Nafasi ya mume. . .

naomba wadada humu wajibu hoja za Husninyo...
 
Hus embu naomba unifafanulie hiyo maana kuna watu hata ukila nyama wakati kwake kapika maharage basi umejionyesha. Je mtu anatakiwa aishije ili asionekane anaishi kwa kujionyesha?

kujionesha ipo kidhamira zaidi lizzy na wengi wanaojionesha hufanya kwa matendo pamoja na kuongea. Kwa tuonaoishi uswahilini kauli kama "watanitambua" "watanikoma mwaka huu."..etc zinasikika sana.
 
mpaka dada waje kuleta maneno kuna jambo moja hapo

shule ndogo na kukosa kazi ya kufanya.......

ukitaka kumlinda mkeo,somesha dada zako
hakikisha wanapata kazi za maana.......

na somesha mkeo pia ikibidi........

Unafikiri madada wote wanaoleta maneno kwenye ndoa za kaka zao hawakusoma?
Wengine na elimu zao zilizoshiba, utakuta ni unafiki, chuki na kutaka kuonekana kwa wifi yao kua wao ndo wenye ndugu yao.
So swala la elimu au kazi huwa haliappy kabisa.
Kuna room mate wangu chuo, alikuwa na kaka yake ameoa, ktk mazungunzo yake na ndugu zake siku moja wakawa wanapanga mipango ya kutafutia kakayao mwanamke. Nikamuliza ananiambia hatumpendi tu wifi, siyo type ya kuolewa na kaka. Na likizo hii tumepanga kupeleka timbwilii, hadi aondoke mwenyewe.
Nilibaki mdomo wazi.
 
hilo tatizo lipo pande zote mbili,

baadhi ya wanaume dada zao wanapoingilia ndoa huwa kimya, anamwachia mke timbwili lake apambane nalo, anaweza kudai kuwa ni

1. mambo ya wanawake asiingilie,au anashindwa kufanya uamuzi kwa upendo alonao kwa ndugu zake na upendo kwa mkewe.

2. Baadhi ya wanawake wakorofi, wakiolewa ndo wanaonyesha makucha, hapa mume mpaka agundue tatizo damage inakua tayari kubwa
 


In blue; Haya mambo hayahitaji comfrotations.... inahitaji tu mtu kua mpole, mstaarabu BUT Firm. One akiwa Firm in matters ambazo ni haki na kweli ni rahisi kufika resolution kuliko akienda kasi ama kujidai ana hasira.

In Red: Mara nyiiingi nia ya mawifi kukuchokoa ni


  • kutaka ukose amani kabisa ndani ya ndoa yako.
  • ujitambue na kujiona sio wa maana kwa kaka yao.
  • Ikiwezekana wavunje ndoa na kumleta wanao ona afaa.

What to do.... Ni kazi saana for nature ya mawifi, tabia ya mawifi na circumtances hupishana from one case to the other... Mie naona la muhimu hapo ni kugangamala na kuonesha your worth, msimamo na kwmba you don't care (hata kama waumia)

In beige: I support you...
 
kujionesha ipo kidhamira zaidi lizzy na wengi wanaojionesha hufanya kwa matendo pamoja na kuongea. Kwa tuonaoishi uswahilini kauli kama "watanitambua" "watanikoma mwaka huu."..etc zinasikika sana.

Hahahaha hapo nimekupata Hus.
Sema kuna wengine hata kama huna mawazo ya kujionyesha kitendo cha wewe kula/kuvaa vizuri, kutumia elimu yako vizuri, kulea watoto wako kwa namna tofauti tayari ni kujionyesha. Hawa hamna namna ya kuwasaidia zaidi ya kuwaacha "walie tu".

Alafu swala la wakwe kutembelea hamna kusema wasije kabisa sio haki, ila kutotaka wahamie na hodi hodi za kila siku mimi naelewa. Hata ndugu zangu wenyewe sitotaka kila siku wawepo kwangu achilia mbali wakwe. Wakae makwao, tutembeleane mara chache basi. Sio watu mnakosa hata uhuru wa kuishi mpendavyo kisa hodi hodi.
 
tena ni upuuzi wa hali ya juu!

 

Duh!!
Kweli kuna watu wana matatizo!!
 

mimi kama kaka yako Husninyo nakujibu
mke wangu lazima 'ajimwage mwage nyumbani' kwake kama wewe unaona dharau tafuta nyumba yako...

na kama unaishi nyumbani kwangu ambako mke wangu ndie malkia wa nyumba
lazima habari zako zote azijue,usije kupewa mimba ukashindwa kusoma nikapoteza pesa nazotumia kukusomesha...


misiba na wagonjwa hawezi kwenda bila mimi kumruhusu....so sio kosa lake
na sio kila msiba unakwenda.....utaenda misiba mingapi mjini hapa....?.

ni lazima ajioneshe ili awaoneshe wale waliosema 'ningeshindwa kumtunza na kumpa furaha' how wrong walikosea
so muache aringe na kujionesha ni haki yake

na kuhusu nyinyi dada zangu kuja nyumbani..
hiyo ndo chanzo cha umbea na majungu....mimi mwenyewe sitaki...
mkiwa na shida mnifuate oficin....mke wangu ana haki ya kulala mmchana na kutazama tamthilia bila bughudha
na nyinyi mna haki hizo majumbani mwenu sawa????

so now umenisikia.......i hope utanielewa...
 
wazungu wanaita 'poverty culture'...
go figure that...
Hata mimi naona ni hivo tu. Kuna watu wanatoa mifano ya roho mbaya out of nowhere ila ukichunguza utaona tu kuna perception ya wrong wealth repartition hapo. wifi anaweza kua na pato lake ila kwa akili yake yeye pato la kaka ni la familia nzima (u-bin) ila ya kwake yeye ni yake (na mume wake, if applicable).
Akikuta umeng'ara anajua ni hela za kaka yao, hence hela yao.
 
Tunajisahau sote wawili. Mke anajisahau kuwa ni wajibu wake kumlinda mumewe dhidi ya nduguze, na mume pia kumlinda mkewe. Kila mtu abawajua ndugu zake vema, kuna mchoyo, mroho, m'mbeya, mwizi, mchafu, muhuni, mgomvi etc. Wakati mwingine ikibidi kumuomba radhi mwenza kwa niaba ya ndugu mkorofi hata kama ni mzazi wako ni muhimu kuhakikisha amani inakuwepo. Na kukemea ndugu zako mwenyewe. Tunashindwa kuelewa ukimkemea mama yako mwenyewe kwa adabu hataweka kinyongo kama akiambiwa na mkwewe. Ni culture ya ustaarabu tu, mbona kuna familia tunakemeana wenyewe manake tunajuana. Mtu akitaka kuweka wifi mezani mnamuanza yeye 'acha mambo ya watuuuu!'
 

Hahahahaha. . .
Ahsante Boss!! Ila hapo ataondoka amenuna mdomo kule. Naakifika aendako ataanza kusema kaka yake kalogwa.
 

Kweli tupu.
Mimi ndio maana nakazia mtu kumalizana na ndugu zake yeye. Inakua ngumu wao kukaidi kwasababu wamesikia toka kwa ndugu yao mwenyewe, tofauti na msemaji anapokua alieyeoa/olewa kwao.
 
Tatizo pia kuna wanawake wakishaolewa wanaanza kuonesha makucha yao. Hapo mwanaume aangalie ni upande upi wenye makosa na sio kumtetea mkewe hata kama anafanya upuuzi.

Umesema kweli dada'angu, nina wifi yangu huyo yupo home yaani siku akiamka saa 2 ujue kuna maajabu! Yeye mida yake ni saa 5 ndo anatoka chumbani kwake , chakula apikiwe ye kupika mpaka ajisikie!! Nguo zikichafuka utaona anawaita madogo ndo wafue yeye huyoo saluni! Dah......huwa namuonea huruma kaka'angu aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…