi).

Achilia mbali baadhi ya vibinti, na hata wamama wenye tamaa watakao jipitisha, ili kuifilisi kabisa hiyo ofisi.


NB:- Biashara inataka usimamizi wa karibu. Haitaki umwamini mtu/kijana kwa 100%.
wabongo tunafeli kwenye usimamizi hata serikalini wako hivio uvivu sana kuridhika starehe
 
Huwa sifungi huwa naangalia kamishen ya kila mwezi na kuwaelekeza vijana wanote hiyo ktk kitabu. mfano.
1. September kamishen 20,000/=
2. October 21,000/=
3. Novemba 21,500/=

kisha najumlisha na lile salio langu nililowekeza najua kiasi kinachoongezeka
Kwa style iyo lazima upate short, hesabu zinafungwa kila siku
 
Mi dukani kwangu kijana akizingua ni KWAO.
Sinaga masihala na hela.

Mi nina duka la vinywaji, wiki mbili zilizopita nilimkuta kijana anakunywa bia moja store, hapohapo nikafukuza na nilimpa 20,000 kwa huruma asepe nayo, maana ili Baki wiki uishe mwezi.

Usiwe na huruma kwa wasio na huruma na wewe.

#YNWA

Nimemshangaa jamaa anajiuliza Kama amuulize mwizi kma amemuibia [emoji28]
Piga chini Tafuta mwingine
 
Wanabodi biashara hii itaniua kwa pressure, tangia nimeianza sijawahi pata pesa zaidi napata hasara tu. Mara ya kwanza ni miezi mitatu iliyopita nimepata short ya 200,000/= leo nimechek nimekuta short ya 150,000/=

Hebu wajuzi wa mambo nishaurini, namna ya udhibiti.
Vijana wako wana laini za siri ndo wanapata faida kuliko wewe.yaani mnagawana wateja.

Sasa wawekee mtego kwa kutumia wateja wapya utawakamata
 
Fanya hivi kila siku jion fatilia mtaji wako uliweka sh ngap,kama ni 500k ikifika jion angalia salio kwenye simu (float) na cash walionayo vijana inapaswa ifike 500k ya mtaji,alaf waambie kitu ambacho sio lzma kuandika n ela ulotuma ukalipwa au alietoa ukampa ela lkn ulikotuma ela alaf hujapewa wajifunze kuandika huenda wanasahau,,
 
Sijui kwa nini wafanyakazi wengi wa serikalini wengi biashara huwashinda !
waajiriwa wanavituko yupo alikopa akafungua duka akamuweka mdogo wake vitutuko wakati wakilpa mapato hite akasubili mshahara hili aongezee [emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6]
 
waajiriwa wanavituko yupo alikopa akafungua duka akamuweka mdogo wake vitutuko wakati wakilpa mapato hite akasubili mshahara hili aongezee [emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6][emoji6]

Mbona mi nipo serikalini na Nina biashara na inasonga sasa.
ilianza na mtaji wa mil 6 sasa ina mil 20 na inaendelekea kukua.

#YNWA
 
Back
Top Bottom