Hii kitu ni ajabu lakini si ajabu.
Kwanza mnatakiwa kujua kwamba SUMA JKT imepewa dhamana ya kusimamia issues zote za vibarua ama kazi za muda zinazofanywa Bandarini na siyo TPA yenyewe na hata malipo ya vibarua hao yanapitia SUMA JKT kila siku baada ya masaa ya kazi.
Kazi hizo za muda ni kama;
1. Udereva (hawa ni wale wanaooa magari kwny meli na kuegesha kwny yard maalum za bandari)
2. Kuendesha mitambo (Kama fork lifts)
3. Makarani.
4. Wasio na fani (Hawa ni wale wa usafi wa mazingira ndani ya Bandari n.k)
Pili tangazo hilo limetolewa ukutani kwa kupigwa picha eneo ambalo vibarua huwa wanafanya mishe zao za kushughurikia vibarua eneo la ofisi ya SUMA JKT iliyopo pale TPA baada ya kuona njia ya kupeleka hard copies za vyeti na barua zinaumbua.
Siyo ajabu kwa SUMA JKT kama kampuni inayosimamia vibarua kutumia GMAIL.
Cha msingi na muhimu ni waombaji kutuma maombi yao na attachments.