Nafasi za kuteuliwa zinaondoa ufahamu na akili

Nafasi za kuteuliwa zinaondoa ufahamu na akili

Nikiwa nafuatilia jinsi hawa wateule wanafanya kazi nahisi wako kama watumwa. Kuna mda naona kabisa sisi ambao tuko kitaa tuna furaha na amani kuliko wao.

Kuna haja ya wateuzi kuwaambia wawe huru kwenye kazi zao. Mfano Rais anakuja kuzindua mradi uliobuniwa na kujengwa na mtangulizi wake, wateule wake wanajitutumua na kumwambia tunashukuru kwà juhudi zako

Hii huwa hainiingii akilini.

Mfano Mwingine ni pale mteuliea anaamua kudanganya umma ili amfurahishe mteuzi wake. Mfano mteule anashindwa kuwaambia mteuzi kwamba Tanzania Kuna uhaba wa madarasa, Madawati, na kwamba Maji Dar hayatoshi. Mnaishia kumsifia sifia tu hadi sisi Wana nchi tunashangaa jinsi mteule alivyopoteza uhuru wake.

Poleni wateule. Ila kwà nini huwa munakuwa hivyo?
Uhuru kwa Wateule uliisha Enzi za nyerere, yeye alikuwa akiwadhibiti Wateule na ili kumuenzi ndio ukaona hadi sasa Wateule mfano Majaji na Mahakimu Achana na hao wa majukwaani wanasiasa, bali uhuru wamekosa, ajabu na cha kushangaza ni kuwa wakati watanganyika wanapambana na ukoloni na kuhitaji uhuru Tulikuwa wa moja sasa hawa wabaguzi ndio wanapelekea utwana kwa ndugu zetu (wateule)
 
Back
Top Bottom