Nafasi mbili za kazi- Flydream Company Limited

Nafasi mbili za kazi- Flydream Company Limited

Manala An Academician

Senior Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
119
Reaction score
57
1. Utangulizi
Flydream Company Limited ni kampuni ya kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2019. Ni mujumuisho wa biashara zinazotoa huduma mbalimbali ikiwemo mafunzo ya Udereva, huduma ya ufundi Magari, Huduma za usafi na unyunyizishi wa dawa za kuua wadudu majumbani na maofisini, huduma za chakula, uuzaji wa viwanja vya makazi na biashara n.k.
Makao makuu ya ofisi yako Goba mnadani. Kampuni kwasasa imepanua wigo katika kuwafikia wateja wake na hivo kupelekea uhitaji wa wafanyakazi wawili katika nafasi zifuatazo.

A. Afisa mapokezi wa shule ya udereva-nafasi (01)
Sifa
1. Uwezo mzuri wa kuongea na watu mbalimbali ili waweze kujiunga na huduma zetu
2. Uwezo wa kufanyakazi yenye matokeo bila kusimamiwa
3. Uelewa zaidi katika kutafuta wateja kwa- njia ya mitandao ya kijamii
4. Nadhimu na mwenye muonekano mzuri mbele ya watu
5. Utayari wakuingia kazini kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 12:00 jioni kwa- kila siku isipokuwa jumapili au kutokana na sababu zingine anaweza kulazimika kufika siku ya jumapili pia
6. Elimu ni kidato cha nne mpaka cheti na uzoefu wa kazi hasa wa masoko na mauzo tutazingatia zaidi.

Mshahara.
Itakuwa ni TZS 300,000 kwa- mwezi kama atafikia malengo.
Pia atapata chakula cha mchana kwa- siku zenye mauzo.
Atapata bonus ya TZS 15,000 kwa- wiki kama atavuka lengo.
Atapata bonus ya TZS 10,000 kwa- wiki kama atafikia lengo.
Atakatwa TZS 2,000 kwa- kila mteja ambaye atakuwa amepungua katika kufikia lengo.

B. Customer care- nafasi (01)

Sifa
1. Mwenye lugha nzuri na yenye mvuto kwa- wateja
2. Ushawishi mzuri sana kwa- wateja
3. Uelewa katika matumizi ya mtandao yote ya kijamii katika kuifikisha huduma kwa- wateja
4. Uzoefu katika kazi za afisa masoko na mauzo utazingatia sana
5. Uzoefu katika kazi ya huduma kwa- wateja itakuwa ni sifa itakayopewa kipaumbele
6. Elimu ni kidato cha nne mpaka diploma katika kozi zinazoendana na nafasi husika

Mshahara
Itakuwa ni TZS 400,000 kwa- mwezi kama malengo yatafikiwa

utapata bonasi ya hadi TZS 15,000/- kwa- wiki kama lengo la wiki litavuka
Utapata TZS 10,000 kwa- wiki kama lengo litafikiwa
Utakatwa TZS 2,000/- kwa- kila mteja ambaye atakuwa amepungua kufikisha lengo

Mahali pakazi
Itakuwa ni moja kati ya vituo vya Goba, Tegeta au Mabibo ndani ya Dar Es Salaam

NB: Wenye sifa hapo juu watume CV zao kupitia email: manager@flydream.co.tz na kwa- WhatsApp namba 0765374146

Mwisho wa kutuma maombi ni Jumatano tarehe 19/10/2022 saa sita usiku
 
Ni mm tu ndio nimeona kazi moja imeandikwa mara mbili au ni uchovu wa usingizi
 
Huyu jamaa mbona kama anatafuta watu wa masoko tu yaani anatafuta watu wa kuzunguka kitaa waktafuta wateja. Na uwenda mshahara huo ni kamishen yan unalipwa kulingana na wateja watakaopatikana au mi ndo sielewi.
 
Ni mm tu ndio nimeona kazi moja imeandikwa mara mbili au ni uchovu wa usingizi
Uko sawa jamaa sjui anadhan humu kuna wapumbavu. Ameshndwa tu kufunguka kwamba ni kaz ya kamishen anatafuta watu wa masoko na wameweka kiwango cha wateja kwa mwez uspofksha lengo kwny mshahara wako wanakata 2000 may be umeambiwa wateja 250 kwa mwez we ukaleta 50 kwa mwez tafsiri yake chkua 2000 mara 2000 jbu ni lak 4 na mshara uliambiwa lak 3 maana yake una den la laki 1 hapo ni hatari sn sn. Hayo mengne aliyoandka ni porojo porojo tu hapo za kunasia wajinga wajinga. Eti nafasi 2 hapo ni anataka hata watu 100 maana kikubwa mlete wateja msipoleta hupati ktu na unaweza kuleta uspofkia lengo lao wakpga hesabu ya bk 2 kwa kchwa maana yake umepoteza hupati hata mia.
 
Yaani wewe ndio umenielewesha
Tangazo maelezo hayaeleweki nilikuwa nashangaa mapokezi na kutafuta wateja wapi na wapi
Aseme tu anataka watu wa masoko malipo kwa kamisheni
 
Humu siyo fb huu usanii wako peleka fb hata kylinda humu walipambana sana kupata angalau vichwa viwili vitatu bt kwa challenges za kufa mtu so not easy bro jipange sana kuleta kaz kwa usanii usanii utapgwa kama ngoma la dufu.
 
Interesting

Back
Top Bottom