Nafanya mazoezi sana ila nazidi kuongeza uzito zaidi, nitakuwa nakosea wapi?

Nafanya mazoezi sana ila nazidi kuongeza uzito zaidi, nitakuwa nakosea wapi?

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Nyie wataalam ni waongo mlionishauri mazoezi ati nitapunguza kilo kumbe ni uongo tu, badala ya kupunguza naongeza KGS

Najituma sana mazoezini, namwaga jasho ili nikate weight ila naona KGS ziziongezeka kuliko kabla sijaanza

Bora hata nisingepiga tizi sioni faida yoyote ya mazoezi
 
Unafanya mazoezi gani kama unanyanyua chuma uzito utaongezeka tu
 
Kupungua uzito kwa kufanya mazoezi ni ngumu sana. Kupunguza kula ndiyo njia pekee yenye mafanikio katika kupunguza uzito. Angalia mfano wa hii hesabu. Ukikimbia km 1 unaburn Kilo calories kama 60. Lakini ukipiga chupa ya pepsi unaingiza kilocalories kama 200. So inabidi ukimbie zaidi ya km 3 ili uburn calories kutoka kwenye pepsi ya buku. Utaona kuwa ni rahisi kutokunywa pepsi kuliko kukimbia km 3. Punguza kula.
 
Wanasema mazoezi husaidia 20% na chakula 80%.

Kwenye chakula pia kuna vitu vingi vya kuzingatia. Mimi siwezi kukushauri utumie vyakula gani bila kujua una slow au fast metabolism, una blood group gani? Jinsia gani? Umri gani? Unene wako ni wa kurithi (genetic) au umeutafuta mwenyewe kwa lifestyle yako.
Factors zinazosababisha usipungue ni nyingi na madaktari na wataalam wa lishe pekee ndio wanaweza kukusaidia
 
Back
Top Bottom