Nafasi za kazi national audit office(nao)

Nafasi za kazi national audit office(nao)

Jamani mimi nina cheti sina transript bt nina provision result,je usipokuwa na transript nayo inamata,pliz advise kama vp niende mkoa nikakichukue
 
Tatizo la virus wizara ya Utumishi ni la muda mrefu saana. We need to escalate this labda ndio wataelewa
 
General lconditions
vii. Applicants for entry levels currently employed in the Public Service should not apply, they have to adhere to Government Circular Na. CAC. 45/257/01/D/140 issued 30th November 2010.

what does it say? kama inawezekana tuwekee hiyo Circular!
 
jamani mimi nina cheti na provision. transcript sina je nayo inamata,pliz advise kama vp nipige mkoa nikaichukue.

mkuu bila transcript sidhani kama utafikiriwa? kachukue transcript ndugu tuje tupambane kwenye mchujo/mtoano ...
 
jamani mi nina kazi niko benki nauliza vip hii kazi ya auditing inalipa sana niweze kuaply kwan huku nalipwa gross 579000 naombeeni ushauri
 
jamani mi nina kazi niko benki nauliza vip hii kazi ya auditing inalipa sana niweze kuaply kwan huku nalipwa gross 579000 naombeeni ushauri

kaka kule mshahara mdogo degree anapewa laki3 ila c unajua serikalini hatuangalii mshahara ni mwendo wa mishe na ufree mkubwa kuliko benk.
 
Thanks God, nafasi hizi zimetangazwa na Utumishi na Secretariat ya ajira ya Utumishi itasimamia zoezi hili. Hali ilikuwa mbaya sana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na kwenda nyuma pale nafasi hizoi za ajira zilipokuwa zinatangazwa na mchakato mzima wa ajira kusimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Upendeleo ulikuwa ni mkubwa sana na ilifikia hatua ya kwamba mwaka 2008/2009 zaidi ya asilimia 80 waajiriwa wapya walikuwa ni wachaga walioajiriwa kupitia mchakato wa NAO (ndani). Kwenye hili sifa ilikuwa ni uchaga tu. Nadhani wale waliokuwa wakifanya shortlisting wanajua hili walipewa directives hizo. Habari hii iliwahi kuandikwa na gazeti la mtanzania lakini mpaka leo hakuna majibu yaliyotolewa na ofisi, ni aibu tupu.

Hilo halitoshi, utaona viongozi wake wakipayuka sana kutaka wapewe uhuru wa kuajiri na ku-fire. Lakini je, mnao mfumo mzuri wa kuhakikisha kila mtu mwenye sifa anapata nafasi? Au ni ubinafisi tu?

Ofisi, inatisha na aiendani na sifa ilizonazo, hasa pale tunapozungumzia upandishwaji wa vyeo (promotion) uchaga kwanza na kisha sifa zingine baadae. Wenzangu na mimi wasio wachaga hata ufanye kazi kwa kiasi gani chance ya kupata promotion ya kiurahisi ni ndogo sana. Hii ni sehemu ya ofisi ya umma itakayodidimizwa na ukabila na upendeleo uliovuka mipaka. Tusidanganyike na sifa inazozipata, kunawachache wanaumia sana na hata hakuna promotion wanazopata. Ni ukabila na upendeleo tu.

Waswahili walisema, ngoma ivumapo sana ipo siku itapasuka. Viongozi wenye ukabila na upendeleo wa NAO kama Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi Selina Lyimo, Athanas Pius Tarimo na wengine wote chini ya Bwana Utouh, tunawaasa kuwa waangalifu na wakweli katika yale mnayoyafanya.

Teuzi nyingi ni uchafu tu ndani ya ofisi, ni ukabila tu.

Nadhani ni muda muafaka kwa vyombo vingine vya uchunguzi vijaribu kupita na kufanyia uchunguzi suala hili, hali ni mbaya na muda si mrefu yatawashinda watu na itakuwa ni hatari kwa mfumo wetu wa usimammizi wa fedha na matumizi ya serikali.
 
Ulimakafu nakubaliana nawe ya kwamba nafasi ni mia na mpambano wake utakuwa ni mkali sana.

Ila naamini ya kwamba ni vizuri mpambano uwe mkali na wa haki. Ofisi zetu za umma zinahitaji watendaji wazuri waliopatikana kupitia mchakato uliofanyika kwa haki na hivyo kuweza kupata watendaji wanaojiamini na kutenda kazi zao kwa haki pia.

Msingi wa utendaji mzuri kote duniani, ni jinsi gani afisa huyo wa umma anavyopatikana.
 
Back
Top Bottom