Nafanyiwa figisu na wafanyabiashara wenzangu kwenye biashara yangu

Bandika bango kubwa "TUNAUZA JUMLA NA REJA REJA" kwa maelezo hayo una mtaji tumia redio za hapo kutangaza bidhaa zako kuwa unauza jumla na reja reja. Hao wapinzani wataanza kuwa wateja wako na bifu litapungua
 
Hapo dukani kwako chora picha ya dole la kati hao wafanyabiashara wenzako watajua uneshajua ujinga wao.
 
Nikwambie tu ukweli hakuna kitu kibaya kama kujifanya wewe unaonesha utofauti na wenzako kwenye bei......

Kiukweli unazingua kiasi mzee wewe uza sawa na wao.....discount zako ziwe siri kwa baadhi ya wateja la sivyo utaanguka vibaya.
 
Kama wewe sio mdigo wa Tanga Ni mtu wakuja, ondoka Tanga.
Utanishukuru baadaye.
Wadigo sio watu, wabondei Wana roho ya kwanini.
 
Hakuna mtu anaemlazimisha mtu mwingine namna ya kuishi lakini kwa uzoefu wangu mdogo wafanyabiashara wengi waliowahi kwenda kinyume na wafanyabiashara wengine kwenye eneo moja la biashara hawajwahi kufika mbali kibiashara hata siku moja.

Ngoja nikwambie kitu,hao wafanya biashara wenzako wakishirikiana wakaamua kushusha bei ya hivyo vinywaji zaidi ya bei unayouza wewe,let say wafanye hivyo kwa miezi sita mtawalia kwa lengo tu la kukuondoa wewe kibiashara ni inawezekana kabisa na wewe aidha ukahama hapo aua unganganie kukaa iliufilisike,yote ni machaguo yako.

Cha kukushauri tu uza bei za eneo husika lakini weka offers tofauti kwa wateja wako zitakazofanya waje kuchukua mzigo kwako kila mara au mara zote

Pia suala la kufikisha mzigo kwa wateja wako mapema pia inavuta sana wateja. Lakini hicho ulichokifanya ni kujichimbia kaburi kabisa.
 
Habari Wana jamiiforum.
Bila kuwachosha naenda kwenye mada moja kwa moja.

Nimejikamua Kama kijana nimeamua kufungua liquor store yangu mkoani Tanga ambayo inafanyakazi masaa 24 kila siku za wiki.
Sasa nauza vinywaji kwa bei ambayo Mimi napata faida
Mfano:-
Highlife -2000
Double kick -2000
Block Gin -2000
Hanson choice ndogo -3500
K vant ndogo -3500
Konyagi ndogo - 3500
K vant kubwa -9000
NK.

Sasa bei hizi zimefanya wafanya biashara wenzangu kuanza kuniundia figisu maana wao walikua wanauza Bei juu wanasema mimi nimewaharibia biashara zao.

Mfano wao huuza hivi
Double kick, Highlife na Black Gin kwa 3500
K vant ndogo, Hanson choice ndogo na konyagi ndogo kwa 5000.

Figisu wanazoniundia wafanya biashara wenzangu ni kama,
1. Kuniletea polisi
2. Imani za kishirikina, nikifungua ofisi nakuta hirizi mlangoni siku nyingine nakuta mayai yamepasuliwa au Nazi na makaratasi yaliyoandikwa Kama kiarabu hivi.
3. Kuniletea maafisa afya na TRA.
4. Kupanga vijana waniibie

Wakuu naombeni ushauri wenu kwa wazoefu wa biashara kipindi na nyakati Kama hizi ni zipi njia sahihi za kupita.
Nikisoma mwandiko wako sidhani kama una ujanja na akili nyingi kunisumbua. Wala huonekani unauweza umafia. Sasa sikia kijana mwenzangu achana na kusikiliza ushauri wa walimu wa chekechea na mafundi cherehani humu ambao hawajawahi fanya biashara. Sikiliza kutoka kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wenyewe. Kwa mwenendo wako huo ningekuwa huko na nafanya biashara hiyo nakuhakikishia usingechukua round.

Dunia nzima biashara ina siri zake na misingi yake, kwa taarifa yako mitandao ya simu inawasiliana na inajua inachokifanya dhidi yetu, Bakhresa na Mo Dewji wanaongea lugha moja kwenye baadhi ya vitu. Kibiashara vilevile Alikiba na Diamond kuna vitu wanakubaliana.
Mambo ya kwenda kienyeji kama mwendawazimu waachie wakulima (team manyanyaso), biashara haiendi hivyo.

Nadhani umesoma, unachokifanya sivyo ulimwengu wa kibepari unavyotaka. Fuatilia kwanini Airbus iliinunua kampuni chipukizi ya ndege ya Brazil, Embraer. Then kwanini Ulaya waliungana kutengeneza consortium ya Airbus, baadae kwanini Airbus iliinunua Bombardier ya Canada. Ndio maana kuna biashara zina monopoly au oligopoly, na wagumu wengine wakishindwa basi wanaunda genge (cartel).

Unakumbuka Dangote alipotaka kushusha sana bei ya simenti na kuuza bei moja mikoa yote walimfanyaje? Unakumbuka Halotel kipindi wameingia walikuwa na gharama za chini sana za vifurushi baadae wakafanywaje? That's sad reality of capitalism.

Ungekuwa mafia na "unajiweza" basi ningekuambia jipange kwa price war ila ninahisi hauko hivyo. Na penyewe price war ingekutoa sababu huna loyal customers, huna brand name kubwa hujazoeleka. Ungeshindikana kwenye kila kitu ungelazimisha washindani wako wakufuate washushe bei kama wewe au zaidi yako, tiyari ungeondoa ile advantage ya kupata wateja wengi kwa bei na ufirisike sababu unachukua faida kidogo sana, au muue hiyo biashara miaka michache muanze kushauri wengine kwamba"siku hizi unadhani huku kuna hela, huku hela ilikuwa zamani kipindi biashara haijavamiwa".

Na hata wasingekufanya kitu, bei za vinywaji nazijua, wewe umeshusha sana kwa ajili ya sifa za kijinga na kutafuta kuwa busy for nothing. Sababu ya kutokuwa na uzoefu hujui biashara ina kupanda na kushuka na pia ina uncertainties nyingi. Hivyo profit margin inabidi iwe kubwa ili kufidia nyakati nyeusi za biashara. Kwa mwenendo wako wewe ukipata black day moja tu kwenye biashara unachanganyikiwa.

Hapo shusha bei kidogo wenzako wanauza 5000 wewe uza 4500 ukizidi sana 4000, sasa wewe unavunja bei mpaka 3500 kwa ghafla tena wala sio gradually. Hapo kuna watu wamechukulia mikopo hiyo faida, unawaondoa kwenye mfumo kwa kufanya predatory pricing.
Hii hutumika na mabepari mapapa wakubwa kuondoa vidagaa. Hii hufanyika makusudi, na anayefanya hivyo hujua na anakuwa amekadiria possible action ambayo mpinzani atachukua. Wewe umeingia kwa predatory pricing ila unashangaa kama mkulima, huna uwezo nayo tumia mbinu nyingine.

Wasiwasi wangu ni kwamba umeingia kwenye soko bila mbinu sahihi za ushindani hivyo pricing strategy yako ni mbovu na haiko sustainable in the long run.

NB: Ushauri wangu ni wa kikatiri kwa mteja, ila ni sahihi na halisi kwa mfanyabiashara.
 
Mkuu chukua huu ushauri. Kama issue ilikuwa ni kutambulika tayari umeshatambulika kwa baadhi ya wateja.

Nenda kaongee na baadhi yao kuwa una adjust bei kwenda kama wao, weka na kisingizio kuwa ile ilikuwa kama promotion.

Kisha hizo bei utakuwa unatoa kama discount na zawadi kwa baadhi ya wateja.

Biashara zote ulimwenguni kuna muda zinakuwa kama vita. Afadhali hata matukio ya 'alarm' yamekukuta. Sehemu nyingine unafatwa physically unajeruhiwa mkuu.

Umeona hata mfano wa biashara ya watoa huduma za simu kama jamaa alivyokuambia hapo juu.
 
Imagine kama ume rent, nao wakiungana na kutoa wazo kwa mwenye nyumba kodi ikiisha watapachukua, ili wakuhamishe, nenda nao sawa man.
 
Lipa kodi ya serikali

Hayo mengine pambana nayo.
Ukielewana na serikali vitisho vingine ni minor
We mjaze tu, kwa uzoefu wangu wafanyabiashara wengi wa maeneo ya karibu huwa kama wana ushirikiano hivi upande wa bei, ukienda tofauti na wengi changamoto huwa zinakuwa nyingi sana.
 
Habari Wana jamiiforum.
Bila kuwachosha naenda kwenye mada moja kwa moja.

Nimejikamua Kama kijana nimeamua kufungua liquor store yangu mkoani Tanga ambayo inafanyakazi masaa 24 kila siku za wiki.
Sasa nauza vinywaji kwa bei ambayo Mimi napata faida
Mfano:-
Highlife -2000
Double kick -2000
Block Gin -2000
Hanson choice ndogo -3500
K vant ndogo -3500
Konyagi ndogo - 3500
K vant kubwa -9000
NK.

Sasa bei hizi zimefanya wafanya biashara wenzangu kuanza kuniundia figisu maana wao walikua wanauza Bei juu wanasema mimi nimewaharibia biashara zao.

Mfano wao huuza hivi
Double kick, Highlife na Black Gin kwa 3500
K vant ndogo, Hanson choice ndogo na konyagi ndogo kwa 5000.

Figisu wanazoniundia wafanya biashara wenzangu ni kama,
1. Kuniletea polisi
2. Imani za kishirikina, nikifungua ofisi nakuta hirizi mlangoni siku nyingine nakuta mayai yamepasuliwa au Nazi na makaratasi yaliyoandikwa Kama kiarabu hivi.
3. Kuniletea maafisa afya na TRA.
4. Kupanga vijana waniibie

Wakuu naombeni ushauri wenu kwa wazoefu wa biashara kipindi na nyakati Kama hizi ni zipi njia sahihi za kupita.
Aisee, pole sana.
 
Hizo bei ni za jumla au reja reja maana kama ni jumla bei iko juu hapa nikipo

Valuer Ndogo 2500
Konyagi Ndogo 3000

Yani kiufupi kuna tofauti ya 1000-1500 kwa kila Kinywaji
 
Back
Top Bottom