Nafanya mazoezi sana ila nazidi kuongeza uzito zaidi, nitakuwa nakosea wapi?

Tafuta video za Prof janabi. Anakula chakula ambacho hakina wanga anakula jioni saa moja. Baada ya hapo anakuja kula kesho yake saa saba mchana. Siku nyingine hali kabisa anashindia maji, ukifanya hivyo miezi sita au 9 utakonda fasta
 
Ukiamua kufanya mazoezi ili kupunguza uzito unatakiwa ucontrol na ulaji wako,kawaida mazoezi ukifanya yanatengeneza hamu ya kula,sasa kama wewe unaitii hiyo hamu ya kula lazima utaongeza uzito...
 
atengeneze calorie deficit kwa kupunguza vitu vyenye nishati nyingi

sasa hapo sijui aende kwa mtaalam

na kuna vitu vingi vina nishati ila tunavipuuzia kama ugali, maharage nk...

maharage yana nishati kuliko chipsi
 
Sio kweli ukiwa serious na mazoezi wiki tu matokeo unayaona
 
Chakula chakula chakula

Mazoezi yakuweka fit
Chakula kinajenga mwili.

Ushawahi kuona watoto wanakula zaidi ya watu wazima? Ni kwasababu wanajenga miili. Kila kitu kinakua, sasa wewe una miaka 35 na kuendelea, bado unakula kama kijana wa below (chini ya) 30 unategemea nini? Ni kwamba, mazoezi ndio yanaharakisha uchakataji wa misosi ulofakamia bila mpango.

Chakula chakula chakula.

Kwa vile tu una pesa, kila siku unaanza na supu na chapati, maziwa mayai, sukar kibao nk. Mchana nyama na mipilau jioni michemsho na ndizi. Je, mwili unahitaji yote hayo ukizingatia umeshaacha au umepungua kukua ulichobakisha ni kurudishia kinachopotea?

Chakula chakula chakula

Kuwa na nidhamu ya kula, fanya mazoezi kuweka fit viungo
 
Me nina 98
Hizo Zipunguze zirud 90 to 88

Nakuambia hakuna zoezi zuri km kukimbia
Kwa wiki walau kimbia mara nne
Katika hizo siku nne kila siku hakakikisha umevunja km 7,8,9 au 10
Baada ya mwezi utaona mwili umeanza kukaza

Kuna bro alikuja uwanjan mwaka juzi ana uzito 103

Kwasasa ana 92 na ule mwili wa kike umeisha na amekaza fresh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…