Jamii Opportunities
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 4,876
- 1,549
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA KUJITOLEA.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya inatangaza nafasi 45 za ajira ya kujitolea katika
Kada mbalimbali kama ifuatavyo;
I. Afisa Ugavi Daraja la Il (supplies Officer Il)- Nafasi 1
- Awe wenye Shahada/Stashahada ya juu ya ununuzi/Ugavi kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Au wenye "Professional Ievel III" inayotolewa na Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement and Supplies Professionals and Technicians
- Board —(PSPTB) au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na PSPTB, na kusajiliwa na PSPTB kama Procurement and Supplies Professional"
2. Mfamasia Daraja la II (Pharmacist II) — Nafasi 02
Sifa wenye Shahada ya Famasi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali aliyehitimu mafunzo ya vitendo kazini (Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi Tanzania.
3. Mteknolojia Madawa Daraja Il — Nafasi 1
Awe mwenye Stashahada katika fani ya uteknolojia Madawa ya muda wa miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi Tanzania.
4. Fundi Sanifu Vifaa tiba (Bio Medical technician) — Nafasi 1
Awe mwenye Stashahada katika fani ya Fundi Sanifu Vifaa Tiba (Bio Medical Technician) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
5. Watunza Kumbukumbu Wasaidizi Afya Daraja la Il — Nafasi 6
Awe na Astashahada/Stashahada ya utunzaji wa kumbukumbu katika masuala ya Afya (Medical Records) Kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
6. Dereva Daraja la Il — Nafasi 02
Awe wenye elimu ya kidato cha nne (IV) leseni class El, DI , CI awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda wa mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi wa kuendesha magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) au Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
7. Daktari Daraja la Il (Medical Doctors Il) — Nafasi 10
Sifa wenye Shahada ya Udaktari kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali, waliomaliza mafunzo ya utarajali "internship" ya muda usiopungua miezi kumi na mbili na kupata usajili katika Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
8. Afisa Muuguzi Il — Nafasi 7
Sifa wenye Shahada (Degree) ya Uuguzi, Kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, awe na leseni ya Uuguzi kutoka Balaza la Uuguzi na Ukunga Tanzania.
9. Afisa Muuguzi Msaidizi Il — Nafasi 02
Sifa wenye Stashada (Diploma) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali awe na leseni ya Uuguzi kutoka Balaza la Uuguzi na Ukunga Tanzania.
Mwenye sifa za ziada ikiwemo mafunzo ya cheti katika fani ya usingizi (Anaesthetist) atafikiriwa zaidi.
10. Muuguzi Daraja Il — 04
Sifa wenye Astashada (Cheti) ya Uuguzi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali awe na leseni ya Uuguzi kutoka Balaza la Uuguzi na Ukunga Tanzania.
11. Msaidizi wa Afya Maabara (Lab. Attendant) — Nafasi 01
Sifa mwenye Astashada (Cheti) ya Usaidizi Afya Maabara ya muda usiopungua mwaka mmoja (1) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
12. Mhudumu wa Afya Chumba cha Maiti (Mortuary Attendant) — Nafasi 01 Awe mhitimu wa kidato cha nne aliyepata mafunzo ya mwaka mmoja (1) katika fani ya Afya (Chumba cha Maiti)
13. Msaidizi wa Afya (Medical Attendant) — Nafasi 02
Awe mhitimu wa kidato cha nne aliyepata mafunzo ya mwaka mmoja (1) katika fani ya Afya kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
14. Afisa Hesabu Il (Accounts Officer) — Nafasi 01
Sifa awe na Shahada ya Sanaa/Biashara aliyejiimarisha kwenye fani ya Uhasibu au Stashahada ya juu ya uhasibu katika Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
15. Afisa Hesabu Msaidizi- Nafasi 01
Sifa awe na Stashahada ya Sanaa/Biashara aliyejiimarisha kwenye fani ya Uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu katika Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
16. Afisa uhusiano Daraja Il
Awe mwenye Shahada katika fani ya Sanaa ya Sayansi au aliyefuzu mafunzo ya awali ya Uandishi wa Habari (Mass Communication).
17. Katibu Muhtasi Daraja Il- Nafasi 01
Awe mwenye Elimu ya kidato cha Nne na mafunzo ya muda usiopungua mwaka mmoja k. katika fani ya "Secretarial Course" kutoka chuo au Taasisi inayotambuliwa na Serikali.
18. Mtunza Kumbukumbu Msaidizi Daraja la Il — Nafasi 01
Awe na Astashahada/Stashahada ya utunzaji wa kumbukumbu (Records Management) Kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kwa Mwombaji•
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
- Awe na cheti cha ufaulu cha kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI)
- Awe na Cheti cha taaluma husika
- Awe na cheti cha kuzaliwa (Birth Certificate).
- Ambatanishe wasifu wake (CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na wadhamini (Referee) watatu wa kuaminika.
- Awe na picha mbili (2) "passport Size" alizopiga hivi karibuni.
- Awe na Nakala ya kitambulisho cha Utaifa (NIDA).
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (NACTE na NECTA).
- Barua za uthibitisho/Matokeo ya mtihani (Testimonial/Provisional/ Statements of results) Havitapokelewa.
- Uwasilishaji na taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
- Malipo ya mshahara wa mwezi yatalipwa nusu mshahara kwa kuzingatia ngazi ya mshahara kwa kila kada husika (TGHS E, D, B, TGS B na D) na mikataba itakuwa kwa kipindi vya miezi kumi na mbili (12) kama muongozo unavyoelekeza.
Barua zote za maombi haya zitumwe/ziwasilishe kwa anuani ya; Mganga Mfawidhi
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,
S.L.P 259,
MBEYA.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 17 Februari, 2022 saa 9:30 Alasiri.
Imetolewa na;
Dkt. Alinanuswe Kasililika