Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hus embu naomba unifafanulie hiyo maana kuna watu hata ukila nyama wakati kwake kapika maharage basi umejionyesha. Je mtu anatakiwa aishije ili asionekane anaishi kwa kujionyesha?
Sio kosa la elimu, ni kosa la pato. ni umasikini tu.
mpaka dada waje kuleta maneno kuna jambo moja hapo
shule ndogo na kukosa kazi ya kufanya.......
ukitaka kumlinda mkeo,somesha dada zako
hakikisha wanapata kazi za maana.......
na somesha mkeo pia ikibidi........
naomba wadada humu wajibu hoja za Husninyo...
khaaa! Jibu wewe.
haya subiri nikujibu
The first para hits home, no doubt about that.Ila bado haibadili the fact that YOU know your family better, na ni rahisi zaidi kwako wewe kuwaweka sawa kuliko watu ambao ni outsiders. Hivyo mimi bado naona umuhimu wa mwenye ndugu kuchukua jukumu la kuwaweka ndugu zake sawa ikiwa mwenzake hawezi/hataki.
Alafu unajua kwamba baadhi ya watu hawawezi comfrontations? Mtu kama huyu akichokonolewa atafanya nini? Mke anatakiwa kumsupport mume na mume mke, hivyo mmoja wao akiona ndugu zake wanamkosesha mwenzake raha ni jukumu lake kuwaweka sawa. Ikiwa mke anaweza kumalizana nao
SAFI, kama hawezi mume anatakiwa awajibike.
kujionesha ipo kidhamira zaidi lizzy na wengi wanaojionesha hufanya kwa matendo pamoja na kuongea. Kwa tuonaoishi uswahilini kauli kama "watanitambua" "watanikoma mwaka huu."..etc zinasikika sana.
ni upuuzi kuonesha dharau kwa wifi na wakwe hata kama unammiliki kaka yao.
Ni upuuzi kufatilia mambo ya wifi zako wakati yako hutaki yajulikane.
Ni upuuzi kutoshirikiana na wifi zako kwa matukio kama vile ya misiba au ugonjwa.
Ni upuuzi kupenda kuishi kwa kujionesha kwa wifi zako baada ya ndoa.
Ni upuuzi kukataza mawifi au wakwe wasije nyumbani kwako.
Ni upuuzi na ukosefu wa akili vile vile.
Unafikiri madada wote wanaoleta maneno kwenye ndoa za kaka zao hawakusoma?
Wengine na elimu zao zilizoshiba, utakuta ni unafiki, chuki na kutaka kuonekana kwa wifi yao kua wao ndo wenye ndugu yao.
So swala la elimu au kazi huwa haliappy kabisa.
Kuna room mate wangu chuo, alikuwa na kaka yake ameoa, ktk mazungunzo yake na ndugu zake siku moja wakawa wanapanga mipango ya kutafutia kakayao mwanamke. Nikamuliza ananiambia hatumpendi tu wifi, siyo type ya kuolewa na kaka. Na likizo hii tumepanga kupeleka timbwilii, hadi aondoke mwenyewe.
Nilibaki mdomo wazi.
ni upuuzi kuonesha dharau kwa wifi na wakwe hata kama unammiliki kaka yao.
Ni upuuzi kufatilia mambo ya wifi zako wakati yako hutaki yajulikane.
Ni upuuzi kutoshirikiana na wifi zako kwa matukio kama vile ya misiba au ugonjwa.
Ni upuuzi kupenda kuishi kwa kujionesha kwa wifi zako baada ya ndoa.
Ni upuuzi kukataza mawifi au wakwe wasije nyumbani kwako.
Ni upuuzi na ukosefu wa akili vile vile.
Hata mimi naona ni hivo tu. Kuna watu wanatoa mifano ya roho mbaya out of nowhere ila ukichunguza utaona tu kuna perception ya wrong wealth repartition hapo. wifi anaweza kua na pato lake ila kwa akili yake yeye pato la kaka ni la familia nzima (u-bin) ila ya kwake yeye ni yake (na mume wake, if applicable).wazungu wanaita 'poverty culture'...
go figure that...
Asante wifi, hapo pa kuambatana ndipo panaponisumbua mimi. Mtu utashindwaje kuwa upande wa mke/mumeo ikiwa sio yeye mwenye makosa? Eti kisa unaogopa kuonekana unachagua.Ofcourse unachagua, ungekua huchagui usingekua na familia yako binafsi.
Alafu huyo rafiki kama anaweza ahamie mbali na hao ndugu wa mke. Maana ukaribu nao ni kichochezi kibaya kweli.
haya subiri nikujibu
mimi kama kaka yako Husninyo nakujibu
mke wangu lazima 'ajimwage mwage nyumbani' kwake kama wewe unaona dharau tafuta nyumba yako...
na kama unaishi nyumbani kwangu ambako mke wangu ndie malkia wa nyumba
lazima habari zako zote azijue,usije kupewa mimba ukashindwa kusoma nikapoteza pesa nazotumia kukusomesha...
misiba na wagonjwa hawezi kwenda bila mimi kumruhusu....so sio kosa lake
na sio kila msiba unakwenda.....utaenda misiba mingapi mjini hapa....?.
ni lazima ajioneshe ili awaoneshe wale waliosema 'ningeshindwa kumtunza na kumpa furaha' how wrong walikosea
so muache aringe na kujionesha ni haki yake
na kuhusu nyinyi dada zangu kuja nyumbani..
hiyo ndo chanzo cha umbea na majungu....mimi mwenyewe sitaki...
mkiwa na shida mnifuate oficin....mke wangu ana haki ya kulala mmchana na kutazama tamthilia bila bughudha
na nyinyi mna haki hizo majumbani mwenu sawa????
so now umenisikia.......i hope utanielewa...
Tunajisahau sote wawili. Mke anajisahau kuwa ni wajibu wake kumlinda mumewe dhidi ya nduguze, na mume pia kumlinda mkewe. Kila mtu abawajua ndugu zake vema, kuna mchoyo, mroho, m'mbeya, mwizi, mchafu, muhuni, mgomvi etc. Wakati mwingine ikibidi kumuomba radhi mwenza kwa niaba ya ndugu mkorofi hata kama ni mzazi wako ni muhimu kuhakikisha amani inakuwepo. Na kukemea ndugu zako mwenyewe. Tunashindwa kuelewa ukimkemea mama yako mwenyewe kwa adabu hataweka kinyongo kama akiambiwa na mkwewe. Ni culture ya ustaarabu tu, mbona kuna familia tunakemeana wenyewe manake tunajuana. Mtu akitaka kuweka wifi mezani mnamuanza yeye 'acha mambo ya watuuuu!'
Tatizo pia kuna wanawake wakishaolewa wanaanza kuonesha makucha yao. Hapo mwanaume aangalie ni upande upi wenye makosa na sio kumtetea mkewe hata kama anafanya upuuzi.