SoC03 Nafasi yako mwajiriwa

SoC03 Nafasi yako mwajiriwa

Stories of Change - 2023 Competition

Vitalice

New Member
Joined
May 4, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Ukikubali kuajiriwa lazima ukubali unafanya kazi ili ulipie gharama za uendeshaji ikiwa pamoja na mshahara wako pia umtengenezee faida muajiri wako.

Muajiriwa-: Jitahidi Sana kutambua kuwa kadri unavyozidi kujituma kazini ndivyo unavyoongeza thamani yako katika ajira yako. Kujituma kwako kunaanda mazingira ya kufanya malipo yako yawe ya uhakika na kufanya ajira yako iendelee kuwa hai. Hakikisha unatambua kupitia kazi yako ndiko malipo yako yanakotoka. Kwa kutambua ivyo fanya kazi kwa kujituma ili ukuze jina la mwajiri wako, na kupitia kukua kwa brand ya mwajiri wako pia Brand yako itakua.

Kukua kwa brand yako kiuhalisia Ni thamani (CV) yako imekuwa ambayo itakupelekea kuongezeka kwa soko la huduma /ajira yako kwa. Kila taasisi au shirika linahitaji watu/mtu anaeweza kuifanya kazi kwa ufanisi wa Hali ya juu, kitu ambacho kinawafanya waweke masharti kwenye kuwatafuta watu hao kwa kupia vyeti vyao wakiamini kwa kuwa na mtu mwenye elimu ya juu ndio umepata muajibikaji la hasha.

Sikatai kuwa elimu Ina nafasi yake Ila kujitambua kilichokufanya kuajiriwa Ni upungungu wa huduma yako katika hicho kitengo na si upungufu wa mtu. Ukifahama hivyo itakupelekea kuonyesha ulicho nacho au kilichowaaminisha kuwa wewe ndiye unaefaa kuwepo hapo na hawajakosea kukuweka hapo.

Kwa mfano kwa utendaji wa Mtangazaji MAULIDI KITENGE kumefanya Kila chombo Cha habari kwa Sasa hapa Tanzania kuwa na hitajiko nae maana kuwa na mtu Kama yeye kunafanya taasisi kukua na Brand kukua pia. Kwa maana hiyo Sasa utendaji wa mtu ndio kinachohitajika katika taasisi au shirika lolote. Majina yote makubwa yametambulika kutokana na uajibikaji wao uliowafanya kutoka kusiko julikana Hadi kufikia kuwa watu maarufu duniani. Kujituma kwa Mcheza mpira Messi kumefanya kutambulika duniani kote. Kwa kutambua yote hayo kujituma Ni muhimu sana kwako na kwa unae mfanyia kazi.

IPENDE KAZI YAKO HESHIMU MIPAKA YAKO, MUHESHIMU ALIYEKUAJIRI MAANA AMEWEZA KUKUTUMIA WEWE ILI UMTENGENEZEE FAIDA, UMRUDISHIE GHARAMA ZA UWEKEZAJI NA ZA UENDESHAJI ZAIDI YA YOTE UJILIPE MSHAHARA MWENYEWE TENA KWA MSHAHARA ALIOUONA KUWA SAHIHI KWAKE.

MWAJIRI-: Heshima zako kwa kuwa na wazo na mtaji. Barikiwa maana unatufanya sisi tuishi mjini, tulipe kodi, ada na wazee vijijini waringe kuwa na vijana mjini. Tunaomba mutambue mchango wetu kwenye maendeleo yenu jamani. Angalau mnachotupa Kama malipo ya huduma/kazi zetu mtukadirie kuendana na Hali ya uchumi wa Sasa. Gharama ya maisha yamepanda mno Ila malipo yetu hayaendani na uhalisia kabisa.

inayopelekea si kwa kutaka kwetu Ila kwa kulazimishwa na Hali tunazeekea makazini na Sasa badala ya kuwajibika(kujituma ili kufanya ajira kuwa hai) inatulazimu kuwa MACHAWA ili kuzilinda ajira zetu. Msijisikie vibaya kutuandaa na sisi tupate mtaji maana MAWAZO TUNAYO MENGI, Ila mnachotulipa kinaishia kwenye mahitaji ya msingi tyuu.

Cha kusikitisha zaidi tumeajiriwa miaka kumi iliyopita lakini Hadi leo tyunaishi nyumba za kupanga, akiba zero, Ada tunadundukiza, chakula dagaa na mchicha ndio mboga za msingi, mavazi lazima tusubirie wazunguu wavai watuachie (mtumba).

Mnisamehe mabosi zangu sijawasema Ila nimeongea kinachotukuta wengi. MORALI YA KAZI ZIMEPUNGUA KUTOKANA NA HALI TUNAZOPITIA TUNAFANYA KAZI KWA MAZOEA NA KUKATISHWA TAMAA. Ninaomba kwa niaba ili mpate kumbukeni anayesababisha upate, wazo na mtaji havitoshi lazima huyu wa tatu nae atambulike na aheshimike.

Unaweza ukawa na wazo nzuri Sana na mtaji wa kutosha Ila ukikosa mtendaji (mfanyakazi) mzuri anayejituma na kuitambua nafasi yake vyote vitafaili. Ajira zimekuwa changamoto kwa sababu hatupeani vijiti/fursa. Umefanikiwa mwezeshe na mwenzako ili nae amwezeshe na mwenzake. Jisikie vibaya kumzeesha mwenzako akiwa Kama mfanyakazi wako na unajusifia umeishi nae vizuri. Jisikie kwa kuwaonyesha wenzako wakurugenzi waliopita kwenye mikono yako Kama wafanyakazi.

Mwisho Ila si kwa ulazima. Mwajiriwa simama katika nafasi yako ibrand taasisi/shirika kadri ya uwezo wako bila kujali kiasi Cha malipo unacholiowa Kama mshahara. Kwa kufanya Ivo kutafanya uiache alama isiyofutika na itakayokuwa motisha kwa watakaopita ulikopita. Furahia kuwa role model kwa wengine kwa mazuri uliyoyafanya katika kazi yako au kitengo chako.

==>Mwajiri tambua mchango wa mfanyakazi wako mtie moyo, mwonyeshe ulikopita asije akahisi umefika uliko kirahisi Ana wakati wa kujifunza kwako. Mfunze ili uje ujisifu kwa uhodari wake wakati atakapo kuwa mkurugenzi katika kampuni kubwa.
 
Upvote 1
"Muajiriwa-: Jitahidi Sana kutambua kuwa kadri unavyozidi kujituma kazini ndivyo unavyoongeza thamani yako katika ajira yako. Kujituma kwako kunaanda mazingira ya kufanya malipo yako yawe ya uhakika na kufanya ajira yako iendelee kuwa hai"

Fanya kwa bidii kujijenga, ila hakuna mahusiano kati ya thamani unayoileta kwenye ajira na unacholipwa
 
Back
Top Bottom