Nafasi za Wakuu wa Wilaya kwa siku nyingi zimenajisiwa sana

Nafasi za Wakuu wa Wilaya kwa siku nyingi zimenajisiwa sana

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Najua leo hii wengi wanapata utulivi baada ya kuona Sabaya akipandishwa kizimbani. Naiona hii haitoshi kwa sababu hatujaona mbele hukumu itakuwaje. Huenda itaibua mapya mengi na mengine yakiwahusu hao waliomtuhumu.

Shida yangu ni ubora duni wa wanaoteuliwa kushika nafasi hizo. Tatizo ni Serikali yetu kuifanya nafasi hiyo ya kujifunzia uongozi. Kwa nini tunateua watoto tunaowaita vijana wa CCM na kuwaweka kwenye nafasi nyeti kiasi hiki? Nafasi hizi za Wakuu wa Wilaya pamoja na wakurugenzi, ziliheshimika sana, tangu mkoloni, enzi ya kikwete nafasi hizo zikawa ni kujaribia uongozi.

Unawezaje kutoka chuo unapewa kuwa Mkuu wa Wilaya? Ally Hapi, Makonda, Jokate, n.k Waangalie matendo yao kwa Wananchi. Baadaye tunawasifu kwa shule moja tu ikijengwa wilayani. Ni shiiiida
 
Una hoja ya Msingi sana, lakini nani anajali?
 
Hoja kama hii inanikumbusha matendo ya Makonda yalivyoanza. Akateuliwa kuwa mkuu wa wilaya na Kikwete, Wakati wa mchakato wa katiba akamkaba mzee Warioba. Ajabu akateuliwa kushika nafasi ya juu na JPM, akawa mkuu wa mkoa. Sijui wahusika walitegemea kwamba sasa kakomaa kiuongozi!

Kuingiza wasio na uzoefu kushika nafasi ya ukuu wa wilaya ni aibu sana! Nafasi hiyo ina madaraka makubwa sana. Hata wale ambao hatujawasikia wakifanya mabaya, siyo kwamba wanaitendea haki nafasi hiyo inavyotakiwa, ni hali ya kulegea tu.
 
Back
Top Bottom