Thanks God, nafasi hizi zimetangazwa na Utumishi na Secretariat ya ajira ya Utumishi itasimamia zoezi hili. Hali ilikuwa mbaya sana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na kwenda nyuma pale nafasi hizoi za ajira zilipokuwa zinatangazwa na mchakato mzima wa ajira kusimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Upendeleo ulikuwa ni mkubwa sana na ilifikia hatua ya kwamba mwaka 2008/2009 zaidi ya asilimia 80 waajiriwa wapya walikuwa ni wachaga walioajiriwa kupitia mchakato wa NAO (ndani). Kwenye hili sifa ilikuwa ni uchaga tu. Nadhani wale waliokuwa wakifanya shortlisting wanajua hili walipewa directives hizo. Habari hii iliwahi kuandikwa na gazeti la mtanzania lakini mpaka leo hakuna majibu yaliyotolewa na ofisi, ni aibu tupu.
Hilo halitoshi, utaona viongozi wake wakipayuka sana kutaka wapewe uhuru wa kuajiri na ku-fire. Lakini je, mnao mfumo mzuri wa kuhakikisha kila mtu mwenye sifa anapata nafasi? Au ni ubinafisi tu?
Ofisi, inatisha na aiendani na sifa ilizonazo, hasa pale tunapozungumzia upandishwaji wa vyeo (promotion) uchaga kwanza na kisha sifa zingine baadae. Wenzangu na mimi wasio wachaga hata ufanye kazi kwa kiasi gani chance ya kupata promotion ya kiurahisi ni ndogo sana. Hii ni sehemu ya ofisi ya umma itakayodidimizwa na ukabila na upendeleo uliovuka mipaka. Tusidanganyike na sifa inazozipata, kunawachache wanaumia sana na hata hakuna promotion wanazopata. Ni ukabila na upendeleo tu.
Waswahili walisema, ngoma ivumapo sana ipo siku itapasuka. Viongozi wenye ukabila na upendeleo wa NAO kama Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi Selina Lyimo, Athanas Pius Tarimo na wengine wote chini ya Bwana Utouh, tunawaasa kuwa waangalifu na wakweli katika yale mnayoyafanya.
Teuzi nyingi ni uchafu tu ndani ya ofisi, ni ukabila tu.
Nadhani ni muda muafaka kwa vyombo vingine vya uchunguzi vijaribu kupita na kufanyia uchunguzi suala hili, hali ni mbaya na muda si mrefu yatawashinda watu na itakuwa ni hatari kwa mfumo wetu wa usimammizi wa fedha na matumizi ya serikali.