Nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM ingekuwa inagombewa Wasira angepata kura au kuthubutu kugombea?

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM ingekuwa inagombewa Wasira angepata kura au kuthubutu kugombea?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Mitandaoni watu wote wanaonekana kutokukubaliana na Mzee Wasira 80yrs kuendelea kuwepo kwenye nafasi za juu za uongozi wa chama. Its like siyo maono ya wana CCM kuwa na viongozi hawa tena kwenye ngazi muhimu kama hizi kwani wanaleta mkwamo wa fikra kwa Gen Z ndani ya chama.

Ushukuriwe utaratibu wa sasa unaowataka wajumbe kupiga kura ya ndiyo kwa jina linaloletwa na mwenyekiti Contrary naamini ingekuwa inagombewa Wasira Mwenyewe asingekubali kuchukua fomu.

Je, kwanini chama kimeona ni wakati wa 80yrs?
 
Hana future yeyote na hatokua threat Kwa mwenyekiti kiujumla!

Samiah ameona hilo!

Wassira hawezi Gombea urais Wala hawezi shawishika kufanya hivyo na huo teuzi ni favor tu kwake kupata ulaji katika uzee wake!!

Kama kundi la kikwete lilikua linawinda hiyo nafasi Ili wafanikishe kile walichokiita "Labda mambo yaharibike sana" matumaini yamefifia sana !

Kama the state Bado Wana operation zao zile bas itabidi wazamishe meli na abiria wake kitu ambacho ni kigumu sana!!!

Kazi iendelee Kwa sasa!
 
Wasira a.k.a Tyson mzee wetu kwa umri wake angebakia nyumbani kulea wajukuu..

Ni muda wake kura pension na ku enjoy Maisha yaliyo bakia ya retirement.

Mzee wasira apumzike Sasa baada ya kutumikia awamu zote sita za maraisi wote sita wa JAMHURI ya TANZANIA na kuachia vijana wasukume hili gurudumu la taifaaa
 
Mitandaoni watu wote wanaonekana kutokukubaliana na Mzee Wasira 80yrs kuendelea kuwepo kwenye nafasi za juu za uongozi wa chama. Its like siyo maono ya wana CCM kuwa na viongozi hawa tena kwenye ngazi muhimu kama hizi kwani wanaleta mkwamo wa fikra kwa Gen Z ndani ya chama.

Ushukuriwe utaratibu wa sasa unaowataka wajumbe kupiga kura ya ndiyo kwa jina linaloletwa na mwenyekiti Contrary naamini ingekuwa inagombewa Wasira Mwenyewe asingekubali kuchukua fomu.

Je, kwanini chama kimeona ni wakati wa 80yrs?
Machawa na wapambe wa CCM kwisha habari yao, wamebaki kama mazezeta!
 
Hapo ndo uwashangae vijana wa CHADEMA wanaosema Mbowe kachoka. Ktk siasa wazee ndo wenye madini na wanakijua chama in and out. Sii hawa vijana wanaokimbilia siasa sababu ya kukosa ajira
 
Back
Top Bottom