Chakula chakula chakula
Mazoezi yakuweka fit
Chakula kinajenga mwili.
Ushawahi kuona watoto wanakula zaidi ya watu wazima? Ni kwasababu wanajenga miili. Kila kitu kinakua, sasa wewe una miaka 35 na kuendelea, bado unakula kama kijana wa below (chini ya) 30 unategemea nini? Ni kwamba, mazoezi ndio yanaharakisha uchakataji wa misosi ulofakamia bila mpango.
Chakula chakula chakula.
Kwa vile tu una pesa, kila siku unaanza na supu na chapati, maziwa mayai, sukar kibao nk. Mchana nyama na mipilau jioni michemsho na ndizi. Je, mwili unahitaji yote hayo ukizingatia umeshaacha au umepungua kukua ulichobakisha ni kurudishia kinachopotea?
Chakula chakula chakula
Kuwa na nidhamu ya kula, fanya mazoezi kuweka fit viungo