Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Siyo pote wanafanya hivyo,inabidi aende akaone wanafanyeje sehemu husika,kwetu sisi ilikuwa unafika-unaandika jina kwenye orodha,unawapatia vyeti then interview inaendelea.
Hii nchi yetu sote aende akaangalie utaratibu-kama itaruhusu azamie.
 
Nimetoka kwenye usahili swali lililonipiga chenga na kutatazika kwenye kujibu ni ; umepelekea sehemu kuna shida ya usafiri utafanyaje ? bado nusu niseme nitakodi bodaboda.
maswali ni mangapi? Tupia mengine tofauti na hilo
 
maswali ni mangapi? Tupia mengine tofauti na hilo
Maswali yanakua kama manne hivi matatu ya possible kama umesoma geography advance topic ya Population kipengele cha census hayawezi kukushinda hata mimi ningejibu bila hata kupata hints za possible maana nilipiga chabo kwenye foleni jamaa alikua na mkeka wa maswali na majibu Pdf mwengine kanote kwenye kidaftari kidogo huku akisoma.

Swali moja anapiga la kufikirisha ili kupima ubunifu wako na ukiwa na wenge unapotea kabisa mfano ;mtu akikataa , usafiri ukiwa shida , simu ikizima na mengineyo ya namna hayo o
 
Swali jingine ni..

Upo tayari kufanya hii kazi ya sensa bila malipo yoyote ikiwa jina lako limechagiliwa??
 
Swali jingine ni..

Upo tayari kufanya hii kazi ya sensa bila malipo yoyote ikiwa jina lako limechagiliwa??
Nacheka kwanza Alafu Najibu Mm Nimzalendo Ikitokea Hivyo nitakubali kwa Manufaa ya Nchi yangu lkn sidhani kama serikali inaweza kufanya Hivyo kwa Jambo Amabalo linafanyika kwa kila baada ya Miaka kumi hivyo Naamini serikali lzm Itawalipa watakaojitolea kufanya kazi.
 
Mimi ni form 4 anayejihic ana akili sana na uelewa mkubwa aniulize swal lolote kuhus technology. Tumechoka kudhalaulika
 
Majina ya waliochaguliwa ngazi ya kata katika halmshauri vipi yatatolewaje , kwa umma tujione. Kama tumo au hatumo ??
 
Ujuaji mwingi unaweza kukukosesha nafasi ndgu yangu, hayo maelezo yote ya nini wakati kuna wenzio 200+ wanasubiri huo usaili huko nje.

Jibu ndiyo nipo tayari.
 
Hivi makarani wanahitajika wangapi kwenye kitongoji kimoja?

Leteni data kamili tufanye tathmini kuwa kuna uwezekano wa kuchaguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…