Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Nafarijika sana kuona wazee wakitumika kushauri masuala mbalimbali kwa sababu:
i) Wazee wanatoa maamuzi yaliyotulia
ii) Wazee hawakurupuki kwa sababu wanaongozwa na hekima
iii) Wazee wana uzoefu wa kutosha hivyo wanatumia uzoefu wao kutoa ushauri bora.
iv) Wazee hawana cha kupoteza kwamba atashauri ili alinde cheo chake. Hivyo ushauri wake unakuwa ni bora
Kama Taifa huko nyuma kama ni makosa yamewahi kufanywa ni kuacha kuwasikiliza wazee na mpaka ikafika vijana kama Ali Happi kuwakemea wakae kimya muda wao umeisha.
Taifa lilibarikiwa linaanza kwa kuwasikiliza wazee.
Natamani Rais Samia aende mbali zaidi kwa kuanzisha Baraza kuu la ushauri likiwahusisha marais wastaafu na viongozi wakuu wengine wa kitaifa wastaafu.